Skip navigation.
Home kabah

Asbaabun-Nuzuul (Sababu Ya Kuteremshwa) Surat Al-Ikhlaasw


 

Sababu Ya Kuteremka Surah hii ni kwamba Washirikina wa Makkah walimuuliza Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kuhusu ukoo wa Allaah,

عن أبي بن كعب أن المشركين قالوا لرسول الله صلى الله عليه وسلم: انسب لنا ربك فأنزل الله تعالى (قُل هُوَ اللهُ أَحَدٌ اللهُ الصَمَدُ) قال: فالصمد الذي لم يلد ولم يولد لأنه ليس شيء يولد إلا سيموت وليس شيء يموت إلا سيورث وإن الله تعالى لا يموت ولا يورث (وَلَم يَكُن لَّهُ كُفُواً أَحَد) قال: لم يكن له شبيه ولا عدل وليس كمثله شي

 


Kutoka kwa Ubay bin Ka'ab kwamba Washirikina (makafiri) walimwambia  Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) tuhusishe (tujulishe nani aliyehusiana Naye) Mola wako. Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Akateremsha

(( قُل هُوَ اللهُ أَحَدٌ اللهُ الصَمَدُ))  

((Sema, Yeye Allaah ni wa pekee)) [Al-Ikhlaasw: 112].

 

Akasema 'Aswamad' (Mkusudiwa) ambaye Hakuzaa wala hakuzaliwa kwa sababu hakuna kitu kinachozaliwa isipokuwa kitakufa na hakuna kitu kitakachokufa isipokuwa kitarithiwa, na Allaah Hafi wala Harithiwi ((Wa Lam yaku-Llahu kufuwan Ahad)) ((Wala hana anayefanana Naye hata mmoja)) Akasema: Hakuna anayefanana Naye wala aliye sawa na hapana kitu kama mfano Wake

SALAAM ALEIKUM NAULIZA

SALAAM ALEIKUM
NAULIZA SWALI:
MIMI NINA BIASHARA AMBAYO NIMECHUKUA KWA MKOPO NA IKAWA SIJAMLIZA KULIPA MKOPO IKAFIKIA MWAKA NA NIKAWA NA NIA YA KUTOA ZAKA. JEE INAWEZEKANA KUAHIRISHA KUTOA ZAKA ILI NIMALIZE KULIPA DENI AMBALO WALONIKOPESHA WANAHIMIZA?
NAITWA RASHID KUTOKA ZANZIBAR

Wa 'alaykumus-salaam Wa

Wa 'alaykumus-salaam Wa RahmatuLLaahi Wa Barakaatuh

Tumepokea Swali lako lakini tunasikitika kuwa hapa sipo mahali pa kuuliza maswali bali ni sehemu ya kuweka maoni kuhusiana na Makala mbali mbali n.k. Mfano hapa ilipasa uweke maoni kuhusu Makala hiyo ya Sababu ya Kuteremshwa Suratul-Ikhlaasw' kwa vile ndiko ulikochagua kutuandikia.

Hivyo tuma swali lako kwa kuingia sehemu ya 'Wasiliana Na Sisi ' iliyoko hapo juu kisha utume kwa kuchagua 'Tuma Maswali' au tumia anuani ya maswali@alhidaaya.com kutoka e-mail yako moja kwa moja.

Tunakuombeni ndugu zetu nyote ushirikiano wenu katika kutufanyia wepesi kutekeleza hizi kazi kwa kufuata njia zipasazo kutuma maswali na pia kufuata taratibu zake, kutuma maoni n.k kwani hakika hizi kazi ni nyingi mno na watendaje ni wachache, hivyo inakuwa vigumu sana kutekeleza maombi yenu pamoja na kukamilisha hizi kazi.

Tunatumai nyote mtafahamu hali hii na ushirikiano wenu pamoja na du'aa zenu ndizo tunazozihitaji ili tuweze kuendelea kuwanufaisha kwa yale tuliyojaaliwa.

Ndugu Zenu
AL HIDAAYA