04-Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Miujiza Yake: Wanyama Kuzungumza Na Swahaba

Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

04-Miujiza Yake: Wanyama Kuzungumza Na Swahaba

 

Alhidaaya.com

 

 

Miongoni mwa miujiza yake Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم) ni kwamba baadhi ya Wanyama walizungumza na wana-Aadam; mmojawapo ni mbwa mwitu aliyezungumza na Swahaba karibu na mji wa Madiynah kama ilivyothibiti katika Hadiyth ifuatayo:

 

حَدَّثَنَا يَزِيدُ، أَخْبَرَنَا الْقَاسِمُ بْنُ الْفَضْلِ الْحُدَّانِيُّ، عَنْ أَبِي نَضْرَةَ، عَنْ أَبِي سَعِيدٍ الْخُدْرِيِّ قَالَ: عَدَا الذِّئْبُ عَلَى شَاةٍ فَأَخَذَهَا، فَطَلَبَهُ الرَّاعِي، فَانْتَزَعَهَا مِنْهُ فَأَقْعَى الذِّئْبُ عَلَى ذَنَبِهِ قَالَ: أَلَا تَتَّقِي اللَّهَ تَنْزِعُ مِنِّي رِزْقًا سَاقَهُ اللَّهُ إِلَيَّ. فَقَالَ: يَا عَجَبِي ذِئْبٌ مُقْعٍ عَلَى ذَنَبِهِ يُكَلِّمُنِي كَلَامَ الْإِنْسِ. فَقَالَ الذِّئْبُ: أَلَا أُخْبِرُكَ بِأَعْجَبَ مِنْ ذَلِكَ، مُحَمَّدٌ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ بِيَثْرِبَ، يُخْبِرُ النَّاسَ بِأَنْبَاءِ مَا قَدْ سَبَقَ. قَالَ: فَأَقْبَلَ الرَّاعِي يَسُوقُ غَنَمَهُ حَتَّى دَخَلَ الْمَدِينَةَ، فَزَوَاهَا إِلَى زَاوِيَةٍ مِنْ زَوَايَاهَا، ثُمَّ أَتَى رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَأَخْبَرَهُ فَأَمَرَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَنُودِيَ: الصَّلَاةُ جَامِعَةٌ، ثُمَّ خَرَجَ فَقَالَ لِلرَّاعِي: أَخْبِرْهُمْ فَأَخْبَرَهُمْ. فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: صَدَقَ وَالَّذِي نَفْسِي، بِيَدِهِ لَا تَقُومُ السَّاعَةُ حَتَّى يُكَلِّمَ السِّبَاعُ الْإِنْسَ، وَيُكَلِّمَ الرَّجُلَ عَذَبَةُ سَوْطِهِ، وَشِرَاكُ نَعْلِهِ، وَيُخْبِرَهُ فَخِذُهُ بِمَا أَحْدَثَ أَهْلُهُ بَعْدَهُروى الإمام أحمد في مسنده (3/ 83 - 84

 

Amesimulia Abu Sa'iyd Al-Khudriyy (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) kwamba: Mchunga kondoo alipokuwa na kondoo zake, mara mbwa mwitu alimshambulia kondoo na kuondoka naye, mchunga kondoo akamkimbiza mbwa mwitu na akamrejesha kondoo, mbwa mwitu akakalia mkia wake na akamwambia mchunga kondoo: "Mche Allaah! Umechukua rizqi yangu Alonijaalia Allaah!” Mchunga kondoo akasema: "Ajabu! Mbwa mwitu anakalia mkia wake na kuzungumza na mimi kwa lugha ya kibin-Aadam." Mbwa mwitu akasema: "Je nikuambie jambo la ajabu zaidi kuliko hilo? Yupo Muhammad (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم) huko Yathrib (Al-Madiynah) akiwajulisha watu kuhusu khabari za kale." Basi mchunga kondoo akaenda (upande wa Al-Madiynah) huku akiwaswaga kondoo wake mpaka akafika Al-Madiynah, akawazuia kondoo wake mahali, na akaja kwa Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم) na kusimulia kisa chote. Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم) akaamuru iadhiniwe Adhaan ya Swalaah ya Jamaa, kisha akatoka na kumwomba mchunga kondoo awaambie watu na akawaambia. Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم) akasema: "Amesema kweli. Naapa kwa Ambaye Mikononi Mwake ipo nafsi yangu, Siku ya Qiyaamah haitasimama isipokuwa mpaka wanyama wawindao wazungumze na wana-Aadam, na fimbo na kamba za viatu za mtu zizungumze naye na paja lake kumjulisha kuhusu familia yake yaliyowatokea nyuma yake. [Musnad Imaam Ahmad (3: 83 - 84)].

 

 

Na pia ng’ombe alizungumza kama ilivyothibiti katika Hadiyth ifuatayo:

 

حَدَّثَنَا أَبُو الْيَمَانِ، أَخْبَرَنَا شُعَيْبٌ، عَنِ الزُّهْرِيِّ، قَالَ أَخْبَرَنِي أَبُو سَلَمَةَ بْنُ عَبْدِ الرَّحْمَنِ، أَنَّ أَبَا هُرَيْرَةَ ـ رضى الله عنه ـ قَالَ سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم يَقُولُ ‏"‏ بَيْنَمَا رَاعٍ فِي غَنَمِهِ عَدَا عَلَيْهِ الذِّئْبُ، فَأَخَذَ مِنْهَا شَاةً، فَطَلَبَهُ الرَّاعِي، فَالْتَفَتَ إِلَيْهِ الذِّئْبُ فَقَالَ مَنْ لَهَا يَوْمَ السَّبُعِ، يَوْمَ لَيْسَ لَهَا رَاعٍ غَيْرِي، وَبَيْنَا رَجُلٌ يَسُوقُ بَقَرَةً قَدْ حَمَلَ عَلَيْهَا، فَالْتَفَتَتْ إِلَيْهِ فَكَلَّمَتْهُ فَقَالَتْ إِنِّي لَمْ أُخْلَقْ لِهَذَا، وَلَكِنِّي خُلِقْتُ لِلْحَرْثِ ‏"‏‏.‏ قَالَ النَّاسُ سُبْحَانَ اللَّهِ‏.‏ قَالَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم ‏"‏ فَإِنِّي أُومِنُ بِذَلِكَ وَأَبُو بَكْرٍ وَعُمَرُ بْنُ الْخَطَّابِ رضى الله عنهما ‏"‏‏.‏

 

Amesimulia Abu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ)   Nimemsikia Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم) akisema, "Mchunga kondoo alipokuwa na kondoo zake, mbwa mwitu alimvamia na kumchukua kondoo mmoja. Mchunga kondoo alipomkimbiza mbwa mwitu, mbwa mwitu alimgeukia na kumwambia, ‘Nani atakayewalinda katika siku ya wanyama mwitu ambapo hakutakuwa na mchungaji isipokuwa mimi’. Na wakati mtu mmoja alipokuwa akimswaga ng’ombe huku akiwa amembebesha mzigo, alimgeukia na kuzungumza naye akisema, ‘Sikuumbwa kwa ajili hii (yaani, kubeba mzigo), bali kwa ajili ya kulima.’" Watu wakasema, "Subhaana Allaah." Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم) akasema, "Hakika Ninaapa yaamini hayo na pia Abu Bakr na ‘Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا)” [Al-Bukhaariy]

 

 

Share