075-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Kusamehe na Kupuuza Wajinga

 

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

 

باب العفو والإعراض عن الجاهلين

075-Mlango Wa Kusamehe na Kupuuza Wajinga

 

Alhidaaya.com

 

قَالَ الله تَعَالَى:

خُذِ الْعَفْوَ وَأْمُرْ بِالْعُرْفِ وَأَعْرِضْ عَنِ الْجَاهِلِينَ ﴿١٩٩﴾

Shikamana na usamehevu, na amrisha mema na jiepushe na majahili. [Al-A'raaf: 199]

فَاصْفَحِ الصَّفْحَ الْجَمِيلَ﴿٨٥﴾

Basi samehe msamaha mzuri. [Al-Hijr: 85]

 

وَلْيَعْفُوا وَلْيَصْفَحُوا ۗ أَلَا تُحِبُّونَ أَن يَغْفِرَ اللَّـهُ لَكُمْ ۗ  ﴿٢٢﴾

Na wasamehe na waachilie mbali. Je, hampendi Allaah Akughufurieni? [An-Nuwr: 22]

وَالْعَافِينَ عَنِ النَّاسِ ۗ وَاللَّـهُ يُحِبُّ الْمُحْسِنِينَ ﴿١٣٤﴾ 

Na wenye kusamehe watu. Na Allaah Anapenda wafanyao ihsaan. [Aal-'Imraan: 134]

وَلَمَن صَبَرَ وَغَفَرَ إِنَّ ذَٰلِكَ لَمِنْ عَزْمِ الْأُمُورِ﴿٤٣﴾

Na atakayevuta subira na akasamehe, hakika hilo bila shaka ni katika mambo ya kuazimiwa. [Ash-Shuwraa: 43]

 

 

Hadiyth – 1

وعن عائشة رضي الله عنها : أنها قالت للنبي صلى الله عليه وسلم : هَلْ أتَى عَلَيْكَ يَوْمٌ كَانَ أشَدَّ مِنْ يَوْمِ أُحُدٍ ؟ قَالَ : ((  لَقَدْ لَقِيتُ مِنْ قَوْمِكِ ، وَكَانَ أشَدُّ مَا لَقيتُ مِنْهُمْ يَوْمَ الْعَقَبَةِ ، إذْ عَرَضْتُ نَفْسِي عَلَى ابْنِ عَبْدِ يَالِيْلَ بْنِ عَبْدِ كُلاَلٍ ، فَلَمْ يُجِبْني إِلَى مَا أرَدْتُ ، فَانْطَلَقْتُ وَأنا مَهْمُومٌ عَلَى وَجْهِي ، فَلَمْ أسْتَفِقْ إِلاَّ وأنَا بِقَرْنِ الثَّعَالِبِ ، فَرَفَعْتُ رَأْسِي ، وَإِذَا أنَا بِسَحَابَةٍ قَدْ أظَلَّتْنِي ، فَنَظَرْتُ فَإذَا فِيهَا جِبريلُ (عليه السلام) ، فَنَادَاني ، فَقَالَ : إنَّ الله تَعَالَى قَدْ سَمِعَ قَوْلَ قَوْمِكَ لَكَ ، وَمَا رَدُّوا عَلَيْكَ، وَقَد بَعَثَ إلَيْكَ مَلَكَ الجِبَالِ لِتَأْمُرَهُ بمَا شِئْتَ فِيهِمْ . فَنَادَانِي مَلَكُ الجِبَالِ ، فَسَلَّمَ عَلَيَّ ، ثُمَّ قَالَ : يَا مُحَمَّدُ إنَّ اللهَ قَدْ سَمِع قَوْلَ قَوْمِكَ لَكَ ، وَأنا مَلَكُ الجِبال ، وَقَدْ بَعَثَنِي رَبِّي إلَيْكَ لِتَأْمُرَنِي بِأَمْرِكَ ، فَمَا شِئْتَ ، إنْ شئْتَ أطْبَقْتُ عَلَيْهِمُ الأَخْشَبَيْنِ )) . فَقَالَ النبي صلى الله عليه وسلم : ((  بَلْ أرْجُو أنْ يُخْرِجَ اللهُ مِنْ أصْلاَبِهِمْ مَنْ يَعْبُدُ اللهَ وَحْدَهُ لاَ يُشْرِكُ بِهِ شَيْئاً )) متفقٌ عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwa 'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) kuwa alimuuliza Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Je umefikwa na siku ngumu zaidi kuliko siku ngumu zaidi kuliko siku ya Uhud?" Akasema: "Hakika nimekutana na watu wako, na ilikuwa ngumu zaidi kutoka kwao kuliko siku ya 'Aqabah, siku hiyo nilijipeleka kwa Ibn 'Adbil Yaaliil bin 'Abdi Kulaal, hakunijibu nililolitaka. Niliondoka nami nikiwa mzito juu ya uso wangu. Nilifarijika nilipofika Qarn Ath-Tha'alib, niliponyanyua kichwa changu na kuona kulikuwa na kiwingu kilichokuwa kimenifunika. Nilipotazama nikamuona Jibriyl ('Alayhis Salaam), aliita akisema: "Hakika Allaah Ta'aalaa amesikia kauli ya kaumu yako kwako, na walivyokujibu, Allaah Amekutumia Malaika wa jabali aliniita akanisalimia, kisha akasema: 'Ee Muhammad! Hakika Allaah amesikia kauli ya watu wako, na mimi ni Malaika wa majabali. Na hakika amenituma Mola wangu kwako uaiamuru amri yako; Utakacho, ukitaka nitawasaga na haya majabali mawili.' Akasemas Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): 'Bali napenda Allaah atoe katika migongo yao watakaomuabudu Allaah Peke Yake hawamshirikishi Yenye na chochote." [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

