027-Majina Ya Allaah Mazuri Na Swifa Zake أسماء الله الحسنى وصفاته: AS-SAMIY'U

أسماء الله الحسنى وصفاته

Majina Ya Allaah Mazuri Na Swifa Zake

 

Alhidaaya.com

 

السَّمِيع

 

AS-SAMIY’U

 

 

 

 

As-Samiy’u: Mwenye Kusikia Yote Daima

 

 

As-Samiy’u imetajwa katika Qur-aan mara arubaini na tano; hii inajulisha umuhimu wa Jina na Sifa hii tukufu ya Allaah ('Azza wa Jalla) Na Jina hili la Allaah ('Azza wa Jalla)  limejumuika na  البصير (Al-Baswiyr: Mwenye Kuona Yote Daima) mara nyingi katika Qur-aan miongoni mwayo ni Kauli Zake Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

 

لَيْسَ كَمِثْلِهِ شَيْءٌ ۖ وَهُوَ السَّمِيعُ الْبَصِيرُ﴿١١﴾

Hakuna chochote kinachofanana Naye, Naye Ndiye Mwenye kusikia yote, Mwenye kuona yote. [Ash-Shuwraa: 11]

 

 

Na pia,

 

وَاللَّـهُ يَقْضِي بِالْحَقِّ ۖ وَالَّذِينَ يَدْعُونَ مِن دُونِهِ لَا يَقْضُونَ بِشَيْءٍ ۗ إِنَّ اللَّـهَ هُوَ السَّمِيعُ الْبَصِيرُ﴿٢٠﴾

Na Allaah Anahukumu kwa haki. Na wale wanaowaomba badala Yake hawawezi kuhukumu kwa chochote. Hakika Allaah Ndiye Mwenye kusikia yote, Mwenye kuona yote. [Ghaafir: 20]

 

 

Na pia,

 

إِنَّ اللَّـهَ يَأْمُرُكُمْ أَن تُؤَدُّوا الْأَمَانَاتِ إِلَىٰ أَهْلِهَا وَإِذَا حَكَمْتُم بَيْنَ النَّاسِ أَن تَحْكُمُوا بِالْعَدْلِ ۚ إِنَّ اللَّـهَ نِعِمَّا يَعِظُكُم بِهِ ۗ إِنَّ اللَّـهَ كَانَ سَمِيعًا بَصِيرًا ﴿٥٨﴾

Hakika Allaah Anakuamrisheni kurudisha amana kwa wenyewe. Na mtakapohukumu baina ya watu mhukumu kwa uadilifu. Hakika uzuri ulioje Anayokuwaidhini nayo Allaah; hakika Allaah daima ni Mwenye kusikia yote, Mwenye kuona yote. [An-Nisaa: 58]

 

 

Usikivu Wake umeenea usikivu wote, kwa lugha mbali mbali, kwa haja za nyingi za watu, yaliyo siri Kwake yako wazi na minong’ono Kwake na sauti yenye kusikika, na aliye mbali na karibu Kwake, usikivu Wake Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) ni wa aina mbili:

 

 

Kwanza: Usikivu Wake wa sauti zote za dhahiri na za siri na kuenea kwake, sauti hazitofautiani Kwake, kadiri zitakavyoongezeka na kuwa aina mbalimbali kana kwamba sauti zote hizo ni moja kwake. Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa)

 

سَوَاءٌ مِّنكُم مَّنْ أَسَرَّ الْقَوْلَ وَمَن جَهَرَ بِهِ وَمَنْ هُوَ مُسْتَخْفٍ بِاللَّيْلِ وَسَارِبٌ بِالنَّهَارِ ﴿١٠﴾

Ni sawasawa kwenu anayefanya siri kauli (yake), au anayeisema kwa jahara, na anayenyemelea usiku na anayatembea huru mchana.  [Ar-Ra’d: 10]

 

 

Pili: Husikiliza maombi ya waja Wake, huwajibu na huwapa malipo kama alivyoomba Nabiy Ibraahiym ('Alayhis-Salaam)

 

الْحَمْدُ لِلَّـهِ الَّذِي وَهَبَ لِي عَلَى الْكِبَرِ إِسْمَاعِيلَ وَإِسْحَاقَ ۚ إِنَّ رَبِّي لَسَمِيعُ الدُّعَاءِ ﴿٣٩﴾

