12-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Fadhila ya Swalah ya Jamaa

 

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

 

باب فضل صلاة الجماعة

12-Mlango Wa Fadhila ya Swalah ya Jamaa

 

Alhidaaya.com

 

Hadiyth – 1

عن ابن عمر رضي الله عنهما : أنَّ رَسُول اللهِ صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( صَلاَةُ الْجَمَاعَة أفْضَلُ مِنْ صَلاَةِ الْفَذِّ بِسَبْعٍ وَعِشْرِينَ دَرَجَةً )) متفقٌ عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwa Ibn 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Swalaah ya jamaa inazidi Swalaah ya mtu peke yake kwa daraja ishirini na saba (27)." [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

Hadiyth – 2

وعن أبي هريرة رضي الله عنه ، قَالَ : قال رَسُولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم : (( صَلاةُ الرَّجُلِ في جَمَاعةٍ تُضَعَّفُ عَلَى صَلاتِهِ فِي بَيْتهِ وفي سُوقِهِ خَمْساً وَعِشْرِينَ ضِعْفَاً ، وَذلِكَ أَنَّهُ إذَا تَوَضَّأ فَأحْسَنَ الوُضُوءَ ، ثُمَّ خَرَجَ إلى المَسْجِدِ ، لا يُخرِجُهُ إلاَّ الصَّلاةُ ، لَمْ يَخْطُ خَطْوَةً إلاَّ رُفِعَتْ لَهُ بِهَا دَرَجَةٌ ، وَحُطَّتْ عَنهُ بِهَا خَطِيئَةٌ ، فَإذَا صَلَّى لَمْ تَزَلِ المَلائِكَةُ تُصَلِّي عَلَيْهِ مَا دَامَ في مُصَلاَّهُ ، مَا لَمْ يُحْدِث ، تقولُ : اللَّهُمَّ صَلِّ عَلَيهِ ، اللَّهُمَّ ارْحَمْهُ ، وَلاَ يَزَالُ في صَلاةٍ مَا انْتَظَرَ الصَّلاَةَ )) متفقٌ عَلَيهِ ، وهذا لفظ البخاري .

Imepokewa kutoka kwa Abuu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Swalaah ya jamaa inazidi Swalaah ya mtu nyumbani kwake, na Swalaah yake sokoni kwake kwa daraja ishirini na tano (25). Hakika mmoja wenu atakapotawadha na akafanya uzuri wudhuu wake na akaja Msikitini hakusudii jingine ila Swalaah, basi hapigi hatua moja ila Allaah atamnyanyua kwa kila hatua daraja na utamuondoshea kwa kila hatua kosa mpaka aingie Msikitini na anpoingia Msikitini atakuwa katika Swalaah muda wa kuwa Swalaah ndiyo inamzuia, na Malaaikah wanamtakia rehema madamu yupo katika kikao chake anachoswalia. Wakisema: 'Ee Mola wetu msamehe, ee Mola wetu mrehemu.' Na anaendelea kuwa katika Swalaah madamu anaingojea Swalaah." [Al-Bukhaariy na Muslim, na hii ni lafdhi ya Al-Bukhaariy]

 

Hadiyth – 3

وعن أبي هريرة رضي الله عنه ، قَالَ : أَتَى النبيَّ صلى الله عليه وسلم رَجُلٌ أعْمَى ، فقَالَ : يا رَسُولَ اللهِ ، لَيسَ لِي قَائِدٌ يَقُودُنِي إلى الْمَسْجِدِ ، فَسَأَلَ رَسُولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم أنْ يُرَخِّصَ لَهُ فَيُصَلِّي فِي بَيْتِهِ ، فَرَخَّصَ لَهُ ، فَلَّمَا وَلَّى دَعَاهُ ، فَقَالَ لَهُ : (( هَلْ تَسْمَعُ النِّدَاءَ بِالصَّلاَةِ ؟ )) قَالَ : نَعَمْ . قَالَ : (( فَأجِبْ )) رواه مُسلِم .

Imepokewa kutoka kwa Abuu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba alikuja mtu kipofu alimwambia: "Ee Rasuli wa Allaah! mimi sina wa kuniongoza kwenda Msikitini", hivyo akamtaka Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amruhusu kuswali nyumbani kwake. Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alimruhusu na alipoondoka akamwita na kumuuliza: "Je, unasikia adhana?" Akasema: "Ndio." Akasema: "Basi itikia wito." [Muslim]

 

Hadiyth – 4

وعن عبدِ الله – وقيل : عَمْرو بن قَيسٍ - المعروف بابن أُمّ مكتوم المؤذن رضي الله عنه أنَّه قَالَ: يا رَسُول اللهِ ، إنَّ المَدينَةَ كَثيرةُ الهَوَامِّ وَالسِّبَاعِ . فَقَالَ رَسُول اللهِ صلى الله عليه وسلم : (( تَسْمَعُ حَيَّ عَلَى الصَّلاةِ حَيَّ عَلَى الفَلاحِ ، فَحَيَّهلاً )) رَوَاهُ أبُو دَاوُدَ بإسناد حسن .

