27-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Ubora wa Swalaah ya Dhuwhaa na Kubainisha Uchache, Wingi, Wastani Wake na Kuhimizwa katika Kuihifadhi

 

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

 

باب فضل صلاة الضحى

وبيان أقلها وأكثرها وأوسطها ، والحث عَلَى المحافظة عَلَيْهَا

27-Mlango Wa Ubora wa Swalaah ya Dhuwhaa na Kubainisha Uchache, Wingi, Wastani Wake na Kuhimizwa katika Kuihifadhi

 

Alhidaaya.com

 

Hadiyth – 1

عن أَبي هريرة رضي اللهُ عنه ، قَالَ : أوْصَانِي خَلِيلي صلى الله عليه وسلم بِصِيَامِ ثَلاَثَةِ أيَّامٍ مِنْ كُلِّ شَهْرٍ ، وَرَكْعَتَي الضُّحَى ، وَأنْ أُوتِرَ قَبْلَ أنْ أرْقُدَ . متفقٌ عَلَيْهِ .

Amesema Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu): Mpenzi wangu Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ameniusia vitu vitatu, nisiviache mpaka ninakufa: "Kufunga siku tatu kila mwezi, kuswali Swalaah ya Dhuwhaa na kulala baada ya witri." [Al-Bukhaariy, Muslim, Abu Daawuwd, At-Tirmidhiy na An-Nasaai]. Witri kabla ya kulala inapendeza kwa yule mwenye shaka ya kuamka mwisho wa usiku. Akiwa ana imani kuwa ataamka basi kuiswali mwisho wa usiku ni bora.

 

 

Hadiyth – 2

وعن أَبي ذَرٍّ رضي اللهُ عنه ، عن النَّبيِّ صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( يُصْبحُ عَلَى كُلِّ سُلاَمَى مِنْ أَحَدكُمْ صَدَقَةٌ : فَكُلُّ تَسْبِيحَةٍ صَدَقَةٌ ، وَكُلُّ تَحْمِيدَةٍ صَدَقَةٌ ، وَكُلُّ تَهْلِيلَةٍ صَدَقَةٌ ، وَكُلُّ تَكْبِيرَةٍ صَدَقَةٌ ، وَأَمْرٌ بِالمَعْرُوفِ صَدَقَةٌ ، وَنَهْيٌ عَنِ المُنْكَرِ صَدَقَةٌ ، وَيُجْزِىء  مِنْ ذَلِكَ رَكْعَتَانِ يَرْكَعُهُمَا مِن الضُّحَى )) رواه مسلم .

Kutoka kwa Abu Dharr (Radhwiya Allaahu 'anhu) ya kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Kila kiungo cha mmoja wenu kinapambazukiwa kwa kufanya swadaqah (jambo jema). Hivyo kila tasbiyh (ni kusema Subhaana Allaah, yaani Allaah ameepukana na kila aina ya upungufu) ni swadaqah, na kila tahmiyd (ni kusema AlhamduliLLaah, yaani kila jinsi ya sifa njema ni za Allaah) ni swadaqah, na kila takbiyr (ni kusema Allaahu Akbar, yaani Allaah ni Mkubwa kuliko wote) ni swadaqah na kuamrisha mema ni swadaqah na kukataza mabaya ni swadaqah. Na rakaa mbili za Swalaah ya Dhuwhaa unazoswali zatosheleza (kama swadaqah ya yote haya)." [Muslim]

 

Hadiyth – 3

وعن عائشة رضي الله عنها ، قالت : كَانَ رسولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم يُصَلِّي الضُّحَى أرْبَعاً ، وَيَزِيدُ مَا شَاءَ الله . رواه مسلم .

'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akiswali Rak'ah nne za Dhuwhaa na akizidisha kama anavyopenda Allaah." [Muslim]

 

Hadiyth – 4

وعن أُمِّ هَانِىءٍ فاختة بنت أَبي طالب رضي الله عنها ، قالت : ذَهَبْتُ إِلَى رَسولِ اللهِ صلى الله عليه وسلم ، عَامَ الفَتْحِ فَوَجَدْتُهُ يَغْتَسِلُ ، فَلَمَّا فَرَغَ مِنْ غُسْلِهِ ، صَلَّى ثَمَانِيَ رَكَعَاتٍ، وَذَلِكَ ضُحىً. متفقٌ عَلَيْهِ . وهذا مختصرُ لفظِ إحدى روايات مسلم.

Kutoka kwa Ummu Haani bint Abu Twaalib (Radhwiya Allaahu 'anhaa) amesema: Nilikwenda kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) mwaka wa Fathi (siku mji wa Makkah ulipotekwa) nikamkuta anakoga. Alipomaliza kukoga aliswali Rak'ah nane na hiyo ilikuwa ni Dhuwhaa." [Al-Bukhaariy, Muslim, Abu Daawuwd, At-Tirmidhiy na An-Nasaai]

 
 
 

 

 
 
 
Share