AlhamduliLLaah (Himdi Anastahiki Allaah), Ambaye Amenitunukia juu ya umri mkubwa wangu Ismaa’iyl na Is-haaq. Hakika Rabb wangu bila shaka ni Mwenye kusikia du’aa yangu. [Ibraahiym: 39]

 

 

Yaani: Mwenye kujibu du’aa za waja Wake, kama alivyosema mtu katika Swalaah na ikathibiti katika Hadiyth:

 

 

حَدَّثَنَا إِسْمَاعِيلُ، قَالَ حَدَّثَنِي مَالِكٌ، عَنْ سُمَىٍّ، عَنْ أَبِي صَالِحٍ، عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ ـ رضى الله عنه ـ أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم قَالَ ‏ "‏ إِذَا قَالَ الإِمَامُ سَمِعَ اللَّهُ لِمَنْ حَمِدَهُ‏.‏ فَقُولُوا اللَّهُمَّ رَبَّنَا لَكَ الْحَمْدُ، فَإِنَّهُ مَنْ وَافَقَ قَوْلُهُ قَوْلَ الْمَلاَئِكَةِ، غُفِرَ لَهُ مَا تَقَدَّمَ مِنْ ذَنْبِهِ ‏"‏‏.‏

 

Amesimulia Abu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)  amesema:  “Pindi Imaam anaposema (katika Swalaah),

 

سَمِعَ اللَّهُ لِمَنْ حَمِدَهُ‏

Sami’a Allaahu liman Hamidah

 

Allaah Anasikia Anayemhimidi

 

Semeni:

اللَّهُمَّ رَبَّنَا لَكَ الْحَمْدُ

 

Allaahumma Rabbanaa Lakal-Hamd

 

Ee Allaah Rabb wetu, Himdi ni Zako

 

Kwani yeyote mwenye kuafikiana na Malaika katika kusema hayo, ataghufuriwa madhambi yake yote yaliyotangulia.” [Al-Bukhaariy]

 

 

Na usikivu wake Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) ni kwa maana ya kumfanya anayeomba kumdiriki Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kwa sauti; Yaani:

 

 

i-Kumtisha; Mfano wake ni Kauli Zake Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

أَمْ يَحْسَبُونَ أَنَّا لَا نَسْمَعُ سِرَّهُمْ وَنَجْوَاهُم ۚ بَلَىٰ وَرُسُلُنَا لَدَيْهِمْ يَكْتُبُونَ﴿٨٠﴾

Au wanadhania kwamba Sisi Hatusikii siri zao na minong’ono yao? Sivyo! (Tunasikia!) Na Wajumbe wetu wako kwao wanaandika. [Az-Zukhruf: 80]

 

 

Na pia,

 

لَّقَدْ سَمِعَ اللَّـهُ قَوْلَ الَّذِينَ قَالُوا إِنَّ اللَّـهَ فَقِيرٌ وَنَحْنُ أَغْنِيَاءُ ۘ سَنَكْتُبُ مَا قَالُوا وَقَتْلَهُمُ الْأَنبِيَاءَ بِغَيْرِ حَقٍّ وَنَقُولُ ذُوقُوا عَذَابَ الْحَرِيقِ ﴿١٨١﴾

Kwa yakini Allaah Ameisikia kauli ya wale (Mayahudi) waliosema: Hakika Allaah ni fakiri na sisi ni matajiri. Tutayaandika waliyoyasema na kuua kwao Manabii pasi na haki na Tutasema: Onjeni adhabu ya kuunguza. [Aal-‘Imraan: 181]

 

 

 

ii-Muradi wake ni Kumuunga mkono; Mfano Kauli Yake Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kwa Nabiy Muwsaa na Haaruwn ('Alayhimas-Salaam)

 

قَالَ لَا تَخَافَا ۖ إِنَّنِي مَعَكُمَا أَسْمَعُ وَأَرَىٰ ﴿٤٦﴾

(Allaah) Akasema: Msikhofu; hakika Mimi Niko pamoja nanyi, Nasikia na Naona. [Twaahaa: 46]

 

 

Yaani: Ninakuungeni mkono na kukunusuruni.

