43-Sharh Asmaa Allaah Al-Husnaa Wa Swifaatihi: جَامِعُ النَّاسُ

Sharh Asmaa Allaah Al-Husnaa Wa Swifaatihi

 

(Maelezo Ya Majina Mazuri Ya Allaah Na Swiffah Zake)

 

Alhidaaya.com

 

جَامِعُ النَّاسُ

 

جَامِعُ النَّاسُ

Jaami’un-Nas

Mwenye Kuwakusanya Watu

 

 

 

Allaah (سبحانه وتعالى) ni Pekee Atakayewakusanya watu katika Siku isiyo na shaka. Atakusanya amali na malipo yao na Hataacha hata jambo moja, kubwa au dogo, bali Atalihesabu. Atayakusanya pamoja masalia ya waliofariki, wa mwanzo na wa baadaye kwa nguvu yake kamilifu na elimu izungukayo yote,  na kuwafufua.

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

رَبَّنَا إِنَّكَ جَامِعُ النَّاسِ لِيَوْمٍ لَّا رَيْبَ فِيهِ ۚ إِنَّ اللَّـهَ لَا يُخْلِفُ الْمِيعَادَ ﴿٩﴾ 

Rabb wetu! Hakika Wewe ni Mkusanyaji watu Siku isiyo na shaka ndani yake. Hakika Allaah Havunji miadi. [Aali ‘Imraan (3): 9]

 

Na Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

لَا أُقْسِمُ بِيَوْمِ الْقِيَامَةِ﴿١﴾

Naapa kwa siku ya Qiyaamah.

 

وَلَا أُقْسِمُ بِالنَّفْسِ اللَّوَّامَةِ﴿٢﴾

Na Naapa kwa nafsi inayojilaumu sana.

 

أَيَحْسَبُ الْإِنسَانُ أَلَّن نَّجْمَعَ عِظَامَهُ﴿٣﴾

Je, anadhani insani kwamba Hatutoikusanya mifupa yake?

 

 

بَلَىٰ قَادِرِينَ عَلَىٰ أَن نُّسَوِّيَ بَنَانَهُ﴿٤﴾

Ndio! Tuna uwezo wa  kusawazisha sawasawa ncha za vidole vyake .

 

 [Al-Qiyaamah (75): 1-4]

 

 

 

 

 

 

 

Share