023-Asbaabun-Nuzuwl: Al-Muuminuwn Aayah 76: وَلَقَدْ أَخَذْنَاهُم بِالْعَذَابِ فَمَا اسْتَكَانُوا لِرَبِّهِمْ وَمَا يَتَضَرَّعُونَ

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

(Sababu Za Kuteremshwa Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)

 

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

 023-Asbaabun-Nuzuwl Al-Muuminuwn Aayah 76

 

 

Kauli Yake Allaah (سبحانه وتعالى):

 

وَلَقَدْ أَخَذْنَاهُم بِالْعَذَابِ فَمَا اسْتَكَانُوا لِرَبِّهِمْ وَمَا يَتَضَرَّعُونَ ﴿٧٦﴾

Kwa yakini Tuliwachukua kwa adhabu, basi hawakunyenyekea kujisalimisha kwa Rabb wao, na wala hawakuomba du’aa kwa raghba na khofu. [Al-Muuminuwn: 76]

 

Sababun-Nuzuwl: 

 

 

حدثنا ابن حميد قال حدثنا أبو تميلة هو يحيى بن واضح عن الحسين عن يزيد عن عكرمة عن ابن عباس قال: جاء أبو سُفيانَ بنُ حَرْبٍ إلى رسولِ اللهِ صلَّى اللهُ عليه وسلَّم فقال : يا مُحمَّدُ أنشُدُكَ اللهَ والرَّحِمَ فقد أكَلْنا العِلْهِزَ - يعني الوَبَرَ والدَّمَ - فأنزَل اللهُ  وَلَقَدْ أَخَذْنَاهُم بِالْعَذَابِ فَمَا اسْتَكَانُوا لِرَبِّهِمْ وَمَا يَتَضَرَّعُونَ ﴿٧٦﴾

Ametuhadithia Ibn Humayd amesema: Ametuhadithia Abu Thamiylah ambaye ni Yahyaa bin Waadhwih, toka kwa Al-Husayn, toka kwa ‘Ikrimah, toka kwa Ibn ‘Abbaas, amesema: Abu Sufyaan (bin Harb, kiongozi wa Maquraysh]) alikuja kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akamwambia: Ee Muhammad!  Nakuomba uape kwa Allaah na kwa damu ya ukaraba, hakika sisi tunakula “Al-‘Ilhiza”, yaani manyoya ya wanyama na damu (kinaya kuashiria hali mbaya sana ya njaa iliyowapata). Na Allaah (سبحانه وتعالى) Akateremsha:

وَلَقَدْ أَخَذْنَاهُم بِالْعَذَابِ فَمَا اسْتَكَانُوا لِرَبِّهِمْ وَمَا يَتَضَرَّعُونَ ﴿٧٦﴾

Kwa yakini Tuliwachukua kwa adhabu, basi hawakunyenyekea kujisalimisha kwa Rabb wao, na wala hawakuomba du’aa kwa raghba na khofu.”

 

[Ibn Jariyr katika Mujallad wa 14 ukurasa wa 45]

 

Ar-Rahm: (Ukaraba wa damu) uliyopo kati yao na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) kuwa atawaondoshea vikwazo vya chakula alivyowaekea Thumaamah bin Uthaal Al-Hanafiy ambaye alikuwa ni Wali wa Al-Yamaamah nchini Yemen. Aliposilimu, alizuia vyakula kupelekwa Makkah mpaka kwa idhini toka kwa Rasuli wa Allaah صلى الله عليه وآله وسلم).

 

[Wapokezi wa Hadiyth ni watu wa kuaminika isipokuwa Sheikh wa At-Twabariy Muhammad bin Humayd Az-Raaziy, yeye ni dhaifu (wa kumbukumbu). Lakini Hadiyth hii imekuja kupitia Isnaad nyinginezo tofauti na Isnaad hii ambaye yeye yumo. Kwani imesimuliwa na Ibn Abiy Haatim kama ilivyo katika Tafsiyr ya Ibn Kathiyr Mujallad wa 3 ukurasa wa 251, pia An-Nasaaiy katika Ibn Kathiyr, vile vile Ibn Hibaan katika Mujallad wa 3 ukurasa wa 434].

 

 

Share