Imaam Al-Bayhaqiy: Kuutukuza Mswahafu: Haijuzu Kuuwekea Kitu Juu Yake

Kuutukuza Mswahafu: Haijuzu Kuuwekea Kitu Juu Yake

 

Imaam Al-Bayhaqiy (Rahimahu Allaah)

 

Alhidaaya.com

 

 

Shaykh As-Sunnah An-Nabawiyyah Imaam Al-Bayhaqiy (Rahimahu Allaah) amesema:

 

 

“Haiwekwi juu ya Mswahafu kitabu kingine wala nguo wala kitu chochote  ila isipokuwa ni Mswahafu mwingine juu yake.”

 

 

[Al-Bayhaqiy - Shu’ab Al-Iymaan (2/329)]

 

Faida: 

 

Hiyo ni kutokana na kauli ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) zifuatazo kuhusu kuadhimisha Vitu Vitukufu Vyake, Alama Zake za Dini na kadhalika:

 ذَٰلِكَ وَمَن يُعَظِّمْ حُرُمَاتِ اللَّـهِ فَهُوَ خَيْرٌ لَّهُ عِندَ رَبِّهِ  

Ndio hivyo iwe na yeyote anayeadhimisha vitukufu vya Allaah basi hivyo ni khayr kwake mbele ya Rabb wake. [Al-Hajj: 30]

Na Anasema pia Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

ذَٰلِكَ وَمَن يُعَظِّمْ شَعَائِرَ اللَّـهِ فَإِنَّهَا مِن تَقْوَى الْقُلُوبِ ﴿٣٢﴾

Ndivyo hivyo, na yeyote anayeadhimisha Ishara za Allaah, basi hayo ni katika taqwa ya nyoyo. [Al-Hajj: 32]

 

 

 

Share