 

 

iii-Kubainisha upana na uenevu wa wa usikivu wa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa); Mfano Kauli Yake:

 

قَدْ سَمِعَ اللَّـهُ قَوْلَ الَّتِي تُجَادِلُكَ فِي زَوْجِهَا وَتَشْتَكِي إِلَى اللَّـهِ وَاللَّـهُ يَسْمَعُ تَحَاوُرَكُمَا ۚ إِنَّ اللَّـهَ سَمِيعٌ بَصِيرٌ﴿١﴾

Allaah Amekwishasikia kauli ya yule mwanamke anayejadiliana nawe (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kuhusu mumewe, na anamshitakia Allaah; na Allaah Anayasikia majibizano yenu. Hakika Allaah ni Mwenye kusikia yote, Mwenye kuona yote. [Al-Mujaadalah: 1]

 

 

 

Faida, Mafunzo Tuyapatayo Na Jinsi Ya Kufanyia Kazi Jina Hili La Allaah; As-Samiy’u:

 

 

1-Tahadhari kusema maneno maovu yoyote yale utambue kuwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anakusikia popote pale ulipo. Tambua kuwa hakuna siri mbele ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) lolote usemalo analisikia na linarekodiwa na Malaika wawili wanaoandika matendo ya mja hata kauli ya Ah!. Kumbuka Kauli Yake:

 

 

أَمْ يَحْسَبُونَ أَنَّا لَا نَسْمَعُ سِرَّهُمْ وَنَجْوَاهُم ۚ بَلَىٰ وَرُسُلُنَا لَدَيْهِمْ يَكْتُبُونَ﴿٨٠﴾

Au wanadhania kwamba Sisi Hatusikii siri zao na minong’ono yao? Sivyo! (Tunasikia!) Na Wajumbe wetu wako kwao wanaandika.[Az-Zukhruf: 80]

 

 

2-Jiepushe na kusikiliza yaliyoharamishwa kama muziki, nyimbo, ghiybah (kusengenya), na yote ambayo Hayamridhishi Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) usije kudhani Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Hasikii au Hajui uyatendayo bali Yeye ni As-Samiy’u kwa kila hali na hatoweza kukanusha mtu Siku ya Qiyaamah kwa sababu viungo vya mwili wako vitakuja kushuhudia yote uyatendayo; yakiwemo masikio Kauli Zake Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa)

 

حَتَّىٰ إِذَا مَا جَاءُوهَا شَهِدَ عَلَيْهِمْ سَمْعُهُمْ وَأَبْصَارُهُمْ وَجُلُودُهُم بِمَا كَانُوا يَعْمَلُونَ﴿٢٠﴾ وَقَالُوا لِجُلُودِهِمْ لِمَ شَهِدتُّمْ عَلَيْنَا ۖ قَالُوا أَنطَقَنَا اللَّـهُ الَّذِي أَنطَقَ كُلَّ شَيْءٍ وَهُوَ خَلَقَكُمْ أَوَّلَ مَرَّةٍ وَإِلَيْهِ تُرْجَعُونَ﴿٢١﴾ وَمَا كُنتُمْ تَسْتَتِرُونَ أَن يَشْهَدَ عَلَيْكُمْ سَمْعُكُمْ وَلَا أَبْصَارُكُمْ وَلَا جُلُودُكُمْ وَلَـٰكِن ظَنَنتُمْ أَنَّ اللَّـهَ لَا يَعْلَمُ كَثِيرًا مِّمَّا تَعْمَلُونَ﴿٢٢﴾ وَذَٰلِكُمْ ظَنُّكُمُ الَّذِي ظَنَنتُم بِرَبِّكُمْ أَرْدَاكُمْ فَأَصْبَحْتُم مِّنَ الْخَاسِرِينَ﴿٢٣﴾

Na Siku watakayokusanywa maadui wa Allaah kwenye moto, nao watakusanywa kupangwa Mpaka watakapoufikia yatashuhudia dhidi yao, masikio yao, na macho yao, na ngozi zao kwa yale waliyokuwa wakiyatenda. Na wataziambia ngozi zao: Mbona mnashuhudia dhidi yetu? Zitasema: Ametutamkisha Allaah Ambaye Ametamkisha kila kitu, Naye Ndiye Aliyekuumbeni mara ya kwanza na Kwake mtarejeshwa. Na hamkuwa mkijisitiri hata yasishuhudie masikio yenu, na wala macho yenu, na wala ngozi zenu; lakini mlidhania kwamba Allaah Hajui mengi katika yale mnayoyatenda. Na hivyo dhana yenu mliyokuwa mkimdhania Rabb wenu, imekuangamizeni, na mmekuwa miongoni mwa waliokhasirika. [Fusw-Swilat: 20 – 23]

