31-Sharh Asmaa Allaah Al-Husnaa Wa Swifaatihi: الْحَسِيبُ

Sharh Asmaa Allaah Al-Husnaa Wa Swifaatihi

 

(Maelezo Ya Majina Mazuri Ya Allaah Na Swiffah Zake)

 

Alhidaaya.com

 

الْحَسِيبُ

 

 

 

الْحَسِيبُ

Al-Hasiyb

Mwenye Kuhesabu, Kutosheleza

 

 

 

Allaah (سبحانه وتعالى) ni Pekee Ajuaye yote ya waja Wake na kuwatosheleza wanaomtegemea. Allaah (سبحانه وتعالى) ni Pekee Anayewalipa waja Wake ima wema au ubaya kwa hikma na elimu juu ya utondoti mdogo kabisa wa amali zao.

 

Kauli Yake Allaah (سبحانه وتعالى):

 

وَإِذَا حُيِّيتُم بِتَحِيَّةٍ فَحَيُّوا بِأَحْسَنَ مِنْهَا أَوْ رُدُّوهَا ۗ إِنَّ اللَّـهَ كَانَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ حَسِيبًا ﴿٨٦﴾

Na mtapoamkiwa kwa maamkizi yoyote, basi itikieni kwa yaliyo mazuri zaidi kuliko hayo au yarudisheni hayo hayo. Hakika Allaah daima ni Mwenye kuhesabu kila kitu. [An-Nisaa (4): 86]

 

Na pia Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

الَّذِينَ يُبَلِّغُونَ رِسَالَاتِ اللَّـهِ وَيَخْشَوْنَهُ وَلَا يَخْشَوْنَ أَحَدًا إِلَّا اللَّـهَ ۗ وَكَفَىٰ بِاللَّـهِ حَسِيبًا ﴿٣٩﴾

Wale wanaobalighisha ujumbe wa Allaah na wanamkhofu Yeye na wala hawamkhofu yeyote isipokuwa Allaah. Na Allaah Anatosheleza kuwa Mwenye kuhesabu. [Al-Ahzaab (33): 39]

 

 

 

Share