Imepokewa kutoka kwa 'Abdillaah, na kulisemwa 'Amru bin Qays (Radhwiya Allaahu 'anhu) maarufu kwa jina la Ibn Umma Maktuum muadhini wa Nabiy kuwa yeye amesema: "Ee Rasuli wa Allaah! Hakika mji wa Madiynah una wadudu wengi na wanyama wabaya." Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) Akasema: "Unasikia Hayya 'alasw Swalaah, Hayya 'alai Falaah (Njooni kwenye Swalaah, njooni kwenye kheri yaani adhana), hivyo njoo Msikitini." [Abuu Daawuwd kwa Isnaad Hasan]

 

Hadiyth – 5

وعن أبي هريرة رضي الله عنه : أنَّ رَسُول اللهِ صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( وَالَّذِي نَفْسِي بِيَدِهِ ، لَقَدْ هَمَمْتُ أنْ آمُرَ بحَطَبٍ فَيُحْتَطَبَ ، ثُمَّ آمُرَ بِالصَّلاَةِ فَيُؤذَّنَ لهَا ، ثُمَّ آمُرَ رَجُلاً فَيَؤُمَّ النَّاسَ ، ثُمَّ أُخَالِفَ إلى رِجَالٍ فَأُحَرِّقَ عَلَيْهِمْ بُيُوتَهمْ )) متفقٌ عَلَيهِ .

Imepokewa kutoka kwa Abuu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Naapa kwa Allaah ambaye nafsi yangu iko mikononi mwake hakika nilitaka kuamrisha ziletwe kuni na ziwashwe, kisha niamrishe Swalaah iadhiniwe, kisha niamrisha mtu awaswalishe watu. Kisha niwaendee watu ambao hawakuhudhura Swalaah ya jamaa nizichome nyumba zao." [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

Hadiyth – 6

وعن ابن مسعود رضي الله عنه ، قَالَ : مَنْ سَرَّهُ أنْ يَلْقَى اللهَ تَعَالَى غداً مُسْلِماً ، فَلْيُحَافِظْ عَلَى هؤُلاَءِ الصَّلَوَاتِ حَيْثُ يُنَادَى بِهِنَّ ، فَإنَّ اللهَ شَرَعَ لِنَبِيِّكم صلى الله عليه وسلم سُنَنَ الهُدَى ، وَإنَّهُنَّ مِنْ سُنَنِ الهُدَى ، وَلَوْ أنَّكُمْ صَلَّيْتُمْ في بُيُوتِكم كَمَا يُصَلِّي هذا المُتَخَلِّفُ فِي بَيْتِهِ لَتَرَكْتُمْ سُنَّةَ نَبِيِّكُمْ ، وَلَوْ تَرَكْتُمْ سُنَّة نَبِيِّكُم لَضَلَلْتُمْ ، وَلَقَدْ رَأيْتُنَا وَمَا يَتَخَلَّفُ عَنْهَا إلاَّ مُنَافِقٌ مَعْلُومُ النِّفَاقِ ، وَلَقَدْ كَانَ الرَّجُلُ يُؤتَى بهِ ، يُهَادَى بَيْنَ الرَّجُلَيْنِ حَتَّى يُقَامَ في الصَّفِّ . رَوَاهُ مُسلِم .

وفي رواية لَهُ قَالَ : إنّ رَسُول اللهِ صلى الله عليه وسلم عَلَّمَنَا سُنَنَ الهُدَى ؛ وإنَّ مِنْ سُنَنِ الهُدَى الصَّلاَةَ في المَسْجِدِ الَّذِي يُؤَذَّنُ فِيهِ .

Ibn Mas'uwd (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: Mwenye kupenda kukutana na Allaah Ta'aalaa kesho akiwa Muislamu basi azihifadhi hizi Swalaah tano anapoitwa kwazo. Hakika Allaah ameweka kwa Nabiy wenu (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) Sunnah za uwongofu na kwa hakika hizo (Swalaah) ni sunnah za uwongofu. Na lau nyinyi mtaswali majumbani mwenu kama anavyoswali huyu anayebaki nyuma katika nyumba yake mtakuwa mumeacha sunnah ya Nabiy wenu. Na lau mtaacha Sunnah ya Nabiy wenu basi mutapotea. Ungetuona ilikuwa mtu hawezi kuacha Swalaah ya jamaa isipokuwa mnafiki anayejulikana unafiki wake, na ilikuwa mtu huletwa hali ya kuwa amebebwa na watu wawili na anawekwa kwenye safu katika hali hiyo." [Mulim]

Na katika riwaayah yake nyengine amesema: "Hakika Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ametufundisha Sunnah za uwongofu na hakika miongoni mwa Sunnah za uwongofu ni kuswali kwenye Msikiti unaoadhiniwa ndani yake."

 

Hadiyth – 7

وعن أبي الدرداء رضي الله عنه ، قال : سمعت رَسُول اللهِ صلى الله عليه وسلم ، يقول : (( مَا مِنْ ثَلاثَةٍ فِي قَرْيةٍ ، وَلاَ بَدْوٍ ، لا تُقَامُ فِيهِمُ الصَّلاَةُ إلاَّ قَد اسْتَحْوَذَ عَلَيْهِم الشَّيْطَانُ . فَعَلَيْكُمْ بِالجَمَاعَةِ ، فَإنَّمَا يَأْكُلُ الذِّئْبُ مِنَ الغَنَمِ القَاصِيَة )) رَوَاهُ أبُو دَاوُدَ بإسناد حسن .

Abuu Dardaa (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: "Hakuna watu watatu katika kijiji au kitongoji ambako haisimamishwi hapo Swalaah ya jamaa isipokuwa watakuwa wamepotezwa na shetani, basi jilazimisheni kusimamisha jamaa kwani mbwa mwitu humla kondoo aliyejitenga." [Abuu Daawuwd kwa Isnaad Hasan]

 

 

 

Share