 

 

 

3-Unapoomba du’aa, tambua kuwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Hasikilizi Du’aa ya mwenye kujionyesha kwa watu bali Anasikiliza du’aa ya mwenye kuomba kwa niyyah safi ya ikhlaasw kama ilivyokuja katika Hadiyth:

 

 

حَدَّثَنَا عُمَرُ بْنُ حَفْصٍ، قَالَ‏:‏ حَدَّثَنَا أَبِي، قَالَ‏:‏ حَدَّثَنَا الأَعْمَشُ قَالَ‏:‏ حَدَّثَنِي مَالِكُ بْنُ الْحَارِثِ، عَنْ عَبْدِ الرَّحْمَنِ بْنِ يَزِيدَ قَالَ‏:‏ كَانَ الرَّبِيعُ يَأْتِي عَلْقَمَةَ يَوْمَ الْجُمُعَةِ، فَإِذَا لَمْ أَكُنْ ثَمَّةَ أَرْسَلُوا إِلَيَّ، فَجَاءَ مَرَّةً وَلَسْتُ ثَمَّةَ، فَلَقِيَنِي عَلْقَمَةُ وَقَالَ لِي‏:‏ أَلَمْ تَرَ مَا جَاءَ بِهِ الرَّبِيعُ‏؟‏ قَالَ‏:‏ أَلَمْ تَرَ أَكْثَرَ مَا يَدْعُو النَّاسَ، وَمَا أَقَلَّ إِجَابَتَهُمْ‏؟‏ وَذَلِكَ أَنَّ اللَّهَ عَزَّ وَجَلَّ لاَ يَقْبَلُ إِلاَّ النَّاخِلَةَ مِنَ الدُّعَاءِ، قُلْتُ‏:‏ أَوَ لَيْسَ قَدْ قَالَ ذَلِكَ عَبْدُ اللهِ‏؟‏ قَالَ‏:‏ وَمَا قَالَ‏؟‏ قَالَ‏:‏ قَالَ عَبْدُ اللهِ‏:‏ لاَ يَسْمَعُ اللَّهُ مِنْ مُسْمِعٍ، وَلاَ مُرَاءٍ، وَلا لاعِبٍ، إِلا دَاعٍ دَعَا يَثْبُتُ مِنْ قَلْبِهِ، قَالَ‏:‏ فَذَكَرَ عَلْقَمَةَ‏؟‏ قَالَ‏:‏ نَعَمْ‏.‏

 

Abdur-Rahmaan ibn Yaziyd alisema: Ar-Rabiy’ alikuwa akienda kwa ‘Alqamah kila Ijumaa. Pindi nilipokuwa siko huko, walikuwa wakiniita. Mara moja alikuja wakati mimi sikuwepo. ‘Alqamah alikutana nami na akaniambia: Je, hukuona alicholeta Ar-Rabiy’? Akasema: Je,  hauoni jinsi watu wanavyoomba du’aa mara kwa mara na jinsi wanavyojibiwa kwa nadra (uchache)? Hivyo ni kwa sababu Allaah (‘Azza wa Jalla) Anataqabali du’aa iliyo na ikhlaasw (niyyah safi) pekee.  Nikamuuliza:  Je! Kwani hivyo sivyo ndivyo alivyosema ‘Abdullaah?    Akauliza: Amesema nini?  Nikasema: ‘Abdullaah amesema kwamba Allaah Hasikilizi (du’aa ya) mtu anayetaka watu wengine wasisikie, mtu anayejivunia au mchezaji, isipokuwa Yeye Humsikiliza tu yule ambaye anaomba du’aa kwa uthibitisho  kutoka moyoni mwake.  Akasema: Je! Alimtaja ‘Alqamah?  Akasema: Naam. [Adab Al-Mufrad Kitaab Ad-Du’aa]

 

 

 

