03-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Fadhila za Kuacha Huru Watumwa

 

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

باب فضل العتق

03-Mlango Wa Fadhila za Kuacha Huru Watumwa

 

Alhidaaya.com

 

قال الله تَعَالَى :

فَلَا اقْتَحَمَ الْعَقَبَةَ ﴿١١﴾

Basi hakujiingiza kwa juhudi njia ya tabu na mashaka. 

وَمَا أَدْرَاكَ مَا الْعَقَبَةُ ﴿١٢﴾

Na nini kitakachokujulisha nini hiyo njia ya tabu na mashaka?

فَكُّ رَقَبَةٍ ﴿١٣﴾

Ni kuacha huru mtumwa. [Al-Balad: 11-13]

 

Hadiyth – 1

وعن أَبي هريرة رضي اللهُ عنه قَالَ : قَالَ لي رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( مَنْ أَعْتَقَ رَقَبَةً مُسْلِمَةً أعْتَقَ اللهُ بِكُلِّ عُضْوٍ مِنْهُ ، عُضْواً مِنْهُ في النَّارِ ، حَتَّى فَرْجَهُ بِفَرْجِهِ )) متفقٌ عَلَيْهِ .

Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Atakayeacha huru shingo ya mtumwa Muislamu, Allaah atamwacha huru na moto kila kiungo cha mtumwa kwa kiungo cha muacha huru hata tupu kwa tupu." [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

Hadiyth – 2

وعن أَبي ذرٍ رضي اللهُ عنه قَالَ : قُلْتُ : يَا رسول الله ، أيُّ الأعمَالِ أفْضَلُ ؟ قَالَ : (( الإيمَانُ بِاللهِ ، وَالجِهَادُ في سَبيلِ اللهِ )) قَالَ : قُلْتُ : أيُّ الرِّقَابِ أفْضَلُ ؟ قَالَ : (( أنْفَسُهَا عِنْدَ أَهْلِهَا ، وَأكْثَرُهَا ثَمَناً )) متفقٌ عَلَيْهِ .

Abu Dharr (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: "Nilisema: Ni amali gani bora zaidi?" Akasema: "Kumuamini Allaah na Jihaad katika njia Yake." Nikasema: "Kuacha gani mtumwa bora zaidi?" Akasema: "Mzuri zaidi kwa watu wake na mwenye thamani kubwa zaidi." [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

Share