59-Sharh Asmaa Allaah Al-Husnaa Wa Swifaatihi: الْهَادِي - الرَّشِيدُ

Sharh Asmaa Allaah Al-Husnaa Wa Swifaatihi

 

(Maelezo Ya Majina Mazuri Ya Allaah Na Swiffah Zake)

 

Alhidaaya.com

 

الْهَادِي - الرَّشِيدُ

 

 

الْهَادِي

Al-Haadiy

Mwenye Kuongoza

 

 

 

الرَّشِيدُ

Ar-Rashiyd

Mwenye Kuelekeza, Kuongoza

 

 

 

Allaah (سبحانه وتعالى) Ndiye Pekee Anayewaongoza na kuwaelekeza waja Wake kwenye yote ya manufaa na mbali na yenye kuwadhuru. Yeye Allaah (عز وجل) Ndiye Pekee Anayewafundisha kile wasichokijua hapo awali na Anawaongoza kwa mwongozo unaowahifadhi imara katika Swiraatw Al-Mustaqiym. (Njia iliyonyooka). Yeye Allaah (عز وجل) Ndiye Pekee Anayezitia msukumo nyoyo zao kwa taqwa na kuzifanya zitubie na kushikamana na amri Zake Allaah (عز وجل).

 

 

Jina la Ar-Rashiyd pia linabeba maana ya Al-Hakiym (Mwenye Hikmah). Yeye Allaah (عز وجل) ni Ar-Rashiyd katika Matendo Yake na Kauli Zake. Shariy’ah Zake zote ni nzuri, zimeongozwa vyema na zina Hikmah, pia uumbaji Wake una Hikmah.

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

وَكَذَٰلِكَ جَعَلْنَا لِكُلِّ نَبِيٍّ عَدُوًّا مِّنَ الْمُجْرِمِينَ ۗ وَكَفَىٰ بِرَبِّكَ هَادِيًا وَنَصِيرًا ﴿٣١﴾

Na hivyo ndivyo Tumemfanyia kila Nabiy adui miongoni mwa wakhalifu. Na Rabb wako Anatosheleza kuwa ni Mwenye kuongoza na Mwenye kunusuru. [Al-Furqaan (25): 31]

 

 

 

Share