4-Unapomuomba Allaah (‘Azza wa Jalla) du’aa muombe ukitaja Jina na Sifa Yake hii tukufu ya As-Samiy’u kuwa Yeye ni Mwenye Kusikia du’aa yako.  Na katika Qur-aan zimo du’aa kama hizo:

 

 

Nabiy Ibraahiym (‘Alayhis-Salaam) alipoomba baadaya kujenga Al-Ka’bah:

 

وَإِذْ يَرْفَعُ إِبْرَاهِيمُ الْقَوَاعِدَ مِنَ الْبَيْتِ وَإِسْمَاعِيلُ رَبَّنَا تَقَبَّلْ مِنَّا ۖ إِنَّكَ أَنتَ السَّمِيعُ الْعَلِيمُ ﴿١٢٧﴾

Na aliponyanyua Ibraahiym na Ismaa’iyl msingi wa Nyumba (Al-Ka’bah): Rabb wetu, Tutakabalie, hakika Wewe ni Mwenye kusikia yote, Mjuzi wa yote.

[Al-Baqarah: 127]

 

 

Na Maryam (‘Alayhas-Salaam) mama wa Nabiy Iysaa ('Alayhis-Salaam) alipoomba:

 

إِذْ قَالَتِ امْرَأَتُ عِمْرَانَ رَبِّ إِنِّي نَذَرْتُ لَكَ مَا فِي بَطْنِي مُحَرَّرًا فَتَقَبَّلْ مِنِّي ۖ إِنَّكَ أَنتَ السَّمِيعُ الْعَلِيمُ ﴿٣٥﴾

Pale aliposema mke wa ‘Imraan: Rabb wangu, hakika mimi nimeweka nadhiri Kwako kilichomo katika tumbo langu kuwa ni wakfu kukutumikia, basi nitakabalie. Hakika wewe ni Mwenye kusikia yote, Mjuzi wa yote. [Aal-‘Imraan: 35]

 

 

Na Nabiy Zakariyyah (‘Alayhis-Salaam) alipoomba:

 

هُنَالِكَ دَعَا زَكَرِيَّا رَبَّهُ ۖ قَالَ رَبِّ هَبْ لِي مِن لَّدُنكَ ذُرِّيَّةً طَيِّبَةً ۖ إِنَّكَ سَمِيعُ الدُّعَاءِ ﴿٣٨﴾

Hapo hapo Zakariyyaa akamwomba Rabb wake, akasema: Rabb wangu Nitunukie kutoka Kwako kizazi chema hakika Wewe ni Mwenye kusikia du’aa yangu. [Aal-‘Imraan: 38]

 

 

 

5-Jikinge na Du’aa isiyosikilizwa na Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Ambaye ni As-Samiy’u kama ilivyothibiti katika du’aa ya Sunnah:

 

 

للَّهُمَّ إِنِّي أَعُوذُ بِكَ مِنْ قَلْبٍ لاَ يَخْشَعُ وَمِنْ دُعَاءٍ لاَ يُسْمَعُ وَمِنْ نَفْسٍ لاَ تَشْبَعُ وَمِنْ عِلْمٍ لاَ يَنْفَعُ أَعُوذُ بِكَ مِنْ هَؤُلآءِ الأَرْبَعِ

 

Allaahumma inniy a’uwdhu bika min-qalbin-laa yakh-sha’u, wamin du’aain-laa yasma’u, wamin nafsin-laa tashba’u, wamin ilmin-laa yanfa’u, a’uwdhu bika min haaulail-arba’i

 

Ee Allaah, hakika mimi najikinga moyo usionyenyekea na du’aa isiyosikizwa na nafsi isiyoshiba na elimu isiyonufaisha, najikinga Kwako dhidi ya haya manne.

 

[Abuu Daawuwd, At-Tirmidhiy, Swahiyh An-Nasaaiy, Swahiyh Al-Jaami’ (1297)]

 

 

Bali omba Allaah ('Azza wa Jalla) Akunufaisha kwa masikio yako:

 

 

للَّهُمَّ مَتِّعْنِي بِسَمْعِي وَبَصَرِي  وَاجْعَلْهُمَا الْوَارِثَ مِنِّي وَانْصُرْنِي عَلَى مَنْ يَظْلِمُنِي وَخُذْ مِنْهُ بِثَأْرِي

Allaahumma matti’-niy bisam-’iy, wa baswariy, waj-’al-humal-waaritha minniy, wanswurniy ‘alaa man yadhwlimuniy, wa khudh minhu bitha-ariy

 

Ee Allaah, ninufaishe kwa masikio yangu, na macho yangu, na vijaalie viwili hivyo viwe wiratha wangu (viimarishe mpaka kufa kwangu) na ninusuru dhidi ya anayenidhulumu, na nilipizie dhidi yake.

