58-Sharh Asmaa Allaah Al-Husnaa Wa Swifaatihi: الْواسِعُ

Sharh Asmaa Allaah Al-Husnaa Wa Swifaatihi

 

(Maelezo Ya Majina Mazuri Ya Allaah Na Swiffah Zake)

 

Alhidaaya.com

 

الْواسِعُ

 

الْواسِعُ

Al-Waasi’u

Aliyeenea

 

  

 

Allaah (سبحانه وتعالى) Ndiye Pekee Aliyeenea kwa mujibu wa Sifa Zake na ubora na yote yanayomhusu. Haya ni kwa mtazamo kuwa hakuna wa kuweza kutaja moja kwa moja sifa Zake kama Anavyostahiki, bali Yeye Allaah (عز وجل) Yuko sawa na Alivyojisia Yeye Mwenyewe. Allaah (عز وجل) Aliyeenea katika utukufu, na mamlaka, Aliyeenea katika kutoa Rahmah na mema, mkubwa katika utukufu.

 

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

مَّثَلُ الَّذِينَ يُنفِقُونَ أَمْوَالَهُمْ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ كَمَثَلِ حَبَّةٍ أَنبَتَتْ سَبْعَ سَنَابِلَ فِي كُلِّ سُنبُلَةٍ مِّائَةُ حَبَّةٍ ۗ وَاللَّـهُ يُضَاعِفُ لِمَن يَشَاءُ ۗ وَاللَّـهُ وَاسِعٌ عَلِيمٌ ﴿٢٦١﴾ 

Mfano wa wale wanaotoa mali zao katika njia ya Allaah ni kama mfano wa punje moja ya mbegu iliyotoa mashuke saba, katika kila shuke kuna punje mia. Na Allaah Humzidishia Amtakaye; na Allaah ni Mwenye wasaa, Mjuzi wa yote. [Al-Baqarah (2): 261]

 

Na Anasema pia Allaah (سبحانه وتعالى):

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا مَن يَرْتَدَّ مِنكُمْ عَن دِينِهِ فَسَوْفَ يَأْتِي اللَّـهُ بِقَوْمٍ يُحِبُّهُمْ وَيُحِبُّونَهُ أَذِلَّةٍ عَلَى الْمُؤْمِنِينَ أَعِزَّةٍ عَلَى الْكَافِرِينَ يُجَاهِدُونَ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ وَلَا يَخَافُونَ لَوْمَةَ لَائِمٍ ۚ ذَٰلِكَ فَضْلُ اللَّـهِ يُؤْتِيهِ مَن يَشَاءُ ۚ وَاللَّـهُ وَاسِعٌ عَلِيمٌ ﴿٥٤﴾

Enyi walioamini! Yeyote atakayeritadi miongoni mwenu kutoka Dini yake, basi Allaah Ataleta watu (badala yao) Atakaowapenda nao watampenda; wanyenyekevu kwa Waumini, washupavu juu ya makafiri; wanafanya jihaad katika njia ya Allaah na wala hawakhofu lawama za mwenye kulaumu. Hiyo ni fadhila ya Allaah Humpa Amtakaye. Na Allaah ni Mwenye wasaa, Mjuzi wa yote. [Al-Maaidah (5): 54]

 

 

Share