17-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Kuhimiza Rak'ah Mbili za Sunnah ya Asubuhi

 

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

باب تأكيد ركعتي سنّةِ الصبح

17-Mlango Wa Kuhimiza Rak'ah Mbili za Sunnah ya Asubuhi

 

Alhidaaya.com

 

Hadiyth – 1

عن عائشة رَضِيَ اللهُ عَنها : أنَّ النَّبيَّ صلى الله عليه وسلم كَانَ لا يَدَعُ أرْبَعاً قَبْلَ الظُّهْرِ ، وَرَكْعَتَيْنِ قَبْلَ الغَدَاةِ . رَوَاهُ البُخَارِيُّ .

Amehadithia 'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) kuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa haachi Rakaa nne kabla ya Adhuhuri na Rak'ah mbili kabla ya Asubuhi." [Al-Bukhaariy]

 

Hadiyth – 2

وعن عائشة رَضِيَ اللهُ عَنها ، قالت : لَمْ يَكُنِ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم عَلَى شَيْءٍ مِنَ النَّوَافِلِ أشَدَّ تَعَاهُدَاً مِنهُ عَلَى رَكْعَتَي الفَجْرِ . متفقٌ عَلَيهِ .

Na amesema 'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa): Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) hakuwa mwenye kuchunga Swalaah za Nawaafil na kuhimiza sana kuichunga, kuliko Rak'ah mbili za Sunnah ya Swalatul Fajr." [Al-Bukhaariy, Muslim na Abu Daawuwd]

 

Hadiyth – 3

وعن عائشة رَضِيَ اللهُ عَنها ، عن النبيِّ صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( رَكْعَتَا الفَجْرِ خَيْرٌ مِنَ الدنْيَا وَمَا فِيهَا )) رواه مُسلِمٌ . وفي رواية : (( لَهُمَا أحَبُّ إليَّ مِنَ الدنْيَا جَمِيعاً )) .

Imepokewa kutoka kwa 'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Rakaa mbili za Alfajiri ni bora kuliko dunia na vilivyomo ndani yake." [Muslim]

Na katika riwaayah nyingine: "Rakaa mbili hizo zinapendeza zaidi kwangu kuliko dunia yote."

 

Hadiyth – 4

وعن أبي عبد الله بلالِ بن رَبَاح رَضِيَ اللهُ عَنه ، مُؤَذِّن رَسُولِ اللهِ صلى الله عليه وسلم : أنَّهُ أتَى رَسُول اللهِ صلى الله عليه وسلم ، لِيُؤْذِنَه بِصَلاةِ الغَدَاةِ ، فَشَغَلَتْ عَائِشَةُ بِلالاً بِأَمْرٍ سَأَلَتْهُ عَنْهُ ، حَتَّى أصْبَحَ جِدّاً، فَقَامَ بِلالٌ فَآذَنَهُ بِالصَّلاَةِ، وَتَابَعَ أذَانَهُ ، فَلَمْ يَخْرُجْ رَسُولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم ، فَلَمَّا خَرَجَ صَلَّى بِالنَّاسِ ، فَأخْبَرَهُ أنَّ عَائِشَةَ شَغَلَتْهُ بِأمْرٍ سَأَلَتْهُ عَنْهُ حَتَّى أصْبَحَ جِدّاً ، وَأنَّهُ أبْطَأَ عَلَيْهِ بِالخُرُوجِ ، فَقَالَ - يَعْنِي النَّبيَّ صلى الله عليه وسلم - : (( إنِّي كُنْتُ رَكَعْتُ رَكْعْتَي الفَجْرِ )) فقالَ : يَا رَسُولَ اللهِ ، إنَّكَ أصْبَحْتَ جِدّاً ؟ فقَالَ : (( لَوْ أصْبَحْتُ أكْثَرَ مِمَّا أصْبَحْتُ ، لَرَكَعْتُهُمَا ، وَأحْسَنْتُهُمَا وَأجْمَلْتُهُمَا )) رواه أبُو دَاوُدَ بإسناد حسن .

Abu 'Abdillaah Bilaal bin Rabaah (Radhwiya Allaahu 'anhu), amesema kuwa siku moja muadhini wa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikwenda kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ili kumfahamisha kuwa Swalaah ya Asubuhi imefika lakini 'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa), alimshughulisha Bilaal kwa jambo alilomuuliza mpaka ikawa asubuhi sana. Ulipoanza kutoka mwangaza Bilaal aliinuka na kumjulisha Rasuli wa Allaah kuwa jamaa iko tayari na kumkumbusha lakini Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) hakutoka. Alipotoka aliwaswalisha watu. Kisha Bilaal alimuuliza ilikuwaje mpaka akashughulishwa na swali kutoka kwa 'Aaishah jambo ambalo lilimfanya kuchelewa kumuarifu kuhusu kufika kwa wakati Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) mpaka kukawa asubuhi sana pamoja na kutokea kwa mwangaza, naye (Nabiy Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akachukua muda kutoka nje (ya chumba chake). Akasema (yaani) Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) : "Hakika nilikuwa nikiswali Rak'ah mbili za Alfajiri." Akasema: "Ee Rasuli wa Allaah! Hakika umepambazukiwa sana." Akasema: "Lau kungepambazuka zaidi ya hivi ningeswali Rak'ah hizo mbili vyema na vizuri zaidi." [Abuu Daawuwd kwa Isnaad iliyo Hasan]

 

 

Share