26-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Kuhimiza Kuswali Witri na Kubainisha Kuwa Hiyo ni Sunnah Muakkadah na Kubainisha Wakati Wake

 

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

 

باب الحث عَلَى صلاة الوتر وبيان أنه سنة مؤكدة وبيان وقته

26-Mlango Wa Kuhimiza Kuswali Witri na Kubainisha Kuwa Hiyo ni Sunnah Muakkadah na Kubainisha Wakati Wake

 

Alhidaaya.com

 

Hadiyth – 1

عن عليٍّ رَضِيَ اللهُ عَنهُ ، قَالَ : الوِتْرُ لَيْسَ بِحَتْمٍ كَصَلاَةِ المَكْتُوبَةِ ، وَلَكِنْ سَنَّ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( إنَّ اللهَ وِتْرٌ يُحِبُّ الوِتْرَ ، فَأَوْتِرُوا يَا أهْلَ القُرْآنِ )) رواه أَبُو داود والترمذي ، وقال : (( حديث حسن )) .

'Ali (Radhwiya Allaahu 'anhu) Amesema: Witri si lazima kama ilivyo Swalaah ya faradhi lakini Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliiweka Sunnah hii, kwa kusema: "Hakika Allaah ni Witri (yaani mmoja pekee), na Anapenda Witri, basi Swalini Witri enyi watu wa Qur-aan." [Abu Daawuwd na At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan]

 

Hadiyth – 2

وعن عائشة رضي الله عنها ، قالت : مِنْ كُلِّ اللَّيْلِ قَدْ أَوْتَرَ رسول الله صلى الله عليه وسلم ، مِنْ أَوَّلِ اللَّيْلِ، وَمِنْ أوْسَطِهِ، وَمِنْ آخِرِهِ، وَانْتَهَى وِتْرُهُ إِلَى السَّحَرِ . متفقٌ عَلَيْهِ .

'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akiswali witri muda wote wa usiku: mwanzo wake, katika ya usiku na mwisho wake ambapo witri yake alikuwa akiimaliza inapofika Alfajiri." [Al-Bukaariy, Muslim, Abu Daawuwd, At-Tirmidhiy na An-Nasaai]

 

Hadiyth – 3

وعن ابن عمر رضي الله عنهما ، عن النَّبيِّ صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( اجْعَلُوا آخِرَ صَلاَتِكُمْ بِاللَّيْلِ وِتْراً )) متفقٌ عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwa Ibn 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Ifanyeni Swalaah yenu ya mwisho katika usiku kuwa ni witri." [Al-Bukhaariy, Muslim, Abu Daawuwd na An-Nasaai]

 

Hadiyth – 4

وعن أَبي سعيد الخدري رَضِيَ اللهُ عَنهُ : أنَّ النَّبيَّ صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( أوْتِرُوا قَبْلَ أنْ تُصْبِحُوا )) رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwa Abu Sa'iyd Al-Khudriy (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Swalini witri kabla ya asubuhi." [Muslim]

 

Hadiyth – 5

وعن عائشة رضي الله عنها: أنَّ النَّبيَّ صلى الله عليه وسلم كَانَ يُصَلِّي صَلاَتَهُ باللَّيْلِ ، وَهِيَ مُعْتَرِضَةٌ بَيْنَ يَدَيْهِ ، فَإذَا بَقِيَ الوِتْرُ ، أيْقَظَهَا فَأوْتَرتْ . رواه مسلم .

وفي روايةٍ لَهُ : فَإذَا بَقِيَ الوِتْرُ ، قَالَ : (( قُومِي فَأوتِري يَا عائِشَةُ )) .

Imepokewa kutoka kwa 'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) kuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akiswali Swalaah zake za usiku akiwa yeye amelala mbele yake (karibu naye). Inapobakia witri alikuwa anamuamsha, nami naswali witri." [Muslim]

Na katika riwaayah yake: Inapobakia witri alisema: "Amka uswali witri, ee 'Aaishah."

 

Hadiyth – 6

وعن ابن عمرَ رضي الله عنهما : أنَّ النَّبيَّ صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( بَادِرُوا الصُّبْحَ بِالوِتْرِ )) رواه أَبُو داود والترمذي ، وقال : (( حديث حسن صحيح )) .

Imepokewa kutoka kwa Ibn 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Shindaneni kuswali witri asubuhi." [Abu Daawuwd na At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan Swahiyh]

 

Hadiyth – 7

وعن جابر رَضِيَ اللهُ عَنهُ ، قَالَ : قَالَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم : (( مَنْ خَافَ أنْ لاَ يَقُومَ مِنْ آخِرِ اللَّيْلِ ، فَلْيُوتِرْ أوَّلَهُ ، وَمَنْ طَمِعَ أنْ يَقُومَ آخِرَهُ فَلْيُوتِرْ آخِرَ اللَّيلِ ، فَإنَّ صَلاَةَ آخِرِ اللَّيْلِ مَشْهُودَةٌ ، وذَلِكَ أفْضَلُ )) رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwa Jaabir (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mwenye kuhofia kuwa hataamka mwisho wa usiku, aswali waitri mwanzoni. Na mwenye tamaa ya kuswali Swalaah ya usiku basi aswali mwisho, kwani Swalaah ya mwishoni mwa mwisho wa usiku inashuhudiwa (na Malaaika) na hiyo ni bora zaidi." [Muslim].

 

 

 

Share