38-Sharh Asmaa Allaah Al-Husnaa Wa Swifaatihi: ذُو الْجَلاَلِ وَالإِكْرامِ

Sharh Asmaa Allaah Al-Husnaa Wa Swifaatihi

 

(Maelezo Ya Majina Mazuri Ya Allaah Na Swiffah Zake)

 

Alhidaaya.com

 

ذُو الْجَلاَلِ وَالإِكْرامِ

 

 

 

ذُو الْجَلاَلِ وَالإِكْرامِ

Mwenye Ujalali Na Ukarimu,

Mwenye Utukufu wa Juu Kabisa, Ukarimu Na Hadhi

 

 

 

 

Allaah (سبحانه وتعالى) ni Pekee  Mwenye ukuu, utukufu, Rahmah na ukarimu. Allaah (سبحانه وتعالى) ni Pekee Mwenye kuonyesha ukarimu katika nyanja zote mbili, jumla na mahsusi. Allaah (سبحانه وتعالى) ni Pekee Anayewapandisha hadhi marafiki Wake na walio karibu Naye.

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

كُلُّ مَنْ عَلَيْهَا فَانٍ ﴿٢٦﴾

Kila aliyekuwa juu yake (ardhi) ni mwenye kutoweka.

 

وَيَبْقَىٰ وَجْهُ رَبِّكَ ذُو الْجَلَالِ وَالْإِكْرَامِ ﴿٢٧﴾

Na utabakia Wajihi wa Rabb wako Mwenye Ujalali na Taadhima. [Ar-Rahmaan (55): 26-27]

 

Na Anasema pia Allaah (سبحانه وتعالى):

 

تَبَارَكَ اسْمُ رَبِّكَ ذِي الْجَلَالِ وَالْإِكْرَامِ ﴿٧٨﴾

Tabaarak, Limebarikika Jina la Rabb wako Mwenye Ujalali na Ukarimu. [Ar-Rahmaan (55): 78]

 

 

 

 

 

Share