16-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Fadhila za Swalaah za Sunnah Rawatib Pamoja na Faradhi na Kubainisha Uchache na Utimilifu Wake na Zilizo Baina Yake

 

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

 

باب فضل السنن الراتبة مع الفرائض

وبيان أقلها وأكملها وما بينهما

16-Mlango Wa Fadhila za Swalaah za Sunnah Rawatib Pamoja na Faradhi na Kubainisha Uchache na Utimilifu Wake na Zilizo Baina Yake

 

Alhidaaya.com

 

Hadiyth – 1

وعن أُمِّ المُؤْمِنِينَ أُمِّ حَبِيبَةَ رملة بِنْتِ أبي سُفْيَانَ رَضِيَ اللهُ عَنهما ، قالت : سمعت رَسُولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم ، يقول : (( مَا مِنْ عَبْدٍ مُسْلِمٍ يُصَلِّي للهِ تَعَالى كُلَّ يَوْمٍ ثِنْتَيْ عَشرَةَ رَكْعَةً تَطَوُّعاً غَيرَ الفَرِيضَةِ ، إلاَّ بَنَى الله لَهُ بَيْتاً في الجَنَّةِ ، أو إلاَّ بُنِيَ لَهُ بَيْتٌ فِي الجَنَّةِ )) رواه مُسلِمٌ .

Imepokewa kutoka kwa Mama wa Waumini, Ummu Habibah Ramlah bint Abu Sufyaan (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) ambaye amesema: Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: "Hakuna mja Muislamu ataswali kwa ajili ya Allaah Ta'aalaa kila siku Rakaa kumi na mbili za nyongeza (kwa hiyari yake) zisizokuwa za faradhi isipokuwa Allaah Humjengea nyumba Peponi au ila hujengewa yeye nyumba Peponi." [Muslim]

 

Hadiyth – 2

وعن ابن عمر رَضِيَ اللهُ عَنهُما ، قَالَ : صَلَّيْتُ مَعَ رَسُولِ اللهِ صلى الله عليه وسلم ، رَكْعَتَيْنِ قَبْلَ الظُّهْرِ، وَرَكْعَتْينِ بَعْدَهَا، وَرَكْعَتَيْنِ بَعْدَ الجُمُعَةِ ، وَرَكْعَتَينِ بَعدَ المَغْرِبِ ، وَرَكْعَتَينِ بَعدَ العِشَاءِ . متفقٌ عَلَيهِ 

Na Ibn 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) amesema: Niliswali pamoja na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) Rak'ah mbili kabla ya Adhuhuri, na Rak'ah mbili baada yake, Rak'ah mbili baada ya Ijumaa, na Rak'ah mbili baada ya Maghrib na Rak'ah mbili baada ya Isha." [Al-Bukhaariy na Muslim].

 

Hadiyth – 3

وعن عبد الله بن مُغَفَّلٍ رَضِيَ اللهُ عَنهُ ، قَالَ : قال رَسُول اللهِ صلى الله عليه وسلم : (( بَيْنَ كُلِّ أذَانَيْنِ صَلاَةٌ ، بَيْنَ كُلِّ أذَانَيْنِ صَلاَةٌ ، بَيْنَ كل أذانين صلاة )) قال في الثَّالِثةِ : (( لِمَنْ شَاءَ )) متفقٌ عَلَيهِ .

Imepokewa kutoka kwa 'Abdillaah bin Mughaffal kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Baina ya kila adhana mbili kuna Swalaah (makusudio ya adhana mbili ni baina ya adhana na iqamah), baina ya kila adhana mbili kuna Swalaah, baina ya kila adhana mbili kuna Swalaah." Akasema katika mara ya tatu: "Kwa mwenye kupenda." [Al-Bukhaariy, Muslim, Abu Daawuwd, At-Tirmidhiy na An-Nasaai].

 

 

Share