18-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Kufanya Nyepesi Rak'ah Mbili za Alfajiri na Kubainisha Kinachosomwa na Wakati Wake

 

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

 

باب تخفيف ركعتي الفجر

وبيان مَا يقرأ فيهما وبيان وقتهما

18-Mlango Wa Kufanya Nyepesi Rak'ah Mbili za Alfajiri na Kubainisha Kinachosomwa na Wakati Wake

 

Alhidaaya.com

 

 

Hadiyth – 1

عن عائشة رَضِيَ اللهُ عَنها : أنَّ رسولَ الله صلى الله عليه وسلم كَانَ يُصَلّي رَكْعَتَيْنِ خَفِيفَتَيْنِ بَيْنَ النِّدَاءِ وَالإقَامَةِ مِنْ صَلاَةِ الصُّبْحِ . متفقٌ عَلَيهِ .

وفي روايَةٍ لَهُمَا : يُصَلِّي رَكْعَتَي الفَجْرِ ، فَيُخَفِّفُهُمَا حَتَّى أقُولَ : هَلْ قَرَأَ فِيهما بِأُمِّ القُرْآنِ .

وفي رواية لمسلم : كَانَ يُصلِّي رَكْعَتَي الفَجْرِ إذَا سَمِعَ الأذَانَ وَيُخَفِّفُهُمَا .

وفي رواية : إذَا طَلَعَ الفَجْرُ .

Kutoka kwa 'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) amesema: "Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa anaswali Rak'ah mbili nyepesi kati ya adhana na Iqamah ya Swallaah ya Asubuhi." [Al-Bukhaariy, Muslim, Abu Daawuwd na An-Nasaai]

Na katika riwaayah nyingine: "Alikuwa akiswali Rakaa mbili za Alfajiri anaposikia adhana kwa kuzifanya nyepesi mpaka nikawa ninasema: "Je, amesoma katika hizo Rak'ah mbili Suwratil Faatihah." 

Katika riwaayah ya Muslim: "Alikuwa akiswali Rakaa mbili za Alfajiri anaposikia adhana na kuzifanya nyepesi."

Na katika riwaayah nyingine: "Alfajiri inapochomoza."

 

Hadiyth – 2

وعن حفصة رَضِيَ اللهُ عَنها : أنَّ رَسُولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم كَانَ إذَا أذَّنَ المُؤَذِّنُ لِلْصُّبْحِ وَبَدَا الصُّبْحُ ، صَلَّى رَكْعَتَيْنِ خَفِيفَتَيْنِ . متفقٌ عَلَيهِ .

وفي رواية لمسلم : كَانَ رَسُول اللهِ صلى الله عليه وسلم ، إذَا طَلَعَ الفَجْرُ لا يُصَلِّي إلاَّ رَكْعَتَيْنِ خَفِيفَتَيْنِ .

Imepokewa kutoka kwake Hafswah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa wakati muadhini anapokuwa tayari ameadhini adhana ya Swalaah ya Asubuhi, na Asubuhi ikabainika, Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akiswali Rak'ah mbili nyepesi kabla Swalaah haijaqimiwa." [Al-Bukhaariy, Muslim na An-Nasaai]

Na katika riwaayah ya Muslim: "Rasuli wa Allaah Alikuwa unapotokea mwangaza akiswali Rak'ah mbili za Sunnah nyepesi wala haswali nyingine." 

 

Hadiyth – 3

وعن ابن عمر رَضِيَ اللهُ عَنهُما ، قَالَ : كَانَ رسول الله صلى الله عليه وسلم يُصَلِّي مِنَ اللَّيْلِ مَثْنَى مَثْنَى ، وَيُوتِرُ بِرَكْعَةٍ مِنْ آخِرِ اللَّيْلِ ، وَيُصَلِّي الرَّكْعَتَيْنِ قَبْلَ صلاةِ الغَدَاةِ ، وَكَأنَّ الأَذَانَ بِأُذُنَيْهِ . متفقٌ عَلَيهِ .

Ibn 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akiswali Swalaah za usiku Rakaa mbili mbili na Rak'ah moja ya witri mwisho wa usiku. Na alikuwa akiswali Rakaa mbili kabla ya Swalaah ya Asubuhi na kama kwamba Iqamah iko katika masikio yake (kwa ukaribu wa Swalaah yake na Iqamah). [Al-Bukhaariy, Muslim na An-Nasaai].

 

Hadiyth – 4

وعن ابن عباسٍ رضي الله عنهما : أنَّ رَسُولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم كَانَ يَقْرَأُ في رَكْعَتَي الفَجْرِ في الأُولَى مِنْهُمَا : [ قُولُوا آمَنَّا بِاللهِ وَمَا أُنْزِلَ إِلَيْنَا ] الآية الَّتي في البقرة ، وفي الآخِرَةِ مِنْهُمَا : [ آمَنَّا بِاللهِ وَاشْهَدْ بِأنَّا مُسْلِمُونَ ] .

وفي رواية : وفي الآخِرَةِ الَّتي في آل عِمْران : [ تَعَالَوْا إلَى كَلِمَةٍ سَوَاءٍ بَيْنَنَا وَبَيْنَكُمْ ] رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwa Ibn 'Abbaas (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akisoma katika Rak'ah mbili za Alfajiri, ya kwanza: "Semeni: Tumemwamini Allaah na yaliyoteremshwa kwetu" [Al-Baqarah: 136], na katika ya mwisho (yaani Rak'ah): "Tumemwamini Allaah, na shuhudia kwamba sisi ni Waislamu (wenye kujisalimisha Kwake). [Aal-'Imraan: 52]. 

Na katika riwaayah ya Muslim: "Katika Rak'ah ya mwisho alikuwa akisoma aya ambayo iko katika Aal-'Imraan: 'Njooni katika neno lililo sawa baina yetu na baina yenu,'" [Muslim].

 

Hadiyth – 5

وعن أبي هريرة رضي الله عنه : أنَّ رَسُولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم قرأ في رَكْعَتَي الفَجْرِ: [ قُلْ يَا أَيُّهَا الكَافِرُونَ ] وَ[ قُلْ هُوَ اللهُ أَحَدٌ ] رَوَاهُ مُسلِمٌ .

Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alisoma katika Rak'ah mbili za Sunnah ya Alfajiri: "Sema: Enyi makafiri!" [Al-Kaafiruwn] na "Sema: Yeye Allaah Ni Mmoja Pekee. [Al-Ikhlaasw]." [Muslim]

 

Hadiyth – 6

وعن ابن عمر رضي الله عنهما ، قَالَ : رَمَقْتُ النَّبيَّ صلى الله عليه وسلم ، شَهْراً فَكَانَ يَقْرَأُ في الرَّكْعَتَيْنِ قَبْلَ الفَجْرِ : [ قُلْ يَا أيُّهَا الْكَافِرُونَ ] وَ[ قُلْ هُوَ اللهُ أَحَدٌ ] رَوَاهُ التِّرمِذِيُّ ، وَقَالَ : (( حَدِيثٌ حَسَنٌ )) .

Na Ibn 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) amesema: Nilimchunguza Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) mwezi mzima alikuwa anasoma katika Rak'ah mbili kabla ya Alfajiri: "Sema: Enyi makafiri!" [Al-Kaafiruwn] na "Sema: Yeye Allaah Ni Mmoja Pekee. [Al-Ikhlaasw]." [At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan]

 

 

Share