43-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Fadhila za Kufuturu Mapema na Unachofuturia Nacho na Anachosema Mfungaji Baada ya Iftari

 

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

 

باب فضل تعجيل الفطر

وَمَا يفطر عَلَيْهِ ، وَمَا يقوله بعد الإفطار

43-Mlango Wa Fadhila za Kufuturu Mapema na Unachofuturia Nacho na Anachosema Mfungaji Baada ya Iftari

 

Alhidaaya.com

 

Hadiyth – 1

عن سهل بن سعد رضي الله عنه : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( لاَ يَزَالُ النَّاسُ بِخَيْرٍ مَا عَجَّلُوا الفِطْرَ )) متفقٌ عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwa Sahl bin sa'ad (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Watu wataendelea kuwa katika kheri muda wa kuwa wanaharakisha kufuturu." [Al-Bukhaariy, Muslim, Maalik na At-Tirmidhiy]

 

Hadiyth – 2

وعن أَبي عطِيَّة ، قَالَ : دَخَلْتُ أنَا وَمَسْرُوقٌ عَلَى عائشة رضي الله عنها ، فَقَالَ لَهَا مَسْرُوق : رَجُلاَنِ مِنْ أصْحَابِ محَمَّدٍ صلى الله عليه وسلم ، كِلاَهُمَا لا يَألُو عَنِ الخَيْرِ ؛ أحَدُهُمَا يُعَجِّلُ المَغْرِبَ وَالإفْطَارَ ، وَالآخَرُ يُؤَخِّرُ المَغْرِبَ وَالإفْطَارَ ؟ فَقَالَتْ : مَنْ يُعَجِّلُ المَغْرِبَ وَالإفْطَارَ ؟ قَالَ : عَبْدُ اللهِ - يعني : ابن مسعود - فَقَالَتْ : هكَذَا كَانَ رسولُ اللهِ يَصْنَعُ . رواه مسلم .

Amesema Abu 'Atiyyah: Tulikwenda mimi na Masruwq kwa 'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) Masruwq akamuuliza: "Watu wawili miongoni mwa Swahaaba wa Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), wote hawana kasoro katika kutenda mambo ya kheri. Mmoja wao anafanya haraka kuswali Maghrib na kufuturu na mwingine anachelewesha Maghrib na kufuturu?" Akauliza: "Ni nani anaye fanya haraka kuswali Maghrib na kufuturu?" Akajibu: " 'Abdullaah - yaani Ibn Mas'uwd." Akasema: "Hivyo ndivyo alivyokuwa akufanya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)." [Muslim]

 

Hadiyth – 3

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم : (( قَالَ اللهُ عَزَّ وَجَلَّ : أحَبُّ عِبَادِي إلَيَّ أعْجَلُهُمْ فِطْراً )) رواه الترمذي ، وقال : (( حديث حسن )) .

Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Amesema Allaah 'Azza wa Jalla: Mja ninayempenda zaidi ni yule mwenye kuharakisha kufuturu." [At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan]

 

Hadiyth – 4

وعن عمر بن الخطاب رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم : (( إِذَا أقْبَلَ اللَّيْلُ مِنْ هاهُنَا ، وَأدْبَرَ النهارُ مِنْ هَاهُنَا ، وَغَرَبَتِ الشَّمْسُ ، فَقَدْ أفْطَر الصَّائِمُ )) متفقٌ عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwa 'Umar bin Al-Khatwaab (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Ukifika usiku kutokea hapa (yaani upande wa Mashariki) na mchana ukaondoka kutokea hapa (yaani upande wa Magharibi), na jua likazama mwenye kufunga amekwisha kufuturu." [Al-Bukhaariy, Muslim, Abu Daawuwd na At-Tirmidhiy] 

 

