52-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Fadhila za Mwenye Kumfuturisha Aliye Funga na Fadhila za Mfungaji Ambaye Watu Wanakula Kwake na Duaa ya Mwalikwa kwa Mwalikaji

 

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

باب فضل من فطَّر صائماً وفضل الصائم

الذي يؤكل عنده ودعاء الآكل للمأكول عنده

52-Mlango Wa Fadhila za Mwenye Kumfuturisha Aliye Funga na Fadhila za Mfungaji Ambaye Watu Wanakula Kwake na Duaa ya Mwalikwa kwa Mwalikaji

 

Alhidaaya.com

 

Hadiyth – 1

عن زيد بن خالد الجُهَنِيِّ رضي اللهُ عنه ، عن النبي صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( مَنْ فَطَّرَ صَائِماً ، كَانَ لَهُ مِثْلُ أجْرِهِ ، غَيْرَ أنَّهُ لاَ يُنْقَصُ مِنْ أجْرِ الصَّائِمِ شَيْءٌ )) رواه الترمذي ، وقال : (( حديث حسن صحيح )) .

Zayd bin Khaalid Al-Juhaniyy amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mwenye kumfuturisha mfungaji anapata thawabu mfano wa thawabu zake bila mfungaji kupunguziwa chochote katika thawabu zake." [At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan Swahiyh]

 

Hadiyth – 2

وعن أُمِّ عُمَارَةَ الأنصارِيَّةِ رَضِيَ اللهُ عنها : أنَّ النبيَّ صلى الله عليه وسلم دَخَلَ عَلَيْهَا ، فَقَدَّمَتْ إِلَيْهِ طَعَاماً ، فَقَالَ : (( كُلِي )) فَقَالَتْ : إنِّي صَائِمَةٌ ، فَقَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( إنَّ الصَائِمَ تُصَلِّي عَلَيْهِ المَلاَئِكَةُ إِذَا أُكِلَ عِنْدَهُ حَتَّى يَفْرغُوا )) وَرُبَّمَا قَالَ : (( حَتَّى يَشْبَعُوا )) رواه الترمذي ، وقال : (( حديث حسن )) .

Imepokewa kwa Ummi 'Umarah Al-Answaariyyah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) kuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alimtembelea naye akamkaribisha kwa kumuwekea chakula. Akasema: "Kula." Akasema: "Hakika mimi nimefunga." Hapo Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akamwambia: "Hakika Malaaika wanamuombea aliyefunga kinapoliwa chakula mbele yake mpaka mwenye kula aondoke", na huenda alisema: "Mpaka ashibe." [At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan]

 

Hadiyth – 3

وعن أنسٍ رضي اللهُ عنه : أنَّ النبيَّ صلى الله عليه وسلم جَاءَ إِلَى سعد بن عبادة رضي اللهُ عنه فَجَاءَ بِخُبْزٍ وَزَيْتٍ ، فَأكَلَ ، ثُمَّ قَالَ النبي صلى الله عليه وسلم : (( أفْطَرَ عِنْدَكُمُ الصَّائِمُونَ ؛ وَأكَلَ طَعَامَكُمُ الأَبرَارُ ، وَصَلَّتْ عَلَيْكُمُ المَلاَئِكَةُ )) رواه أَبُو داود بإسناد صحيح .

Imepokewa kutoka kwa Anas (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikwenda kwa Sa'ad bin 'Ubaadah (Radhwiya allahu 'anhu), naye akamletea mkate na mafuta na Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akala hicho chakula, kisha akasema: "Aftwara 'indakumus Swaa'imuuna wa akala twa'aamakumul Abraar wa Swallat 'alaykumul Malaaikah - Wamefuturu kwenu walio funga na watu wema wamekula chakula chenu na Malaaika wamewaombea nyinyi maghfira." [Abu Daawuwd kwa Isnaad iliyo Swahiyh]

 

 

Share