25-Sharh Asmaa Allaah Al-Husnaa Wa Swifaatihi: الْمُتَكَبِّرُ

Sharh Asmaa Allaah Al-Husnaa Wa Swifaatihi

 

(Maelezo Ya Majina Mazuri Ya Allaah Na Swiffah Zake)

 

Alhidaaya.com

 

  الْمُتَكَبِّرُ

 

 

الْمُتَكَبِّرُ

Al-Mutakabbir

Mwenye Kustahiki Kutakabari, Yuko Juu Ya Viumbe

 

 

 

Allaah (سبحانه وتعالى) ni Pekee mwenye kustahiki kutakabari, Aliye juu ya lolote ovu, lenye ila na upungufu kutokana na ukubwa Wake na utukufu.

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

هُوَ اللَّـهُ الَّذِي لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ الْمَلِكُ الْقُدُّوسُ السَّلَامُ الْمُؤْمِنُ الْمُهَيْمِنُ الْعَزِيزُ الْجَبَّارُ الْمُتَكَبِّرُ ۚ سُبْحَانَ اللَّـهِ عَمَّا يُشْرِكُونَ﴿٢٣﴾

Yeye Ndiye Allaah Ambaye hakuna Muabudiwa wa haki ila Yeye, Mfalme, Mtakatifu Ametakasika na sifa zote hasi, Mwenye kusalimisha na Amesalimika na kasoro zote, Mwenye kusadikisha ahadi na kuaminisha, Mwenye kudhibiti, kushuhudia, kuchunga na kuhifadhi, Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika, Jabari, Asiyeshindwa kufanya Atakalo, Mwenye ukubwa na uadhama, Subhaana Allaah! Utakasifu ni wa Allaah kutokana na ambayo wanamshirikisha. [Al-Hashr (59): 23]

 

 

 

 

 

 

Share