13-Sharh Asmaa Allaah Al-Husnaa Wa Swifaatihi: الرَّحْمنُ - الرَّحِيمُ - الْبَرُّ - الْكَرِيمُ - الْجَوَّادُ - الرَّؤُوفُ - الْوَاهَّابُ

Sharh Asmaa Allaah Al-Husnaa Wa Swifaatihi

 

(Maelezo Ya Majina Mazuri Ya Allaah Na Swiffah Zake)

 

Alhidaaya.com

 

الرَّحْمنُ - الرَّحِيمُ - الْبَرُّ - الْكَرِيمُ - الْجَوَّادُ - الرَّؤُوفُ - الْوَاهَّابُ

 

Allaah (سبحانه وتعالى), Majina yote haya yana maana yaliyokaribiana, na yote yanaelekeza katika kueleza sifa za Ar-Rabb kuwa na Rahmah na ukarimu. Zinaelekeza katika eneo kubwa la Rahmah yake na hadiya, tunuku inayokizunguka kila kilichopo, wanazopewa kwa mujibu wa amri za Yake. Waumini wamechaguliwa makhususi kwa ajili ya hili na wanapewa fungu zuri lililo bora katika haya, ni sawa na kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى):

 

 وَرَحْمَتِي وَسِعَتْ كُلَّ شَيْءٍ ۚ فَسَأَكْتُبُهَا لِلَّذِينَ يَتَّقُونَ وَيُؤْتُونَ الزَّكَاةَ وَالَّذِينَ هُم بِآيَاتِنَا يُؤْمِنُونَ ﴿١٥٦﴾

Na Tuandikie katika dunia hii mazuri na katika Aakhirah. Hakika sisi Na rahmah Yangu imeenea kila kitu. Basi Nitawaandikia wale wenye taqwa na wanaotoa Zakaah na ambao wao wanaziamini Aayaat (ishara, dalili) Zetu. [Al-A’raaf (7):156]

 

Allaah (سبحانه وتعالى), Baraka zote na namna mbali mbali za ukarimu zinatokana na athari ya Rahmah Yake na ukarimu kama ukarimu humu duniani na Aakhirah zinatokana na athari ya Rahmah Yake.

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

الرَّحْمَـٰنُ ﴿١﴾

Ar-Rahmaan.

 

عَلَّمَ الْقُرْآنَ ﴿٢﴾

Amefundisha Qur-aan.

 

خَلَقَ الْإِنسَانَ ﴿٣﴾

Ameumba insani.

 

عَلَّمَهُ الْبَيَانَ ﴿٤﴾

Amemfunza ufasaha. 

 

[Ar-Rahmaan (55): 1 - 4]

 

Na Anasema pia Allaah (سبحانه وتعالى):

=

إِنَّا كُنَّا مِن قَبْلُ نَدْعُوهُ ۖ إِنَّهُ هُوَ الْبَرُّ الرَّحِيمُ ﴿٢٨﴾

Hakika sisi tulikuwa kabla Tunamuomba Yeye Pekee, hakika yeye Ndiye Mwingi huruma na fadhila, Mwenye kurehemu. [At-Tuwr (52):28]

 

Na Anasema pia Allaah (سبحانه وتعالى):

يَا أَيُّهَا الْإِنسَانُ مَا غَرَّكَ بِرَبِّكَ الْكَرِيمِ ﴿٦﴾

Ee mwana Aadam! Nini kilichokughuri kuhusu Rabb wako Mkarimu? [Al-Infitwaar (82): 6]

 

 

Na Anasema pia Allaah (سبحانه وتعالى):

 

وَلَوْلَا فَضْلُ اللَّـهِ عَلَيْكُمْ وَرَحْمَتُهُ وَأَنَّ اللَّـهَ رَءُوفٌ رَّحِيمٌ ﴿٢٠﴾

Na lau si fadhila ya Allaah juu yenu na rahmah Yake, na kwamba Allaah ni Mwenye huruma mno, Mwenye kurehemu. [An-Nuwr (24): 20]

 

Na Anasema pia Allaah (سبحانه وتعالى):

 

رَبَّنَا لَا تُزِغْ قُلُوبَنَا بَعْدَ إِذْ هَدَيْتَنَا وَهَبْ لَنَا مِن لَّدُنكَ رَحْمَةً ۚ إِنَّكَ أَنتَ الْوَهَّابُ ﴿٨﴾

 (Husema): Rabb wetu, Usizipotoe nyoyo zetu baada ya kuwa Umetuhidi na Tutunukie kutoka kwako rahmah. Hakika Wewe ni Mwingi wa kutunuku na kuneemesha.  [Aali ‘Imraan (3):8]

 

 

 

Share