39-Sharh Asmaa Allaah Al-Husnaa Wa Swifaatihi: الْوَدُودُ

Sharh Asmaa Allaah Al-Husnaa Wa Swifaatihi

 

(Maelezo Ya Majina Mazuri Ya Allaah Na Swiffah Zake)

 

Alhidaaya.com

 

 

الْوَدُودُ

 

 

الْوَدُودُ

Al-Waduwd

Mwenye Mapenzi Tele Halisi

 

 

 

Allaah (سبحانه وتعالى) ni Pekee Anayewapenda Manabii na Rusuli Wake na wafuasi wao, nao pia wanampenda. Yeye Allaah (سبحانه وتعالى) ni mpendwa wao zaidi kuliko kingine chochote. Nyoyo zao zimejazwa na mapenzi Kwake, ndimi zao mara huendelea kuwa na rutuba kwa kumhimidi Yeye na nyoyo zao mara zote zimevutwa Kwake kwa mapenzi, unyoofu na tawbah.

 

Kauli Yake Allaah (عز وجل):

 

وَاسْتَغْفِرُوا رَبَّكُمْ ثُمَّ تُوبُوا إِلَيْهِ ۚ إِنَّ رَبِّي رَحِيمٌ وَدُودٌ﴿٩٠﴾

Na ombeni maghfirah kwa Rabb wenu, kisha tubieni Kwake. Hakika Rabb wangu ni Mwenye kurehemu, Mwenye upendo halisi. [Huwd (11): 90]

 

Na Anasema pia Allaah (سبحانه وتعالى):

وَهُوَ الْغَفُورُ الْوَدُودُ ﴿١٤﴾

Naye ni Mwingi wa kughufuria, Mwenye upendo halisi. [Al-Buruwj (85): 14]

 

 

 

 

Share