35-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Fadhila za Kisimamo cha Usiku wa Qadr (Cheo Kitukufu) na Kubainisha Usiku Unaotarajiwa

 

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

 

باب فضل قيام ليلة القدر وبيان أرجى لياليها

35-Mlango Wa Fadhila za Kisimamo cha Usiku wa Qadr (Cheo Kitukufu) na Kubainisha Usiku Unaotarajiwa

 

Alhidaaya.com

 

قال الله تَعَالَى :

إِنَّا أَنزَلْنَاهُ فِي لَيْلَةِ الْقَدْرِ ﴿١﴾

Hakika Sisi Tumeiteremsha Qur-aan katika Laylatul-Qadr (Usiku wa Qadr). 

وَمَا أَدْرَاكَ مَا لَيْلَةُ الْقَدْرِ ﴿٢﴾

Na nini kitakachokujulisha ni nini Laylatul-Qadr?

لَيْلَةُ الْقَدْرِ خَيْرٌ مِّنْ أَلْفِ شَهْرٍ ﴿٣﴾

Laylatul-Qadr ni mbora kuliko miezi elfu.

تَنَزَّلُ الْمَلَائِكَةُ وَالرُّوحُ فِيهَا بِإِذْنِ رَبِّهِم مِّن كُلِّ أَمْرٍ ﴿٤﴾

Wanateremka humo Malaika pamoja na Ar-Ruwh (Jibriyl) kwa Idhini ya Rabb wao kwa kila jambo.

سَلَامٌ هِيَ حَتَّىٰ مَطْلَعِ الْفَجْرِ ﴿٥﴾

Usiku huo ni amani mpaka kuchomoza Alfajiri. [Al-Qadr: 1-5]

 

إِنَّا أَنزَلْنَاهُ فِي لَيْلَةٍ مُّبَارَكَةٍ ۚ ﴿٣﴾

Hakika Sisi Tumekiteremsha katika usiku uliobarikiwa. [Ad-Dukhaan: 3]

 

 

Hadiyth – 1

وعن أَبي هريرة رضي اللهُ عنه ، عن النبيِّ صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( مَنْ قَامَ لَيْلَةَ القَدْرِ إيمَاناً وَاحْتِسَاباً غُفِرَ لَهُ مَا تَقَدَّمَ مِنْ ذَنْبِهِ )) متفقٌ عَلَيْهِ .

Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: "Mwenye kusimama Laylatul Qadr kwa Imaani, na kutarajia thawabu huyo husamehewa madhambi yakeyaliyotangulia." [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

Hadiyth – 2

وعن ابن عمر رضي الله عنهما : أنَّ رِجالاً مِنْ أصْحَابِ النبيِّ صلى الله عليه وسلم أُرُوا لَيْلَةَ القَدْرِ في المَنَامِ في السَّبْعِ الأَوَاخِرِ ، فَقَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( أرَى رُؤْيَاكُمْ قَدْ تَوَاطَأتْ في السَّبْعِ الأوَاخِرِ ، فَمَنْ كَانَ مُتَحَرِّيهَا فَلْيَتَحَرَّهَا في السَّبْعِ الأَوَاخِرِ )) متفقٌ عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwa Ibn 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kuwa watu fulani miongoni mwa Swahaaba wa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) walionyeshawa Laylatul Qadr ndotoni katika siku saba za mwisho. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: "Naona ndoto zenu zimeangukia siku saba za mwisho basi mwenye kutafuta na atafute katika siku saba za mwishao." [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

Hadiyth – 3

وعن عائشة رضي الله عنها ، قالت : كَانَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم يُجَاوِرُ في العَشْرِ الأَوَاخِرِ مِنْ رَمَضَانَ ، ويقول : (( تَحرَّوا لَيْلَةَ القَدْرِ في العَشْرِ الأواخرِ منْ رَمَضانَ ))متفقٌ عَلَيْهِ .

'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa anakaa itikafu katika kumi la mwisho la Ramadhwaan na anasema: "Itafuteni Laylatul Qadr katika kumi la mwisho la Ramadhwaan." [Al-Bukhaariy na Muslim].

 

Hadiyth – 4

وعن عائشة رضي الله عنها : أنَّ رسولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( تَحَرَّوْا لَيْلَةَ القَدْرِ في الوَتْرِ مِنَ العَشْرِ الأوَاخِرِ مِنْ رَمَضَانَ )) رواه البخاري .

Imepokewa kutoka kwa 'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Itafuteni Laylatul Qadr katika siku za witr (yaani usiku wa tarehe 21, au 23, au 27, au 29) katika kumi la mwisho la Ramadhwaan." [Al-Bukhaariy]

 

Hadiyth – 5

وعن عائشة ، رضي الله عنها ، قالت : كَانَ رسول الله صلى الله عليه وسلم إِذَا دَخَلَ العَشْرُ الأَوَاخِرُ مِنْ رَمَضَانَ ، أحْيَا اللَّيْلَ ، وَأيْقَظَ أهْلَهُ ، وَجَدَّ وَشَدَّ المِئزَرَ . متفقٌ عَلَيْهِ .

Amesema 'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) : Zilipokuwa zinaanza siku kumi za mwisho katika mwezi wa Ramadhwaan Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa anaswali usiku kucha na akiwaamsha familia yake na anajipinda na kukaza mkanda wake." [Al-Bukhaariy na Muslim].

 

Hadiyth – 6

وعن عائشة ، رضي الله عنها ، قالت : كَانَ رسولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم يَجْتَهِدُ في رَمَضَانَ مَا لاَ يَجْتَهِدُ في غَيْرِهِ ، وَفِي العَشْرِ الأوَاخِرِ مِنْهُ مَا لا يَجْتَهِدُ في غَيْرِهِ . رواه مسلم .

Amesema 'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa): Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) Alikuwa akijitahidi (kwa kufanya 'Ibadah) katika mwezi wa Ramadhwaan zaidi kuliko miezi mingine. Na katika mwezi huo alikuwa anajitahidi zaidi katika kuni la mwisho kuliko siku nyinginezo katika mwezi huo." [Muslim]

 

Hadiyth – 7

وعن عائشة ، رضي الله عنها ، قالت : قُلْتُ : يَا رسول الله ، أرَأيْتَ إنْ عَلِمْتُ أيُّ لَيلَةٍ لَيْلَةُ القَدْرِ مَا أقُولُ فِيهَا ؟ قَالَ : (( قُولِي : اللَّهُمَّ إنَّكَ عَفُوٌ تُحِبُّ العَفْوَ فَاعْفُ عَنّي )) رواه الترمذي ، وقال : (( حديث حسن صحيح )) .

'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) amesema: Nilimuuliza: "Ee Rasuli wa Allaah! Waonaje nikiweza kuujua usiku wa Laylatul Qadr, niseme nini ndani yake?" Akasema: "Sema: Allaahumma Innaka 'Afuwwun Tuhibbul 'Afwa Fa'fu'anniy - Ee Mola wangu! Hakika Wewe ni Mwingi wa kusamehe na Unapenda kusamehe, hivyo nismehe." [At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan Swahiyh]

 

 

Share