27-Sharh Asmaa Allaah Al-Husnaa Wa Swifaatihi: الْمُؤمِنُ

Sharh Asmaa Allaah Al-Husnaa Wa Swifaatihi

 

(Maelezo Ya Majina Mazuri Ya Allaah Na Swiffah Zake)

 

Alhidaaya.com

 

الْمُؤمِنُ

 

 

 

الْمُؤمِنُ

Al-Muumin

Mwenye Kusadikisha Ahadi, Mwenye Kuaminisha

 

 

 

Allaah (عز وجل) ni Pekee Aliyejisifia Mwenyewe kwa Sifa kamilifu na kwa ukamilifu wa utukufu na uzuri. Allaah (عز وجل) ni Pekee Aliyewapeleka Rusuli Wake na Akateremsha Vitabu Vyake pamoja na dalili na ushahidi dhahiri. Allaah (عز وجل) ni Pekee Anayeshuhudia ukweli wa Rusuli Wake kwa kuwapa kila dalili na ushahidi wa kuthibitisha ukweli wa kile walichokuja nacho.

 

Kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى):

 

هُوَ اللَّـهُ الَّذِي لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ الْمَلِكُ الْقُدُّوسُ السَّلَامُ الْمُؤْمِنُ الْمُهَيْمِنُ الْعَزِيزُ الْجَبَّارُ الْمُتَكَبِّرُ ۚ سُبْحَانَ اللَّـهِ عَمَّا يُشْرِكُونَ﴿٢٣﴾

Yeye Ndiye Allaah Ambaye hakuna Muabudiwa wa haki ila Yeye, Mfalme, Mtakatifu Ametakasika na sifa zote hasi, Mwenye kusalimisha na Amesalimika na kasoro zote, Mwenye kusadikisha ahadi na kuaminisha, Mwenye kudhibiti, kushuhudia, kuchunga na kuhifadhi, Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika, Jabari, Asiyeshindwa kufanya Atakalo, Mwenye ukubwa na uadhama, Subhaana Allaah! Utakasifu ni wa Allaah kutokana na ambayo wanamshirikisha. [Al-Hashr (59): 23]

 

 

 

 

 

 

Share