03-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Adabu za Salam

 

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

 

باب آداب السلام

03-Mlango Wa Adabu za Salam

 

Alhidaaya.com

 

 

Hadiyth – 1

عن أَبي هريرة رضي الله عنه : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( يُسَلِّمُ الرَّاكِبُ عَلَى المَاشِي ، وَالمَاشِي عَلَى القَاعِدِ ، وَالقَليلُ عَلَى الكَثِيرِ )) متفقٌ عَلَيْهِ .

وفي رواية للبخاري : (( والصغيرُ عَلَى الكَبيرِ )) .

Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Aliyepanda atamsalimia anayetembea kwa miguu, na anayetembea kwa miguu atamsalimia aliyekaa na wachache watawasalimia walio wengi." [Al-Bukhaariy, Muslim, Abu Daawuwd na At-Tirmidhiy]

Na katika riwaayah ya Al-Bukhaariy: "Na mtoto atamsalimia mkubwa."

 

 

Hadiyth – 2

وعن أَبي أُمَامَة صُدَيِّ بن عجلان الباهِلي رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم : (( إنَّ أَوْلى النَّاسِ بِاللهِ مَنْ بَدَأهُمْ بِالسَّلامِ )) رواه أَبُو داود بإسنادٍ جيدٍ .

ورواه الترمذي عن أَبي أُمَامَةَ رضي الله عنه ، قِيلَ : يَا رسول الله ، الرَّجُلانِ يَلْتَقِيَانِ أَيُّهُمَا يَبْدَأُ بِالسَّلاَمِ ؟ ، قَالَ : (( أَوْلاَهُمَا بِاللهِ تَعَالَى )) قَالَ الترمذي : (( هَذَا حديث حسن )) .

Imepokewa kutoka kwa Abu Umamah Swudayy bin 'Ajlaan Al-Baahiliy (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Hakika aliye karibu zaidi na Allaah ni yule anayeanza kutoka salamu." [Abu Daawuwd kwa Isnaad nzuri].

Na ameipokea At-Tirmidhiy kutoka kwa Abu Umamah (Radhwiya Allaahu 'anhu): Aliulizwa: "Ee Rasuli wa Allaah! Watu wawili wanaokutana, ni yupi anayefaa kutoa salamu?" Akasema: "Yule aliye karibu na Allaah Ta'aalaa." [At-Tirmidhiy na akasema ni Hadiyth Hasan].

 

 

 

Share