46-Sharh Asmaa Allaah Al-Husnaa Wa Swifaatihi: بَدِيعُ السَّمَوَاتِ وَالأَرْضِ

Sharh Asmaa Allaah Al-Husnaa Wa Swifaatihi

 

(Maelezo Ya Majina Mazuri Ya Allaah Na Swiffah Zake)

 

Alhidaaya.com

 

بَدِيعُ السَّمَوَاتِ وَالأَرْضِ

 

 

بَدِيعُ السَّمَوَاتِ وَالأَرْضِ

Badiy’us-Samaawaat Wal-Ardhw

Mwanzishaji Wa Mbingu Na Ardhi

 

 

 

Allaah (سبحانه وتعالى) ni  Muumbaji na Mwanzilishi wa mbingu na ardhi. Amefanya hivyo katika namna bora kuliko zote na kwa maajabu zaidi ya uumbaji, yote katika namna ya ajabu na kamilifu zaidi, umbo na upatanifu.

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

 بَدِيعُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۖ وَإِذَا قَضَىٰ أَمْرًا فَإِنَّمَا يَقُولُ لَهُ كُن فَيَكُونُ ﴿١١٧﴾

Mwanzilishi wa mbingu na ardhi. Anapokidhia jambo basi huliambia Kun! Basi nalo huwa. [Al-Baqarah (2): 117]

 

Na Anasema pia Allaah (سبحانه وتعالى):

 

بَدِيعُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۖ أَنَّىٰ يَكُونُ لَهُ وَلَدٌ وَلَمْ تَكُن لَّهُ صَاحِبَةٌ ۖ وَخَلَقَ كُلَّ شَيْءٍ ۖ وَهُوَ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمٌ ﴿١٠١﴾

Mwanzilishi wa mbingu na ardhi. Inamkinikaje kuwa Yeye Ana mwana na hali hana mke! Naye Ameumba kila kitu, Naye kwa kila kitu ni Mjuzi. [Al-An’aam (6): 101]

 

 

 

Share