09-Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Hikmah Zake: Jirani Aliyekuwa Akimuudhi Mwenziwe

 

 

Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Hikmah Zake:

 

09-Jirani Aliyekuwa Akimuudhi Mwenziwe

 

Alhidaaya.com

 

حَدَّثَنَا الرَّبِيعُ بْنُ نَافِعٍ أَبُو تَوْبَةَ، حَدَّثَنَا سُلَيْمَانُ بْنُ حَيَّانَ، عَنْ مُحَمَّدِ بْنِ عَجْلاَنَ، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ، قَالَ جَاءَ رَجُلٌ إِلَى النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم يَشْكُو جَارَهُ فَقَالَ ‏"‏ اذْهَبْ فَاصْبِرْ ‏"‏ ‏.‏ فَأَتَاهُ مَرَّتَيْنِ أَوْ ثَلاَثًا فَقَالَ ‏"‏ اذْهَبْ فَاطْرَحْ مَتَاعَكَ فِي الطَّرِيقِ ‏"‏ ‏.‏ فَطَرَحَ مَتَاعَهُ فِي الطَّرِيقِ فَجَعَلَ النَّاسُ يَسْأَلُونَهُ فَيُخْبِرُهُمْ خَبَرَهُ فَجَعَلَ النَّاسُ يَلْعَنُونَهُ فَعَلَ اللَّهُ بِهِ وَفَعَلَ وَفَعَلَ فَجَاءَ إِلَيْهِ جَارُهُ فَقَالَ لَهُ ارْجِعْ لاَ تَرَى مِنِّي شَيْئًا تَكْرَهُهُ ‏

 

Amesimulia Abuu Hurayrah  (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) : Mtu mmoja alikuja kwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم) akimshtakia kuhusu jirani yake akamwambia: “Nenda na uvute subra.” Akamjia tena mara mbili au tatu. Kisha akamwambia: “Nenda katupe vitu vyako njiani.”  Akatupa vitu vyake njiani, basi pindi watu walipopita na kumuuliza aliwahadithia (kuhusu maudhi ya jirani yake) wakawa wanamlaani na kumuombea Allaah Amfanyie kadhaa wa kadhaa. Akamjia yule jirani yake akamwambia: “Rudi hutopata kuona tena kutoka kwangu ya kukuchukiza.” 

 

[Sunan Abiy Daawuwd Kitaab Al-Adab na ameisahihisha Al-Albaaniy katika Swahiyh Abiy Daawuwd (5153)]

 

Share