Hadiyth – 5

وعن أَبي إبراهيم عبدِ الله بنِ أَبي أوفى رضي الله عنهما ، قَالَ : سِرْنَا مَعَ رسولِ الله صلى الله عليه وسلم ، وَهُوَ صَائِمٌ ، فَلَمَّا غَرَبَتِ الشَّمْسُ ، قَالَ لِبَعْضِ القَوْمِ : (( يَا فُلاَنُ انْزِلْ فَاجْدَحْ لَنَا )) ، فَقَالَ : يَا رسول الله ، لَوْ أمْسَيْتَ ؟ قَالَ : (( انْزِلْ فَاجْدَحْ لَنَا )) قَالَ : إنَّ عَلَيْكَ نَهَاراً ، قَالَ : (( انْزِلْ فَاجْدَحْ لَنَا )) قَالَ : فَنَزَلَ فَجَدَحَ لَهُمْ فَشَرِبَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم ، ثُمَّ قَالَ : (( إِذَا رَأَيْتُمُ اللَّيْلَ قَدْ أقْبَلَ مِنْ هاهُنَا ، فَقَدْ أفْطَرَ الصَّائِمُ )) وَأشَارَ بِيَدِهِ قِبَلَ المَشْرِقِ . متفقٌ عَلَيْهِ .

Amesema Abu Ibraahiym 'Abdillaah bin Abi Awfaa (Radhwiya Allaahu 'anhumaa): Tulikuwa pamoja na Rasuli wa Allaah (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) katika safari, naye alikuwa amefunga, jua lilipozama aliwaambia baadhi ya watu: "Ee fulani! Terema utuchanganyie (sawiqa na maji)." Akasema: "Ee Rasuli wa Allaah! Lau kungekuchwa (yaani hakujaingia usiku)?" Akasema: "Teremka utuchanganyie." Akasema: "Hakika bado ni mchana." Akasema: "Teremka utuchanganyie." Akasema: "Akateremka akawachanganyia, akanywa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), kisha akasema: "Mkiona usiku umekuja kutokea hapa basi mwenye kufunga amekwisha kufuturu." Akaashiria kwa mkono wake upande wa Mashariki." [Al-Bukhaariy, Muslim na Abu Daawuwd].

 

Hadiyth – 6

وعن سلمان بن عامر الضَّبِّيِّ الصحابي رضي الله عنه ، عن النبيِّ صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( إِذَا أفْطَرَ أحَدُكُمْ ، فَلْيُفْطِرْ عَلَى تَمْرٍ ، فَإنْ لَمْ يَجِدْ ، فَلْيُفْطِرْ عَلَى مَاءٍ ؛ فإنَّهُ طَهُورٌ )) رواه أَبُو داود والترمذي ، وقال : (( حديث حسن صحيح )) .

Imepokewa kutoka kwa Salmaan bin 'Aamir Adh-Dhibbiy, ambaye ni Swahaaba (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Alllahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Anapofuturu mmoja wenu basi afuturu kwa tende. Ikiwa hakupata tende basi afuturu kwa maji kwani hayo ni tohara." [Abu Daawuwd na At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan Swahiyh]

 

Hadiyth – 7

وعن أنس رضي الله عنه ، قَالَ : كَانَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم يُفْطِرُ قَبْلَ أنْ يُصَلِّي عَلَى رُطَبَاتٍ ، فَإنْ لَمْ تَكُنْ رُطَبَاتٌ فَتُمَيْرَاتٌ ، فَإنْ لَمْ تَكُنْ تُمَيْرَاتٌ حَسَا حَسَوَاتٍ مِنْ مَاءٍ . رواه أَبُو داود والترمذي ، وقال : (( حديث حسن )) .

Amesema Anas (Radhwiya Allaahu 'anhu): Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) Alikuwa akifuturu kabla ya kuswali kwa tende zilizo komaa, zikikosekana anafuturia tende zilizo wiva na zikikosekana anachukua maji kidogo." [Abu Daawuwd na At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan].

 

Share