02-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Kupendeza Kusafiri kwa Kikundi Chini ya Kiongozi na Kumtii

 

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

 

باب استحباب طلب الرفقة وتأميرهم عَلَى أنفسهم واحداً يطيعونه

02-Mlango Wa Kupendeza Kusafiri kwa Kikundi Chini ya Kiongozi na Kumtii

 

Alhidaaya.com

 

Hadiyth – 1

عن ابن عمرَ رضي اللهُ عنهما ، قَالَ : قَالَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم : ((  لَوْ أنَّ النَّاسَ يَعْلَمُونَ مِنَ الوحدَةِ مَا أعْلَمُ، مَا سَارَ رَاكبٌ بِلَيْلٍ وَحْدَهُ ! )) رواه البخاري.

Imepokewa Kutoka kwa Ibn 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Lau kwamba watu wangejua katika upweke ninayoyajua, basi msafiri asingekwenda usiku hali ya kuwa peke yake." [Al-Bukhaariy]

 

 

Hadiyth – 2

وعن عمرِو بن شُعَيْبٍ، عن أبيه، عن جَدهِ رضي الله عنه، قَالَ : قَالَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم : ((  الرَّاكِبُ شَيْطَانٌ ، وَالرَّاكِبَانِ شَيْطَانَانِ ، وَالثَّلاَثَةُ رَكْبٌ )) رواه أَبُو داود والترمذي والنسائي بأسانيد صحيحةٍ ، وقال الترمذي : (( حديث حسن )) .

Imepokewa kutoka kwa 'Amru bin Shu'ayb kutoka kwa babake kutoka kwa babu yake (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Msafiri mmoja ni shetani, na wasafiri wawili ni mashetani wawili na wasafiri watatu ni msafara." [Abu Daawuwd, At-Tirmidhiy na An-Nasaai kwa Isnaad Swahiyh na akasema At-Tirmidhiy ni Hadiyth Hasan]

 

 

Hadiyth – 3

وعن أَبي سعيد وأبي هُريرة رضي اللهُ تَعَالَى عنهما، قالا : قَالَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم : ((  إِذَا خَرَجَ ثَلاَثَةٌ في سَفَرٍ فَليُؤَمِّرُوا أحَدَهُمْ )) حديث حسن ، رواه أَبُو داود بإسنادٍ حسن .

Imepokewa kutoka kwa Abu Sa'iyd Al-Khudriy na Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Wakitoka watu watatu katika safari wamfanye mmoja wao kiongozi." [Hadiyth Hasan, Abu Daawuwd kwa Isnaad iliyo Hasan]

 

 

Hadiyth – 4

وعن ابن عبّاسٍ رضي الله عنهما ، عن النبيِّ صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : ((  خَيْرُ الصَّحَابَةِ أرْبَعَةٌ ، وَخَيْرُ السَّرَايَا أرْبَعُمِئَةٍ ، وَخَيْرُ الجُيُوشِ أرْبَعَةُ آلاَفٍ ، وَلَنْ يُغْلَبَ اثْنَا عَشَرَ ألْفاً مِنْ قِلةٍ )) رواه أَبُو داود والترمذي، وقال : (( حديث حسن )).

Imepokewa kutoka kwa Ibn 'Abbaas (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Bora wa masahibu katika kikundi ni wanne, na bora wa kipote kidogo cha jeshi ni watu mia nne na bora wa jeshi ni elfu nne na jeshi la watu elfu kumi na mbili haliwezi kushindwa kwa sababu ya uchache." [Abu Daawuwd na At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan]

 

Share