20-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Sunnah ya Adhuhuri

 

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

 

باب سنة الظهر

20-Mlango Wa Sunnah ya Adhuhuri

 

Alhidaaya.com

 

Hadiyth – 1

عن ابن عمر رَضِيَ اللهُ عَنهُما ، قَالَ : صَلَّيْتُ مَعَ رَسُولِ اللهِ صلى الله عليه وسلم رَكْعَتَيْنِ قَبْلَ الظُّهْرِ وَرَكْعَتَيْنِ بَعْدَهَا . متفقٌ عَلَيهِ .

Amesema Ibn 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhumaa): Niliswali pamoja na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) Rak'ah mbili kabla ya Swalaah ya Adhuhuri na Rak'ah mbili baada yake." [Al-Bukhaariy, Muslim na At-Tirmidhiy]

 

Hadiyth – 2

وعن عائشة رَضِيَ اللهُ عَنها : أنَّ النَّبيَّ صلى الله عليه وسلم كَانَ لا يَدَعُ أرْبَعاً قَبْلَ الظُّهْرِ . رَوَاهُ البُخَارِيُّ .

'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) amesema: Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa haachi rakaa nne kabla ya Adhuhuri." [Al-Bukhaariy]

 

Hadiyth – 3

وعن عائشة رَضِيَ اللهُ عَنها ، قالت : كَانَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم يُصَلِّي في بَيْتِي قَبْلَ الظُّهْرِ أرْبَعاً ، ثُمَّ يَخْرُجُ ، فَيُصَلِّي بِالنَّاسِ ، ثُمَّ يَدْخُلُ فَيُصَلِّي رَكْعَتَيْنِ . وَكَانَ يُصَلِّي بِالنَّاسِ المَغْرِبَ ، ثُمَّ يَدْخُلُ فَيُصَلِّي رَكْعَتَيْنِ ، وَيُصَلِّي بِالنَّاسِ العِشَاءِ ، وَيَدْخُلُ بَيتِي فَيُصَلِّي رَكْعَتَيْنِ . رَوَاهُ مُسلِم .

'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) amesema: Alikuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akiswali nyumbani kwangu Rak'ah nne kabla ya Adhuhuri, kisha anatoka kuwaswalisha watu kisha anarudi na kuswali Rak'ah mbili. Na alikuwa akiwaswalisha watu Swalaah ya Magharib, kisha anaingia (nyumbani kwangu) na kuswali Rakaa mbili. Na alikuwa anawaswalisha watu Swalaah ya Ishaa na anaingia nyumbani kwangu na kuswali Rakaa mbili." [Muslim]

 

Hadiyth – 4

وعن أُمّ حَبِيبَةَ رَضِيَ اللهُ عَنها ، قالت : قال رَسُولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم : (( مَنْ حَافَظَ عَلَى أرْبَعِ رَكَعَاتٍ قَبْلَ الظُّهْرِ ، وَأرْبَعٍ بَعْدَهَا ، حَرَّمَهُ اللَّهُ عَلَى النَّارِ )) رواه أبُو دَاوُدَ وَالتِّرمِذِيُّ ، وَقَالَ : (( حَدِيثٌ حَسَنٌ صحيح )) .

Imepokewa kutoka kwa Ummu Habibah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mwenye kuzihifadhi (kuzichunga kwa kuswali) Rak'ah nne kabla ya Adhuhuri na nne baada yake, Allaah atamharamisha Moto." [Abu Daawuwd na At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan Swahiyh]

 

Hadiyth – 5

وعن عبد الله بن السائب رَضِيَ اللهُ عَنه : أنَّ رَسُولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم كَانَ يُصَلِّي أرْبَعاً بَعْدَ أنْ تَزُولَ الشَّمْسُ قَبْلَ الظُّهْرِ ، وقَالَ : (( إنَّهَا سَاعَةٌ تُفْتَحُ فِيها أبْوَابُ السَّمَاءِ ، فَأُحِبُّ أنْ يَصْعَدَ لِي فيهَا عَمَلٌ صَالِحٌ )) رواه التِّرمِذِيُّ، وَقَالَ: (( حَدِيثٌ حَسَنٌ )) .

Imepokewa kutoka kwa 'Abdillaah bin As-Saa'ib (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akiswali Rak'ah nne baada ya jua kuzama na kabla ya Adhuhuri na akasema: "Hakika huo ni wakati ambao milango ya mbinguni hufunguliwa, hivyo napenda amali yangu njema iwe inapanda (mbinguni) wakati huo." [At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan]

 

Hadiyth – 6

وعن عائشة رَضِيَ اللهُ عَنها : أنَّ النَّبيَّ صلى الله عليه وسلم كَانَ إذا لَمْ يُصَلِّ أربَعاً قَبلَ الظُّهْرِ ، صَلاَّهُنَّ بَعْدَهَا . رَوَاهُ التِّرمِذِيُّ ، وَقَالَ : (( حَدِيثٌ حَسَنٌ )) .

Imepokewa kutoka kwa 'Aaishah(Radhwiya Allaahu 'anhaa) kuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) anapokosa kuswali Rak'ah nne kabla ya Adhuhuri ya alikuwa akiswali baada yake (yaani baada ya Swalaah ya Adhuhuri) ." [At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan]

 

 

Share