60-Sharh Asmaa Allaah Al-Husnaa Wa Swifaatihi: الْحَقُّ

Sharh Asmaa Allaah Al-Husnaa Wa Swifaatihi

 

(Maelezo Ya Majina Mazuri Ya Allaah Na Swiffah Zake)

 

Alhidaaya.com

 

الْحَقُّ

 

 

الْحَقُّ

Al-Haqq

Wa Haki, Wa Kweli

 

 

 

Yeye Allaah (سبحانه وتعالى) ni wa Haki katika Nafsi Yake yote. Yeye Allaah (عز وجل) Ndiye muhimu kuliko vitu vyote. Yeye Ndiye anayehitajiwa na vitu. Allaah (عز وجل) Ana Sifa kamilifu. Yeye Ndiye Pekee hapo awali Aliyekuwa na sifa za utukufu, uzuri na ukamilifu mpaka sasa. Yeye Allaah (عز وجل) Ndiye Pekee aliyekuwa Mtukuka na hadi sasa.

 

 

Kauli Yake Allaah (عز وجل) ni kweli. Matendo Yake ni kweli, kukutana Naye ni kweli, Manabii Wake wake ni kweli, Vitabu vyake ni Kweli, Dini yake ni kweli, kumwabudu Yeye Peke Yake ni kweli, kila kinachomhusu Yeye ni kweli. Haya ni kwa sababu Allaah (عز وجل)  ndiye Kweli na vile wanavyoviomba ghairi Yake ni batili na kwasababu Allaah (عز وجل)  Ndiye wa juu kuliko wote, na Mkubwa Ametukuka kwa ‘Uluwa.

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

ذَٰلِكَ بِأَنَّ اللَّـهَ هُوَ الْحَقُّ وَأَنَّهُ يُحْيِي الْمَوْتَىٰ وَأَنَّهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ ﴿٦﴾

Hivyo ni kwa kuwa Allaah Ndiye wa Haki, na kwamba Yeye Anahuisha wafu, na kwamba Yeye juu ya kila kitu ni Muweza. [Al-Hajj (22: 6)]

 

Na pia Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

وَقُلِ الْحَقُّ مِن رَّبِّكُمْ ۖ فَمَن شَاءَ فَلْيُؤْمِن وَمَن شَاءَ فَلْيَكْفُرْ ۚ  

Na sema: Hii ni haki kutoka kwa Rabb wenu. Basi anayetaka aamini, na anayetaka akufuru.  [Al-Kahf (18): 29]

 

Na Anasema pia Allaah (سبحانه وتعالى):

 

فَذَٰلِكُمُ اللَّـهُ رَبُّكُمُ الْحَقُّ ۖ فَمَاذَا بَعْدَ الْحَقِّ إِلَّا الضَّلَالُ ۖ فَأَنَّىٰ تُصْرَفُونَ﴿٣٢﴾

Basi Huyo Ndiye Allaah, Rabb wenu wa haki. Na kuna nini baada ya haki ila upotofu? Basi wapi mnageuzwa? [Yuwnus (10): 32]

 

Na Anasema pia Allaah (سبحانه وتعالى):

وَقُلْ جَاءَ الْحَقُّ وَزَهَقَ الْبَاطِلُ ۚ إِنَّ الْبَاطِلَ كَانَ زَهُوقًا ﴿٨١﴾

Na sema: Haki imekuja, na ubatili umetoweka. Hakika ubatili ni wenye kutoweka daima. [Al-Israa (17): 81]

 

 

Share