30-Sharh Asmaa Allaah Al-Husnaa Wa Swifaatihi: اللَّطِيف

Sharh Asmaa Allaah Al-Husnaa Wa Swifaatihi

 

(Maelezo Ya Majina Mazuri Ya Allaah Na Swiffah Zake)

 

Alhidaaya.com

 

اللَّطِيف

 

 

اللَّطِيف

Al-Latwiyf

Latifu, Mwenye Kudabiri Mambo Kwa Utuvu,

Mjuzi Wa Ya Dhihiri Na Ya Siri

 

 

 

Allaah (سبحانه وتعالى) ni Pekee Ambaye elimu Yake inakizingira siri zote na mambo yalifichikana, Allaah (سبحانه وتعالى) ni Pekee Ambaye Anayekijua vyema yote yaliyofichikana katika kina cha mbingu na ardhi na Anakijua kila kitu hadi chini mpaka utondoti mdogo wa chini kabisa.  Allaah (سبحانه وتعالى) ni Pekee Aliye mwema kwa waja Wake Waumini, Akiwaongoza kuelekea kwenye lililo na faida kwao na kuwasaidia kupitia njia wasizozijua, haya ni kwa Ukarimu na Ukarimu Wake. Jina hili linabeba pia maana za Al-Kabiyr na Ar-Rauwf.

 

Kauli Yake Allaah (سبحانه وتعالى):

 

لَّا تُدْرِكُهُ الْأَبْصَارُ وَهُوَ يُدْرِكُ الْأَبْصَارَ ۖ وَهُوَ اللَّطِيفُ الْخَبِيرُ ﴿١٠٣﴾

Macho hayamzunguki bali Yeye Anayazunguka macho yote; Naye ni Mwenye kudabiri mambo kwa ulatifu, Mwenye upeo wa khabari za dhahiri na za kufichika [Al-An’aam (6): 103]

 

Na Anasema pia Allaah (سبحانه وتعالى):

 

أَلَمْ تَرَ أَنَّ اللَّـهَ أَنزَلَ مِنَ السَّمَاءِ مَاءً فَتُصْبِحُ الْأَرْضُ مُخْضَرَّةً ۗ إِنَّ اللَّـهَ لَطِيفٌ خَبِيرٌ ﴿٦٣﴾

Je, huoni kwamba Allaah Ameteremsha kutoka mbinguni maji kisha ardhi ikawa chanikiwiti. Hakika Allaah bila shaka ni Mwenye kudabiri mambo kwa ulatifu, Mwenye upeo wa khabari za dhahiri na za kufichika. [Al-Hajj (22): 63]

 

 

 

 

Share