026-Majina Ya Allaah Mazuri Na Swifa Zake أسماء الله الحسنى وصفاته: AL-HAKIYM

أسماء الله الحسنى وصفاته

Majina Ya Allaah Mazuri Na Swifa Zake

 

Alhidaaya.com

 

 

الْحَكِيم

 

AL-HAKIYM

 

 

 

 

Al-Hakiym:  Mwenye Hikmah

 

Mwenye kutenganisha baina ya mambo.  Mwenye kuweka vitu sehemu yake na Ambaye mtu hapendi kufanyiwa vitu visivyofaa.

 

Ni Mwenye Hikmah katika maneno, matendo na hukumu Zake, hivyo Hasemi, Hafanyi wala Hatenganishi isipokuwa ni haki, uadilifu, kilicho sawa.  

 

Haondoki katika Hikmah Yake kuimbe chochote.

 

Haingii katika mpangilio Wake makosa yoyote.

 

Ni Mwenye Hikmah ya juu katika uumbaji Wake na katika maamrisho Yake.

 

Haumbi kwa mchezo, wala Hafanyi Shariy’ah bila lengo, wala Hawaachi waja Wake hivi hivi tu.

 

Haamrishi kwa yasiyokuwa na maslahi wala Hakatazi ila yaliyo na madhara.

 

Mwenye Hikmah za mwanzo na mwisho na katika ukamilifu wa Hikmah Yake Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa), ni kuja kwa Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Dini ya Kiislamu na Qur-aan. Ni dalili kuu ya ukweli wake, na Akasadikisha alichokuja nacho kwa kuwa Kwake Mwenye kuhukumu kwa ukamilifu haipatikani islahi duniani na Aakhirah ila Kwake. Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

لَّا يَأْتِيهِ الْبَاطِلُ مِن بَيْنِ يَدَيْهِ وَلَا مِنْ خَلْفِهِ ۖ تَنزِيلٌ مِّنْ حَكِيمٍ حَمِيدٍ﴿٤٢﴾

Hakitokifikia ubatili mbele yake, na wala nyuma yake; ni uteremsho kutoka kwa Mwenye hikmah wa yote, Mwenye kustahiki kuhimidiwa kwa yote. [Fusw-Swilat: 42]

 

 

 

Faida, Mafunzo Tuyapatayo Na Jinsi Ya Kufanyia Kazi Jina Hili La Allaah; Al-Hakiym:

 

 

1-Zingatia Hikmah Yake Al-Hakiym jinsi Alivyoumba dunia Akaweka kila kitu na mahitajio yote ya waja Wake. Jinsi Alivyoumba mbingu, ardhi Akaitandaza na ardhi ili viumbe viweze kuishi humo.

 

 

2-Zingatia uumbaji Wake wa mwili wa mwana Aadam na jinsi Alivyojaalia kila kiungo kiko sehemu ifaayo. Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

 الَّذِي أَحْسَنَ كُلَّ شَيْءٍ خَلَقَهُ ۖ وَبَدَأَ خَلْقَ الْإِنسَانِ مِن طِينٍ ﴿٧﴾

Ambaye Amefanya uzuri kila kitu Alichokiumba; na Akaanzisha uumbaji wa insani kutokana na udongo.

 

ثُمَّ جَعَلَ نَسْلَهُ مِن سُلَالَةٍ مِّن مَّاءٍ مَّهِينٍ ﴿٨﴾

Kisha Akajaalia kizazi chake kutokana na mchujo safi wa maji dhalilifu.

 

 

ثُمَّ سَوَّاهُ وَنَفَخَ فِيهِ مِن رُّوحِهِ ۖ وَجَعَلَ لَكُمُ السَّمْعَ وَالْأَبْصَارَ وَالْأَفْئِدَةَ ۚ قَلِيلًا مَّا تَشْكُرُونَ ﴿٩﴾

Kisha Akamsawazisha, na Akapuliza humo roho yake (Aliyoiumba Allaah). Na Akakujaalieni kusikia na kuona na nyoyo, ni machache mno yale mnayoshukuru. [As-Sajdah: 7-9]

 

 

3-Omba du’aa Allaah ('Azza wa Jalla) Akujaalie uwe mwenye hikmah kwani anayepewa hikmah hakika amepewa kheri nyingi kama Anavyosema Mwenyewe Allaah ('Azza wa Jalla):

 

يُؤْتِي الْحِكْمَةَ مَن يَشَاءُ ۚ وَمَن يُؤْتَ الْحِكْمَةَ فَقَدْ أُوتِيَ خَيْرًا كَثِيرًا ۗ وَمَا يَذَّكَّرُ إِلَّا أُولُو الْأَلْبَابِ ﴿٢٦٩﴾

Humpa hikmah Amtakaye. Na anayepewa hikmah basi kwa yakini huwa amepewa khayr nyingi. Na hawakumbuki isipokuwa wenye akili. [Al-BaqaraHl 269]

 

4-Tumia hikmah katika kutaamuli na watu, kama vile katika kusuluhisha watu, katika kutakwa ushauri wa jambo zito na kadhaalika.

 

5- Unapopatwa na mitihani amini kwamba ni majaaliwa ya Allaah ('Azza wa Jalla) na ni kheri kwako badala ya shari kwa sababu Yeye Al-Hakiym Anajua kwanini Amejaalia mitihani hiyo ikusibu, bila shaka kwa hikmah Yake kama Anavyosema:

 

وَعَسَىٰ أَن تَكْرَهُوا شَيْئًا وَهُوَ خَيْرٌ لَّكُمْ ۖ وَعَسَىٰ أَن تُحِبُّوا شَيْئًا وَهُوَ شَرٌّ لَّكُمْ ۗ وَاللَّـهُ يَعْلَمُ وَأَنتُمْ لَا تَعْلَمُونَ ﴿٢١٦﴾

Na asaa mkachukia jambo na hali lenyewe ni khayr kwenu. Na asaa mkapenda jambo na hali lenyewe ni la shari kwenu. Na Allaah Anajua na nyinyi hamjui. [Al-Baqarah: 216]

 

 

 

Share