 

[At-Tirmidhiy Taz Swahiyh At-Tirmidhiy (3/188)]

 

 

Na jikinge na shari za masikio:

 

أللَّهُمَّ إِنِّي أَعُوذُ بِكَ مِنْ شَرِّ سَمْعِي وَمِنْ شَرِّ بَصَرِي وَمِنْ شَرِّ لِسَانِي وَمِنْ شَرِّ قَلْبِي وَمِنْ شَرِّ مَنِيِّي

 

Allaahumma inniy a’uwdhu bika min sharri sam-’iy wamin sharri baswariy, wamin sharri lisaaniy wamin sharri qalbiy, wamin sharri maniyyi

 

Ee Allaah, hakika mimi najikinga Kwako shari ya masikio yangu na shari ya macho yangu, na shari ya ulimi wangu, na shari ya moyo wangu, na shari ya manii yangu

 

 

[Abuu Daawuwd , At-Tirmidhiy, An-Nasaaiy –Swahiyh At-Tirmidhiy (3/166) na Swahiyh An-Nasaaiy (3/1108)]

 

 

 

6-Omba du’aa ya kijikinga na kila shari ambayo kila siku asubuhi na jioni utamdhukuru Allaah ('Azza wa Jalla) kwa Jina na Sifa hii tukufu ya As-Samiy’u; nayo ni du’aa iliyothibiti katika Sunnah kuwa ni katika Adhkaar za asubuhi na jioni; imekuja katika Hadiyth ifuatayo:

 

 عَنْ أَبَانَ بْنِ عُثْمَانَ، قَالَ سَمِعْتُ عُثْمَانَ بْنَ عَفَّانَ، رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ وَهُوَ يَقُولُ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ مَنْ قَالَ فِي أَوَّلِ يَوْمِهِ أَوْ فِي أَوَّلِ لَيْلَتِهِ بِسْمِ اللَّهِ الَّذِي لَا يَضُرُّ مَعَ اسْمِهِ شَيْءٌ فِي الْأَرْضِ وَلَا فِي السَّمَاءِ وَهُوَ السَّمِيعُ الْعَلِيمُ ثَلَاثَ مَرَّاتٍ لَمْ يَضُرَّهُ شَيْءٌ فِي ذَلِكَ الْيَوْمِ أَوْ فِي تِلْكَ اللَّيْلَةِ‏.‏

 

Amesimulia ‘Abaan bin ‘Uthmaan kwamba kamsikia ‘Uthmaan bin ‘Affaan (Radhwiya Allaahu ‘anhu) akisema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Atakayesema mwanzoni wa siku yake au usiku wake:

 

بِسْمِ اللَّهِ الَّذِي لَا يَضُرُّ مَعَ اسْمِهِ شَيْءٌ فِي الْأَرْضِ وَلَا فِي السَّمَاءِ وَهُوَ السَّمِيعُ الْعَلِيمُ

BismiLLaahiLLadhiy laa yadhwuru ma’-Smihi shay-un fil-ardhwi walaa fissamaai wa Huwas-Samiy’ul-‘Aliym

(Kwa jina la Allaah Ambaye hakidhuru kwa jina Lake kitu chochote kile kilicho ardhini, wala mbinguni, Naye ni Mwenye Kusikia yote daima Mjuzi wa yote daima)

 

Mara tatu; hakuna chochote kile kitakachomdhuru siku hiyo au usiku huo.”  [Musnad Ahmad na riwaaya nyenginezo kama hizo za Abu Daawuwd (4/323) [5089, 5088]. At-Tirmidhiy (5/465) [3388], Ibn Maajah [3869], Taz Swahiyh Ibn Maajah (2/332), Swahiyh Abi Daawuwd (5088), Swahiyh Al-Jaami’ (5745)]

 

 

 

 

Share