080-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Wajibu wa Kuwatii Viongozi kwa Mambo Yasiyo ya Maasiya na Kukatazwa Kuwatii Katika Maasiya

 

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

 

باب وجوب طاعة ولاة الأمر في غير معصية وتحريم طاعتهم في المعصية

080-Mlango Wa Wajibu wa Kuwatii Viongozi kwa Mambo Yasiyo ya Maasiya na Kukatazwa Kuwatii Katika Maasiya

 

Alhidaaya.com

 

قَالَ الله تَعَالَى:

أَطِيعُوا اللَّـهَ وَأَطِيعُوا الرَّسُولَ وَأُولِي الْأَمْرِ مِنكُمْ ۖ  ﴿٥٩﴾

Mtiini Allaah na mtiini Rasuli na wenye madaraka katika nyinyi. [An-Nisaa: 59]

 

 

Hadiyth – 1

وعن ابن عمر رضي الله عنهما ، عن النبيِّ صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : ((  عَلَى المَرْءِ الْمُسْلِمِ السَّمْعُ والطَّاعَةُ فِيمَا أحَبَّ وكَرِهَ ، إِلاَّ أنْ يُؤْمَرَ بِمَعْصِيةٍ ، فَإذَا أُمِرَ بِمَعْصِيةٍ فَلاَ سَمْعَ وَلاَ طَاعَةَ )) متفقٌ عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwa Ibn 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Kusikia na kutii ni wajibu kwa kila Muislamu katika alichokipenda na alicho kichukia, kwa muda ambao hakuamrishwa kufanya maasi. Kama ataamrishwa kufanya maasi basi hakuna kusikia wala kutii." [Al-Bukhaariy, Muslim, Abu Daawuud, At-Tirmidhiy na An-Nasai].

 

 

Hadiyth – 2

وعن ابن عمر رضي الله عنهما ، قَالَ : كُنَّا إِذَا بَايَعْنَا رسولَ الله صلى الله عليه وسلم عَلَى السَّمعِ والطَّاعَةِ ، يَقُولُ لَنَا : ((  فِيمَا اسْتَطَعْتُمْ )) متفقٌ عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwa Ibn 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kwamba amesema: Tulipokuwa tukimbai Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) juu ya kusikia na kutii alikuwa akituambia: "Kwa mnayo weza." [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

Hadiyth – 3

وعن ابن عمر رضي الله عنهما ، قَالَ : سَمِعْتُ رسول الله صلى الله عليه وسلم ، يقول : ((  مَنْ خَلَعَ يَداً مِنْ طَاعَةٍ لَقِيَ اللهَ يَوْمَ الْقِيَامَةِ وَلاَ حُجَّةَ لَهُ ، وَمَنْ مَاتَ وَلَيْسَ في عُنُقِهِ بَيْعَةٌ ، مَاتَ مِيتَةً جَاهِلِيَّةً )) رواه مسلم .

وفي رواية لَهُ : ((  وَمَنْ مَاتَ وَهُوَ مُفَارِقٌ لِلجَمَاعَةِ ، فَإنَّهُ يَمُوتُ مِيتَةً   جَاهِلِيَّةً )) .

Imepokewa kutoka kwa Ibn 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) amesema: Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: "Mwenye kuondosha mkono katika kutii atamkuta Allaah Siku ya Qiyaamah hana hoja. Na atakaye kufa na shingoni mwake hana bai'ah amekufa mauti ya kijahiliya. [Muslim]

Na katika riwaayah yake nyingine: "Na atakaye kufa naye amejitenga na jamaa (kikundi cha waislamu), hakika atakufa mauti ya ujahiliyyah."

 

 

Hadiyth – 4

وعن أنسٍ رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم : ((  اسْمَعُوا وأطِيعُوا ، وَإنِ استُعْمِلَ عَلَيْكُمْ عَبْدٌ حَبَشيٌّ ، كأنَّ رأْسَهُ زَبيبةٌ )) رواه البخاري .

Imepokewa kwa Anas (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Sikieni na mutii, japokuwa atachaguliwa juu yenu kama kiongozi mtumwa wa Habeshi (Ethiopia) kama kwamba kichwa chake kimefanana na zabibu." [Al-Bukhaariy]

 

 

Hadiyth – 5

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : ((  عَلَيْكَ السَّمْعُ وَالطَّاعَةُ في عُسْرِكَ وَيُسْرِكَ ، وَمَنْشَطِكَ وَمَكْرَهِكَ ، وَأثَرَةٍ عَلَيْكَ )) رواه مسلم .

