50-Sharh Asmaa Allaah Al-Husnaa Wa Swifaatihi: الْمُبْدِئُ - الْمُعِيدُ

Sharh Asmaa Allaah Al-Husnaa Wa Swifaatihi

 

(Maelezo Ya Majina Mazuri Ya Allaah Na Swiffah Zake)

 

Alhidaaya.com

 

الْمُبْدِئُ - الْمُعِيدُ

 

الْمُبْدِئُ

Al-Mubdiu:

Mwanzishaji

 

 

 

الْمُعِيدُ

Al-Mu’iyd

Mrejeshaji

 

 

 

Allaah (سبحانه وتعالى) ni Pekee Ambaye Ameanzisha uumbaji wa wana Aadam ili Awajaribu nani kati yao ni mwenye ‘amali njema kabisa, kisha Atawakusanya Siku ya Qiyaamah na kuwafanyia hesabu kwa kuwalipa jazaa zao wale waliotennda wema na kuwaadhibu wale waliotenda maovu. Pia ni Yeye Allaah (سبحانه وتعالى) Pekee Ambaye Ameanzisha uumbaji wa ulimwengu na Akaumba kila kilichomo ndani ya dunia na Huendelea kuumba na kukariri uumbaji wa viumbe na vinginevyo.

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

إِلَيْهِ مَرْجِعُكُمْ جَمِيعًا ۖ وَعْدَ اللَّـهِ حَقًّا ۚ إِنَّهُ يَبْدَأُ الْخَلْقَ ثُمَّ يُعِيدُهُ لِيَجْزِيَ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ بِالْقِسْطِ ۚ وَالَّذِينَ كَفَرُوا لَهُمْ شَرَابٌ مِّنْ حَمِيمٍ وَعَذَابٌ أَلِيمٌ بِمَا كَانُوا يَكْفُرُونَ﴿٤﴾

Kwake ni marejeo yenu nyote. Ni ahadi ya Allaah ya kweli. Hakika Yeye Anaanzisha uumbaji, kisha Anaurejesha ili Awalipe kwa uadilifu wale walioamini na wakatenda mema. Na wale waliokufuru watapata kinywaji cha maji ya kuchemka, na adhabu iumizayo kwa yale waliyokuwa wakikufuru. [Yuwnus (10): 4]

 

Na Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

أَمَّن يَبْدَأُ الْخَلْقَ ثُمَّ يُعِيدُهُ وَمَن يَرْزُقُكُم مِّنَ السَّمَاءِ وَالْأَرْضِ ۗ أَإِلَـٰهٌ مَّعَ اللَّـهِ ۚ قُلْ هَاتُوا بُرْهَانَكُمْ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ ﴿٦٤﴾

Au nani Anayeanzisha uumbaji, kisha Anaurejesha; na nani anayekuruzukuni kutoka mbinguni na kwenye ardhi? Je, yuko mwabudiwa pamoja na Allaah? Sema: Leteni ushahidi wenu wa wazi mkiwa ni wakweli. [An-Naml (27): 64]

 

Na Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

إِنَّهُ هُوَ يُبْدِئُ وَيُعِيدُ ﴿١٣﴾

Hakika Yeye Ndiye Anayeanzisha asili (ya uumbaji) na Atayerudisha. [Al-Buruwj (85): 13]

 

 

 

 

Share