A-Majina Ya Swahaba: Maana, Wasifu Wao Kwa Mukhtasari: 'Abu 'Ubaydah Bin Aamir Al-Jarraah

 

A-Majina Ya Swahaba: Maana, Wasifu Wao Kwa Mukhtasari

 

Abu ‘Ubaydah 'Aamir Bin Al-Jarraah  (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ)

 

 

Alhidaaya.com

 

 

 

 

Jina Lake:‘ Abu ‘Ubayadah ‘Aamir bin Al-Jarraah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ)

 

(Al-Qurayshiyy)

أبو عبيدة عامر بن الجرّاح

 

Maana Yake: ‘Ubaydah ni Mja au Mtumishi wa Allaah

 

 

 

Wasifu Wake:

 

 

Abu ‘Ubaydah Bin Al-Jarraah ni Swahaba aliyejulikana  kuwa ni  hakimu mwaminifu.

 

 

Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alimpa jukumu la kuliongoza jeshi lililokwenda kumsaidia ‘Amru bin Al-‘Aasw (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ)  katika vita vilivyojulikana kwa jina la 'Dhaatus Salaasil'. Katika vita hivyo alipewa uongozi wa jeshi ambalo ndani yake alikuwemo Abu Bakr na ‘Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا).

 

 

Abu ‘Ubaydah  Bin Al-Jarraah   ni Swahaba ambaye Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم)  alisema kuhusu yake: "Hakika kila umma una mwaminifu wake, na mwaminifu wa Umma huu ni Abu ‘Ubaydah ‘Aamir bin Al-Jarraah."

 

 

Abu ‘Ubaydah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) alikuwa mwenye uso mkunjufu, mwembamba, mrefu, na jicho hutulia na kufurahi kila linapomuona.  Alikuwa mpole mwenye huruma.

 

 

‘Abdullaah bin ‘Umar bin Al Khattwaab (رَضِيَ اللهُ عَنْهما) alisema juu yake: "Watatu katika ma-Quraysh walikuwa wenye nyuso kunjufu, mwenendo na tabia njema, wingi wa hayaa, na hawasemi uongo wanapozungumza na wala hawakukadhibishi unapozungumza nao; Abu Bakr Asw-Swiddiyq, ‘Uthmaan bin ‘Affaan na Abu ‘Ubaydah bin Al-Jarraah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمْ)."

 

 

 

Kufariki Kwake:

 

 

Abu ‘Ubaydah 'Aamir Bin Al-Jarraah  alifariki dunia akiwa na umri wa miaka 58 kwa ugonjwa wa tauni uliojulikana kwa jina la ‘Twa’uwn Amuwaas’  kutokana na jina la mji wa Amuwaas (Jordan) ulioshambuliwa na maradhi hayo. Na hii ilikuwa katika mwaka wa kumi na nane (18), na wengine wakasema kuwa amefariki katika mwaka wa kumi na saba (17) Hijriyyah.

 

 

 

Share