Kutoka kwa abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Ni juu yako kusikia na kutii katika utajiri wako na umasikini na uwe muaminifu." [Muslim]

 

 

Hadiyth – 6

وعن عبدِ اللهِ بن عمرو رضي الله عنهما ، قَالَ : كنا مَعَ رسول الله صلى الله عليه وسلم في سَفَرٍ ، فَنَزَلْنَا مَنْزِلاً ، فَمِنَّا مَنْ يُصْلِحُ خِبَاءهُ ، وَمِنّا مَنْ يَنْتَضِلُ ، وَمِنَّا مَنْ هُوَ في جَشَرِهِ ، إذْ نَادَى مُنَادِي رسولِ الله صلى الله عليه وسلم : الصَّلاةَ جَامِعَةً . فَاجْتَمَعْنَا إِلَى رسولِ الله صلى الله عليه وسلم ، فَقَالَ : ((  إنَّهُ لَمْ يَكُنْ نَبيٌّ قَبْلِي إِلاَّ كَانَ حَقّاً عَلَيْهِ أنْ يَدُلَّ أُمَّتَهُ عَلَى خَيْرِ مَا يَعْلَمُهُ لَهُمْ ، وَيُنْذِرَهُم شَرَّ مَا يَعْلَمُهُ لَهُمْ . وَإنَّ أُمَّتَكُمْ هذِهِ جُعِلَ عَافِيَتُهَا في أوَّلِهَا ، وَسَيُصيبُ آخِرَهَا بَلاَءٌ وَأمُورٌ تُنْكِرُونَهَا ، وَتَجِيءُ فِتنَةٌ يُرَقِّقُ بَعْضُهَا بَعْضاً ، وَتَجِيءُ الفتنَةُ فَيقُولُ المُؤْمِنُ : هذه مُهلكتي ، ثُمَّ تنكشفُ ، وتجيء الفتنةُ فيقولُ المؤمنُ : هذِهِ هذِهِ . فَمَنْ أحَبَّ أنْ يُزَحْزَحَ عَنِ النَّارِ، ويُدْخَلَ الجَنَّةَ، فَلْتَأتِهِ منيَّتُهُ وَهُوَ يُؤْمِنَ باللهِ واليَوْمِ الآخِرِ ، وَلْيَأتِ إِلَى النَّاسِ الَّذِي يُحِبُّ أنْ يُؤتَى إِلَيْهِ. وَمَنْ بَايَعَ إمَاماً فَأعْطَاهُ صَفْقَةَ يَدِهِ ، وَثَمَرَةَ قَلْبِهِ ، فَلْيُطِعْهُ إن استَطَاعَ ، فإنْ جَاءَ آخَرُ يُنَازِعُهُ فَاضْرِبُوا عُنْقَ الآخَرِ )) رواه مسلم .

Kutoka kwa 'Abdillah bin 'Amru (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: Tulikuwa pamoja na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) safarini, tukashuka mahali. Katika sisi kuna anaetengeneza hema lake, katika sisi kuna wanaoshindana, mwengine anailisha mifugo yake. Mwitaji wa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Swalaah ya jamaa," Tukakusanyika mbele ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), akasema: "Hakika hakukuwa Nabiy kabla yangu ila ilikuwa ni haki yake kuonyesha Ummah wake kheri anayoijua kwa ajili yao, Na kuwaonya shari anayoijua kwa ajili yao. Hakika Umma wenu huu afya yake iko katika wa mwanzo wake, Na wa mwisho wake utapata balaa na mambo mnayo yakataa. Na itakuja fitna moja baada ya nyingine. Itakuja fitna Muumini atasema: 'Haya ni maangamivu yangu. Kisha itatoweka, na itakuja fitina muumini atasema: 'Ni haya haya Haya." Hivyo, anayependa kuepushwa na Moto na kuingizwa Peponi, Basi akutane na kifo chake akiwa anamuamini Allaah na Siku ya Mwisho, na awaletee watu ambao anapenda waletwe kwake. Na mwenye kumbai Imamu kwa kumpatia ahadi kwa mkono wake na tunda la moyo wake, Basi amtii anavyoweza. Akija mwingine kushindana naye, Basi ipigeni shingo ya yule Mwingine." [Muslim].

