15-Sharh Asmaa Allaah Al-Husnaa Wa Swifaatihi: الْبَصِيرُ

Sharh Asmaa Allaah Al-Husnaa Wa Swifaatihi

 

(Maelezo Ya Majina Mazuri Ya Allaah Na Swiffah Zake)

 

Alhidaaya.com

 

الْبَصِيرُ

 

 

 

الْبَصِيرُ

Al-Baswiyr

Mwenye Kuona Yote Daima

 

 

 

Allaah (عز وجل), Anayeona vitu vyote hata visivyo muhimu na vidogo sana. Yeye (سبحانه وتعالى) Anamwona sisimizi mweusi juu ya jiwe jeusi katika usiku wa giza. Anakiona kilicho chini ya ardhi ya saba na kilicho juu ya mbingu ya saba. Pia Anawasikia na Anawaona wale wenye kustahiki jazaa, kwa mujibu wa amri na Hikma Yake.

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

قُلْ أَؤُنَبِّئُكُم بِخَيْرٍ مِّن ذَٰلِكُمْ ۚ لِلَّذِينَ اتَّقَوْا عِندَ رَبِّهِمْ جَنَّاتٌ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا وَأَزْوَاجٌ مُّطَهَّرَةٌ وَرِضْوَانٌ مِّنَ اللَّـهِ ۗ وَاللَّـهُ بَصِيرٌ بِالْعِبَادِ ﴿١٥﴾

Sema: Je, nikujulisheni yaliyo bora kuliko hayo? Kwa wale waliokuwa na taqwa kwa Rabb wao watapata Jannaat zipitazo chini yake mito, ni wenye kudumu humo na wake waliotakasika na radhi kutoka kwa Allaah. Na Allaah ni Mwenye kuwaona waja. [Aali ‘Imraan (3): 15]

 

Na pia Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

لَن تَنفَعَكُمْ أَرْحَامُكُمْ وَلَا أَوْلَادُكُمْ ۚ يَوْمَ الْقِيَامَةِ يَفْصِلُ بَيْنَكُمْ ۚ وَاللَّـهُ بِمَا تَعْمَلُونَ بَصِيرٌ﴿٣﴾

Hawatokufaeni jamaa zenu wa uhusiano wa damu, na wala watoto wenu Siku ya Qiyaamah (Allaah) Atapambanua baina yenu; na Allaah kwa yale myatendayo ni Mwenye kuona. [Al-Mumtahinah (60): 3]

 

 

 

Share