56-Sharh Asmaa Allaah Al-Husnaa Wa Swifaatihi: الْكَافِي

Sharh Asmaa Allaah Al-Husnaa Wa Swifaatihi

 

(Maelezo Ya Majina Mazuri Ya Allaah Na Swiffah Zake)

 

Alhidaaya.com

 

الْكَافِي

 

 

الْكَافِي

Al-Kaafiy

Aliyejitosheleza

 

 

 

Allaah (سبحانه وتعالى) ni Pekee Anayewatosheleza waja Wake katika kila kitu wanachokihitaji. Yeye Allaah (عز وجل) ni Pekee Anayewatosheleza, katika hali mahsusi, wanaomwamini Yeye na wanaomtegemea Yeye na wanahitaji mahitaji ya kidunia na ya kidini kutoka Kwake.

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

وَرَدَّ اللَّـهُ الَّذِينَ كَفَرُوا بِغَيْظِهِمْ لَمْ يَنَالُوا خَيْرًا ۚ وَكَفَى اللَّـهُ الْمُؤْمِنِينَ الْقِتَالَ ۚ وَكَانَ اللَّـهُ قَوِيًّا عَزِيزًا ﴿٢٥﴾

Na Allaah Akawarudisha nyuma wale waliokufuru kwa ghaidhi zao hawakupata kheri yoyote. Na Allaah Amewatosheleza Waumini vitani. Na Allaah daima ni Mwenye nguvu zote, Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika. [Al-Ahzaab (33): 25]

 

Na Anasema pia Allaah (سبحانه وتعالى):

 

أَلَيْسَ اللَّـهُ بِكَافٍ عَبْدَهُ ۖ وَيُخَوِّفُونَكَ بِالَّذِينَ مِن دُونِهِ ۚ وَمَن يُضْلِلِ اللَّـهُ فَمَا لَهُ مِنْ هَادٍ﴿٣٦﴾

Je, kwani Allaah si Mwenye kumtosheleza mja Wake? Na wanakutisha na wale wasiokuwa Yeye? Na ambaye Allaah Amempotoa basi hana wa kumwongoa. [Az-Zumar (39): 36]

 

 

Share