19-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Kupendeza Kujilaza Baada ya Rak'ah Mbili za Alfajiri kwa Ubavu Wake wa Kulia na Kuhimizwa Sawa Ikiwa ni Tahajjud Au La

 

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

 

باب استحباب الاضطجاع بعد ركعتي الفجرعَلَى جنبه الأيمن والحث عليه

سواءٌ كَانَ تَهَجَّدَ بِاللَّيْلِ أمْ لا

19-Mlango Wa Kupendeza Kujilaza Baada ya Rak'ah Mbili za Alfajiri kwa Ubavu Wake wa Kulia na Kuhimizwa Sawa Ikiwa ni Tahajjud Au La

 

Alhidaaya.com

 

Hadiyth – 1

عن عائشة رَضِيَ اللهُ عَنها ، قالت : كَانَ النبيُّ صلى الله عليه وسلم إذَا صَلَّى ركعتي الفجر ، اضْطَجَعَ عَلَى شِقِّهِ الأَيْمَن . رَوَاهُ البُخَارِي .

'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) amesema: Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa anapomaliza kuswali Rakaa mbili za Alfajiri akijilaza kwa ubavu wake wa kulia." [Al-Bukhaariy]

 

Hadiyth – 2

وعن عائشة رَضِيَ اللهُ عَنها ، قالت : كَانَ النَّبيُّ صلى الله عليه وسلم يُصَلِّي فِيمَا بَيْنَ أنْ يَفْرُغَ مِنْ صَلاَةِ العِشَاءِ إلَى الفَجْرِ إحْدَى عَشرَةَ رَكْعَةً ، يُسَلِّمُ بَيْنَ كُلِّ رَكْعَتَيْنِ ، وَيُوتِرُ بِوَاحِدَةٍ ، فَإذَا سَكَتَ المُؤَذِّنُ مِنْ صَلاَةِ الفَجْرِ ، وَتَبَيَّنَ لَهُ الفَجْرُ ، وَجَاءهُ المُؤَذِّنُ ، قَامَ فَرَكَعَ رَكْعَتَيْنِ خَفِيفَتَينِ ، ثُمَّ اضْطَجَعَ عَلَى شِقِّهِ الأَيْمَنِ ، هكَذَا حَتَّى يأْتِيَهُ المُؤَذِّنُ لِلإِقَامَةِ . رَوَاهُ مُسلِم .

Amesema 'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa): Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akiswali Rakaa kumi na moja baina ya Swalaah ya Isha na Swalaah ya Alfajiri akitoa salamu baada ya kila Rakaa mbili, na anaswali rakaa moja witri. Muadhini anapomaliza kuadhini adhana ya Swalaah ya Alfajiri, na mwangaza kutokeza, muadhini anakuja. Anasimama kuswali Rakaa mbili hafifu, kisha akijilaza kwa ubavu wake wa kulia, hivi hadi muadhini anapomjia kukimu." [Muslim]

 

Hadiyth – 3

وعن أبي هريرة رَضِيَ اللهُ عَنه ، قَالَ : قال رَسُول اللَّهِ صلى الله عليه وسلم : (( إذا صَلَّى أحَدُكُمْ رَكْعَتَي الفَجْرِ ، فَلْيَضْطَجِعْ عَلَى يَمِينِهِ )) رواه أبُو دَاوُدَ وَالتِّرمِذِيُّ بأسانيد صحيحة ، قال الترمذي : (( حديث حسن صحيح )) .

Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Anaposwali mmoja wenu Rak'ah mbili za Sunnah ya Alfajiri ajilaze kwa ubavu wake wa kulia." [Abu Daawuwd na At-Tirmidhiy kwa Isnaad zilizo Swahiyh. Na akasema At-Tirmidhiy kuwa hii ni Hadiyth Hasan Swahiyh].

 

 

Share