04-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Kupendeza Kuacha Mavazi ya Kifahari kwa Sababu ya Unyenyekevu

 

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

 

باب استحباب ترك الترفع في اللباس تواضعاً

04-Mlango Wa Kupendeza Kuacha Mavazi ya Kifahari kwa Sababu ya Unyenyekevu

 

Alhidaaya.com

 

 

 

قَدْ سَبَقَ في بَابِ فَضْل الجُوعِ وَخشُونَةِ العَيْشِ جُمَلٌ تَتَعَلَّقُ بهذا الباب .

Tumetaja katika mlango wa fadhila za kuwa katika hali ya njaa na dhiki za kimaisha jumla ya Hadiythi zinazuhusiana na mlango huu.

 

 

وعن معاذ بن أنسٍ رضي الله عنه : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : ((  مَنْ تَرَكَ اللِّبَاس تَوَاضُعاً للهِ ، وَهُوَ يَقْدِرُ عَلَيْهِ ، دَعَاهُ اللهُ يَومَ القِيَامَةِ عَلَى رُؤوسِ الخَلائِقِ حَتَّى يُخَيِّرَهُ مِنْ أيِّ حُلَلِ الإيمَانِ شَاءَ يَلْبَسُهَا )) رواه الترمذي ، وقال : (( حديث حسن )) .

Imepokewa kutoka kwa Mu'aadh bin Anas (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mwenye  kuacha mavazi ya gharama japokuwa ana uwezo huo kwa unyenyekevu kwa ajili ya Allaah basi atatanguliza kuitwa na Allaah Siku wa Qiyaamah mbele ya viumbe vyote mpaka apatiwe fursa ya kuchagua vazi lolote la Imaani analolitaka." [At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan]

 

 

 

Share