25-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Kupendeza Kuswali Sunnah Nyumbani Sawa ni Zile Zilizohimizwa au Nyinginezo na Maagizo ya Kubadilisha Sehemu Uliyoswali Swalaah ya Faradhi au Kupambanua Baina yao kwa Mazungumzo

 

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

 

 

باب استحباب جعل النوافل في البيت

سواء الراتبة وغيرها والأمر بالتحول للنافلة من موضع

الفريضة أَو الفصل بينهما بكلام

25-Mlango Wa Kupendeza Kuswali Sunnah Nyumbani Sawa ni Zile Zilizohimizwa au Nyinginezo na Maagizo ya Kubadilisha Sehemu Uliyoswali Swalaah ya Faradhi au Kupambanua Baina yao kwa Mazungumzo

 

Alhidaaya.com

 

Hadiyth – 1

عن زيد بن ثابت رَضِيَ اللهُ عَنهُ : أنَّ النَّبيَّ صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( صَلُّوا أَيُّهَا النَّاسُ فِي بُيُوتِكُمْ ، فَإنَّ أفْضَلَ الصَّلاَةِ صَلاَةُ المَرْءِ في بَيْتِهِ إِلاَّ المَكْتُوبَةَ )) متفقٌ عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwa Zayd bin Thaabit (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Enyi watu swalini majumbani mwenu. Hakika Swalaah bora ni ile mtu anayoswali nyumbani kwake isipokuwa Swalaah za faradhi (ndio anayowajibika kuswali Msikitini)." [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

Hadiyth – 2

وعن ابن عمر رضي الله عنهما ، عن النَّبيِّ صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( اجْعَلُوا مِنْ صَلاَتِكُمْ فِي بُيُوتِكُمْ ، وَلاَ تَتَّخِذُوهَا قُبُوراً )) متفقٌ عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwa Ibn 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Swalini Swalaah zenu majumbani na wala msifanye nyumba zenu kuwa kama makaburi." [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

Hadiyth – 3

وعن جابر رَضِيَ اللهُ عَنهُ ، قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( إِذَا قَضَى أحَدُكُمْ صَلاَتَهُ في مَسْجِدِهِ فَلْيَجْعَلْ لِبَيْتِهِ نَصِيباً مِنْ صَلاَتِهِ ؛ فَإنَّ اللهَ جَاعِلٌ في بَيْتِهِ مِنْ صَلاَتِهِ خَيْراً )) رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwa Jaabir (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Anapomaliza mmoja wenu Swalaah yake ya faradhi katika Msikiti, ajaalie nyumbani kwake sehemu ya Swalaah zake (za Sunnah), kwani Allaah atampatia kheri kwenye nyumba kwa sababu hiyo." [Muslim]

 

Hadiyth – 4

وعن عمر بن عطاءٍ : أنَّ نَافِعَ بْنَ جُبَيْرٍ أرْسَلَهُ إِلَى السَّائِبِ ابن أُخْتِ نَمِرٍ يَسأَلُهُ عَنْ شَيْءٍ رَآهُ مِنْهُ مُعَاوِيَةُ في الصَّلاَةِ ، فَقَالَ : نَعَمْ ، صَلَّيْتُ مَعَهُ الجُمُعَةَ في المَقْصُورَةِ ، فَلَمَّا سَلَّمَ الإمَامُ ، قُمْتُ في مَقَامِي ، فَصَلَّيْتُ ، فَلَمَّا دَخَلَ أَرْسَلَ إلَيَّ ، فَقَالَ: لاَ تَعُدْ لِمَا فَعَلْتَ. إِذَا صَلَّيْتَ الجُمُعَةَ فَلاَ تَصِلْهَا بِصَلاةٍ حَتَّى تَتَكَلَّمَ أَوْ تَخْرُجَ ؛ فَإنَّ رسولَ الله صلى الله عليه وسلم أمَرَنَا بِذلِكَ ، أن لاَ نُوصِلَ صَلاَةً بِصَلاَةٍ حَتَّى نَتَكَلَّمَ أَوْ نَخْرُجَ . رواه مسلم .

'Umar bin 'Atwaa' Amesema: Naafi' bin Jubayr alimtuma kwa Saa'ib mtoto wa dada wa Namir alichoona kwake katika Swalaah. Akasema: "Ndio niliswali pamoja nye Ijumaa katika sehemu ya Msikiti iliyofungwa. Alipotoa salamu imamu nilisimama katika sehemu niliyoswali, (Sunnah). Alipotoka Msikitini alinitumia mtu, akasema: 'Usirudie tena ulichofanya, unaposwali Ijumaa, usiswali Swalaah nyingine mpaka uzungumze au utoke. Kwani Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ametuamuru hilo, tusiunganishe Swalaah kwa Swalaah mpaka tuzungumze au tutoke." [Muslim]

 

 

 

Share