074-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Upole, Umakini na Utaratibu

 

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

 

باب الحلم والأناة والرفق

074-Mlango Wa Upole, Umakini na Utaratibu

 

Alhidaaya.com

 

قَالَ الله تَعَالَى:

وَالْكَاظِمِينَ الْغَيْظَ وَالْعَافِينَ عَنِ النَّاسِ ۗ وَاللَّـهُ يُحِبُّ الْمُحْسِنِينَ ﴿١٣٤﴾ 

Na wanazuia ghadhabu, na wenye kusamehe watu. Na Allaah Anapenda wafanyao ihsaan. [Aal-'Imraan: 136]

 

خُذِ الْعَفْوَ وَأْمُرْ بِالْعُرْفِ وَأَعْرِضْ عَنِ الْجَاهِلِينَ ﴿١٩٩﴾

Shikamana na usamehevu, na amrisha mema na jiepushe na majahili. [Al-A;raaf: 199]

 

وَلَا تَسْتَوِي الْحَسَنَةُ وَلَا السَّيِّئَةُ ۚ ادْفَعْ بِالَّتِي هِيَ أَحْسَنُ فَإِذَا الَّذِي بَيْنَكَ وَبَيْنَهُ عَدَاوَةٌ كَأَنَّهُ وَلِيٌّ حَمِيمٌ﴿٣٤﴾

Na wala haulingani sawa wema na uovu. Lipiza (uovu) kwa ambalo ni zuri zaidi; tahamaki yule ambaye baina yako na baina yake kuna uadui, atakuwa kama ni rafiki mwandani.

 

وَمَا يُلَقَّاهَا إِلَّا الَّذِينَ صَبَرُوا وَمَا يُلَقَّاهَا إِلَّا ذُو حَظٍّ عَظِيمٍ﴿٣٥﴾

Na hapewi hayo isipokuwa wale waliovuta subira, na hapewi hayo isipokuwa mwenye fungu adhimu. [Fusw-swilat: 34 - 35]

 

وَلَمَن صَبَرَ وَغَفَرَ إِنَّ ذَٰلِكَ لَمِنْ عَزْمِ الْأُمُورِ﴿٤٣﴾

Na atakayevuta subira na akasamehe, hakika hilo bila shaka ni katika mambo ya kuazimiwa. [Ash-Shuwraa: 43]

 

 

Hadiyth – 1

وعن ابن عباس رضي الله عنهما ، قَالَ : قَالَ رسولُ الله  صلى الله عليه وسلم لأَشَجِّ عَبْدِ القَيْسِ : ((  إنَّ فيكَ خَصْلَتَيْنِ يُحِبُّهُمَا اللهُ : الْحِلْمُ وَالأنَاةُ )) رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwa Ibn 'Abbaas (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) ameseam: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alimwambia Ashajj 'Abdil-Qays: "Hakika wewe una sifa mbili anazozipenda Allaah: Uvumilivu na uthabiti na kuacha haraka." [Muslim].

 

 

Hadiyth – 2

وعن عائشة رضي الله عنها ، قالت : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : ((  إنَّ اللهَ رفيقٌ يُحِبُّ الرِّفْقَ فِي الأَمْرِ كُلِّه )) متفقٌ عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwa 'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Hakika Allaah ni Mpole na anapenda upole katika mambo yote." [Al-Bukhaariy, Muslim na Ahmad]

 

 

Hadiyth – 3

وعن عائشة رضي الله عنها ، قالت : أنَّ النبيَّ صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : ((  إنَّ اللهَ رَفِيقٌ يُحِبُّ الرِّفقَ ، وَيُعْطي عَلَى الرِّفق ، مَا لاَ يُعْطِي عَلَى العُنْفِ ، وَمَا لاَ يُعْطِي عَلَى مَا سِوَاهُ )) رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwa 'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) kuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Hakika Allaah ni Mpole, hivyo anapenda upole, na anatoa kwa upole asichotoa kwa ukali na wala kwa chengine chochote mbali na upole na ulaini." [Muslim]

 

 

Hadiyth – 4

وعن عائشة رضي الله عنها : أنَّ النبيَّ صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : ((  إنَّ الرِّفْقَ لاَ يَكُونُ في شَيْءٍ إِلاَّ    زَانَهُ ، وَلاَ يُنْزَعُ مِنْ شَيْءٍ إِلاَّ شَانَهُ )) رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwa 'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Hakika upole unafanya kitu kiwe kizuri, na pindi upole unapoondolewa katika kitu chochote isipokuwa uzuri wake huondoka." [Muslim]

 

 

Hadiyth – 5

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه ، قَالَ : بَال أعْرَابيٌّ في المسجدِ ، فَقَامَ النَّاسُ إِلَيْهِ لِيَقَعُوا فِيهِ ، فَقَالَ النبيُّ صلى الله عليه وسلم : ((  دَعُوهُ وَأرِيقُوا عَلَى بَوْلِهِ سَجْلاً مِنْ مَاءٍ ، أَوْ ذَنُوباً مِنْ مَاءٍ ، فَإنَّمَا بُعِثْتُمْ مُيَسِّرِينَ وَلَم تُبْعَثُوا مُعَسِّرِينَ )) رواه البخاري .

Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: Bedui mmoja alikojoa Msikitini, watu wakamsimamia ili kumpiga, Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: "Muacheni na mwagieni ndoo ya maji juu ya mkojo wake. Hakika nyinyi mmetumwa kurahisisha, wala hamkutumwa kufanya uzito." [Al-Bukhaariy]

 

 

Hadiyth – 6

وعن أنس رضي الله عنه ، عن النبيِّ صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : ((  يَسِّرُوا وَلاَ تُعَسِّرُوا ، وَبَشِّرُوا وَلاَ تُنَفِّرُوا )) متفقٌ عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwa Anas (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Rahisisheni wala msiyafanye uzito, na toeni bishara wala msifukuze." [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

Hadiyth – 7

وعن جريرِ بنِ عبدِ اللهِ رضي الله عنه ، قَالَ : سَمِعْتُ رسولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم ، يقولُ : ((  مَنْ يُحْرَمِ الرِفْقَ ، يُحْرَمِ الخَيْرَ كلَّهُ )) رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwa Jariyr bin 'Abdillah (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: "Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: "Anayeharimishiwa (kukosa) upole amekosa kheri zote." [Muslim].

 

 

Hadiyth – 8

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه : أنَّ رَجُلاً قَالَ للنبيِّ صلى الله عليه وسلم : أوْصِني . قَالَ : ((  لاَ تَغْضَبْ )) ، فَرَدَّدَ مِرَاراً ، قَالَ : ((  لاَ تَغْضَبْ )) رواه البخاري .

Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba mtu mmoja alimwambia Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Niusie." Akasema: "Usighadhibike." Akakariri mara nyingi. Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) Akasema: "Usighadhibike." [Al-Bukhaariy].

 

 

Hadiyth – 9

وعن أَبي يعلى شَدَّاد بن أوسٍ رضي الله عنه ، عن رسول الله صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : ((  إنَّ الله كَتَبَ الإحْسَانَ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ فَإذَا قَتَلْتُم فَأحْسِنُوا القِتْلَة ، وَإِذَا ذَبَحْتُمْ فَأحْسِنُوا الذِّبْحَةَ ، وَليُحِدَّ أَحَدُكُمْ شَفْرَتَه ، وَلْيُرِح ذَبِيحَتَهُ )) رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwa Abu Ya'laa Shaddaad bin Aws (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Hakika Allaah Ameamrisha Ihsaan (wema) kwa kila kitu. Kwa hivyo, mkiuwa uweni vizuri, na mkichinja chinjeni vizuri. Kila mmoja wenu akitie makali kisu chake, na akipunguzie uchungu kichinjwa chake." [Muslim].

 

 

Hadiyth – 10

وعن عائشة رضي الله عنها ، قالت : مَا خُيِّرَ رسول الله صلى الله عليه وسلم بَيْنَ أمْرَيْنِ قَطُّ إِلاَّ أَخَذَ أيْسَرَهُمَا ، مَا لَمْ يَكُنْ إثماً ، فَإنْ كَانَ إثماً ، كَانَ أبْعَدَ النَّاسِ مِنْهُ . وَمَا انْتَقَمَ رسول الله صلى الله عليه وسلم  لِنَفْسِهِ في شَيْءٍ قَطُّ ، إِلاَّ أن تُنْتَهَكَ حُرْمَةُ الله ، فَيَنْتَقِمَ للهِ تَعَالَى . متفقٌ عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwa 'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) amesema: "Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) hakupewa fursa ya kuchagua baina ya mambo mawili katu isipokuwa alichadua jepesi lao, madamu si dhambi, ikiwa ni dhambi huwa mbali nalo zaidi. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) hakulipiza kisasi kwa nafsi yake katika jambo lolote isipokuwa mipaka ya Allaah inapokiukwa, kwa hilo hulipiza kisasi kwa ajili ya Allaah Ta'aalaa." [Al-Bukhaariy na Muslim].

 

 

 

Hadiyth – 11

وعن ابن مسعود رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : ((  ألا أخْبِرُكُمْ بِمَنْ يَحْرُمُ عَلَى النَّار ؟ أَوْ بِمَنْ تَحْرُمُ عَلَيْهِ النَّار ؟ تَحْرُمُ عَلَى كُلِّ قَرِيبٍ ، هَيّنٍ ، لَيِّنٍ ، سَهْلٍ )) رواه الترمذي ، وقال : (( حديث حسن )) .

Imepokewa kutoka kwa Ibn Mas'uwd (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Niwajulishe nyinyi ambaye moto ni haramu kwake?. ni haramu kwa kila wa karibu, mwepesi, laini, mwepesi." [At-Tirmidhiy, na akasema ni hadiyth Hasan]

 

 

 

 

 

 

Share