26-Sharh Asmaa Allaah Al-Husnaa Wa Swifaatihi: الْخَالِقُ - الْبَارِئُ - الْمُصَوِّرُ

Sharh Asmaa Allaah Al-Husnaa Wa Swifaatihi

 

(Maelezo Ya Majina Mazuri Ya Allaah Na Swiffah Zake)

 

Alhidaaya.com

 

الْخَالِقُ - الْبَارِئُ - الْمُصَوِّرُ

 

 

الْخَالِقُ

Al-Khaaliq

Muumbaji

 

 

الْبَارِئُ

Al-Baariu

Muumbaji Viumbe Kwa Maumbile

Yanayonasibiana Na Mazingira Ya Maisha Yao

 

 

 

الْمُصَوِّرُ

Al-Muswawwir

Muundaji Sura Na Maumbile

 

 

 

Allaah (سبحانه وتعالى) ni Pekee Aliyeumba vyote vilivyopo na Alivianzisha, Aliyekifanya kila kitu sawa na katika mahali pake kwa mujibu wa amri na Hikmah Yake. Aliyekitia umbo kila kitu Hikma Yake. Allaah (سبحانه وتعالى) Anaendelea kufanya hivyo.

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

هُوَ اللَّـهُ الْخَالِقُ الْبَارِئُ الْمُصَوِّرُ ۖ لَهُ الْأَسْمَاءُ الْحُسْنَىٰ ۚ يُسَبِّحُ لَهُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۖ وَهُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ﴿٢٤﴾

Yeye Ndiye Allaah, Muumbaji, Mwanzishi viumbe bila kasoro, Muundaji sura na umbile, Ana Majina Mazuri kabisa, kinamsabihi Pekee kila kilichokuweko katika mbingu na ardhi, Naye Ndiye Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika, Mwenye hikmah wa yote. [Al-Hashr (59): 24]

 

Na Anasema pia Allaah (سبحانه وتعالى):

 

 هُوَ الَّذِي يُصَوِّرُكُمْ فِي الْأَرْحَامِ كَيْفَ يَشَاءُ ۚ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ ﴿٦﴾

Yeye Ndiye Aliyekusawirini umbo katika matumbo ya uzazi vile Atakavyo. Hapana mwabudiwa wa haki ila Yeye, Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika, Mwenye hikmah wa yote. [Aal-‘Imraan: (3): 6]

 

 

 

 

 

Share