 

 

Hadiyth – 7

وعن أَبي هُنَيْدَةَ وَائِلِ بن حُجرٍ رضي الله عنه ، قَالَ : سَألَ سَلَمَةُ بن يَزيدَ الجُعفِيُّ رسولَ الله صلى الله عليه وسلم ، فَقَالَ : يَا نَبِيَّ الله ، أرأيتَ إنْ قامَت عَلَيْنَا أُمَرَاءُ يَسألُونَا حَقَّهُم ، وَيمْنَعُونَا حَقَّنَا ، فَمَا تَأْمُرُنَا ؟ فَأعْرَضَ عنه ، ثُمَّ سَألَهُ ، فَقَالَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم : ((  اسْمَعْوا وَأَطِيعُوا ، فإنَّمَا عَلَيْهِمْ مَا حُمِّلُوا ، وَعَلَيْكُمْ مَا حملْتُمْ )) رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwa Abu Hunaydah Waail bin Hujr (Radhwiya Allaahu 'anhu) ambaye amesema: Salamah bin Yaziyd Al-Ju'fiy alimuuliza Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kwa kusema: "Ee Nabiy wa Allaah! Waonaje wakisimama juu yetu viongozi wakitaka haki zao na kukataa zetu, unatuamuru nini?" Nabiy alijiepusha na kujibu swalihilo. Kisha alimuuliza mara nyengine, hapo Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: "Sikieni na mtii, hakika wao watabeba mzigo waliojitikwa nanyi mtabeba wenu." [Muslim]

 

 

Hadiyth – 8

وعن عبد الله بن مسعود رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم : ((  إنَّهَا سَتَكُونُ بَعْدِي أثَرَةٌ وَأُمُورٌ تُنْكِرُونَهَا ! )) قالوا : يَا رسول الله ، كَيْفَ تَأمُرُ مَنْ أدْرَكَ مِنَّا ذَلِكَ ؟ قَالَ : ((  تُؤَدُّونَ الحَقَّ الَّذِي عَلَيْكُمْ ، وَتَسْأَلُونَ اللهَ الَّذِي لَكُمْ )) متفقٌ عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwa 'Abdillaah bin Mas'uwd (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Kutakuwa na ubinafsi na mambo msiyoyakubali." Wakauliza: "Ee Rasuli wa Allaah! Unatuamuru nini kwa yule atakaye fikiwa na hayo?" Akajibu: "Tekelezeni wajibu wenu na mumuombe Allaah (Awapeni) ambalo ni haki yenu." [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

 

Hadiyth – 9

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : ((  مَنْ أطَاعَنِي فَقَدْ أطَاعَ اللهَ ، وَمَنْ عَصَانِي فَقَدْ عَصَى اللهَ ، وَمَنْ يُطِعِ الأَمِيرَ فَقَدْ أطَاعَنِي ، وَمَنْ يَعصِ الأميرَ فَقَدْ عَصَانِي )) متفقٌ عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mwenye kunitii mimi basi amemtii Allaah na mwenye kuniasi mimi basi amemuasi Allaah. Na mwenye kumtii amiri (kiongozi) basi amenitii mimi na mwenye kumuasi amiri basi ameniasi mimi." [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

Hadiyth – 10

وعن ابن عباسٍ رضي الله عنهما : أن رسول الله صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : ((  مَنْ كَره مِنْ أمِيرِهِ شَيْئاً فَلْيَصْبِرْ ، فَإنَّهُ مَنْ خَرَجَ مِنَ السُّلطَانِ شِبْراً مَاتَ مِيتَةً جَاهِلِيَّةً )) متفقٌ عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwa Ibn 'Abbaas (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mwenye kuchukia kwa amiri wake kitu basi asubiri, kwa sababu mwenye kutoka nje ya utawala wa amiri shubiri moja amekufa kifo cha kijahiliya (kikafiri)." [Al-Bukhaariy, Muslim na Ahmad]

 

 

Hadiyth – 11

وعن أَبي بكرة رضي الله عنه ، قَالَ : سَمِعْتُ رسول الله صلى الله عليه وسلم ، يقول : ((  مَنْ أهانَ السُّلطَانَ أَهَانَهُ الله )) رواه الترمذي ، وقال : (( حديث حسن )) .

Imepokewa kutoka kwa Abu Bakrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) ambaye amesema: Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Alaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: "Yeyote mwenye kumtweza kiongozi Allaah atamtweza." [At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan]

 

 

 

 

 

 

Share