Hadiyth – 2

وعن عائشة رضي الله عنها ، قالت : مَا ضَرَبَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم شَيْئاً قَطُّ بِيَدِهِ ، وَلاَ امْرَأةً وَلاَ خَادِماً ، إِلاَّ أنْ يُجَاهِدَ فِي سَبيلِ اللهِ ، وَمَا نِيلَ مِنْهُ شَيْءٌ قَطُّ فَيَنْتَقِمَ مِنْ صَاحِبِهِ ، إِلاَّ أن يُنْتَهَكَ شَيْءٌ مِنْ مَحَارِمِ اللهِ تَعَالَى ، فَيَنْتَقِمُ للهِ تَعَالَى . رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwa 'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) kuwa: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) hakupiga kitu chochote kwa mkono wake na wala hakumpiga mwanamke wala mjakazi isipokuwa anapopigana jihadi katika njia ya Allaah. Na hakulipiza kisasi kwa lolote alilofanyiwa yeye isipokuwa inapovukwa mipaka ya Allaah Ta'aalaa, hapo ndio alikuwa akilipiza kisasi." [Muslim] 

 

 

Hadiyth – 3

وعن أنس رضي الله عنه ، قَالَ : كُنْتُ أمشي مَعَ رسول الله صلى الله عليه وسلم وَعَلَيْهِ بُرْدٌ نَجْرَانيٌّ غَلِيظُ الحَاشِيَةِ ، فأدْرَكَهُ أعْرَابِيٌّ فَجَبذَهُ بِرِدَائِهِ جَبْذَةً شَديدةً ، فَنَظَرْتُ إِلَى صَفْحَةِ عَاتِقِ النَّبيِّ صلى الله عليه وسلم ، وَقَدْ أثَّرَتْ بِهَا حَاشِيَةُ الرِّدَاءِ مِنْ شِدَّةِ جَبْذَتِهِ ، ثُمَّ قَالَ : يَا مُحَمَّدُ ، مُر لِي مِنْ مَالِ اللهِ الَّذِي عِنْدَكَ . فَالتَفَتَ إِلَيْهِ ، فَضَحِكَ ثُمَّ أَمَرَ لَهُ بِعَطَاءٍ . متفقٌ عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwa Anas (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: Nilikuwa nikitembea pamoja na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akiwa amevaa shuka la Najran lililokuwa na ugumu pembezoni mwake. Akamkuta njiani Mbedui amabaye alimshika na kumvuta kwa shuka lake hilo kwa nguvu. Nilipomwangalia Nabiy (Swalla allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) katika shingo yake akiwa ameathirika kwa ule ugumu wa pembezoni wa shuka lake kwa ile nguvu kubwa ya kuvutwa. Kisha alisema: 'Ee Muhammad! Toa amri nipatwe katika ile mali ya Allaah uliyokuwa nayo.' Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alimwangalia na kucheka, kisha akaamrisha apatiwe sehemu katika mali hiyo." [Al-Bukhaariy na Muslim].

 

 

Hadiyth – 4

وعن ابن مسعود رضي الله عنه ، قَالَ : كأني أنظر إِلَى رسول الله صلى الله عليه وسلم يَحْكِي نَبِيّاً مِنَ الأنبياءِ ، صَلَوَاتُ اللهِ وَسَلامُه عَلَيْهِمْ ، ضَرَبَهُ قَوْمُهُ فَأدْمَوْهُ ، وَهُوَ يَمْسَحُ الدَّمَ عَنْ وَجْهِهِ ، ويقول : ((  اللَّهُمَّ اغْفِرْ لِقَوْمِي ؛ فَإنَّهُمْ لاَ يَعْلَمُونَ )) متفقٌ عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwa Ibn Mas'uwd (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: Kana kwamba ninamwangalia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akimzungumzia Nabiy miongoni mwa Manabiy ambaye alipigwa na watu wake mpaka akawa anatoka damu; alipokuwa anaifuta hiyo damu usoni alikuwa anasema: "Ee Mola wangu wasamehe watu wangu kwani wao hawajui." [Al-Bukhaariy na Muslim].

 

 

Hadiyth – 5

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : ((  لَيْسَ الشَّديدُ بِالصُّرَعَةِ ، إنَّمَا الشَّدِيدُ الَّذِي يَمْلِكُ نَفْسَهُ عِنْدَ الْغَضَبِ )) متفقٌ عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwa abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mwenye nguvu ni yule amabye anamiliki nafsi yake anaposhikwa na ghadhabu." [Al-Bukhaariy na Muslim].

 

 

 

 

 

Share