Hiswnul Muslim - Du'aa Na Adhkaar Mbalimbali Kutoka Katika Qur-aan, Sunnah Na Athar

 

بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمن الرَّحيم

Kwa Jina La Allaah Mwingi Wa Rehema (Duniani) Mwenye Kurehemu (Akhera)

 

UTANGULIZI

Hakika sifa njema zote ni za Allaah, tunamsifu, tunamuomba msaada na tunamuomba maghfirah, tunamuomba Atuhifadhi na shari za nafsi zetu, na maovu ya matendo yetu. Anayemuongoza Allaah hapana wa kumpoteza, na Anayempoteza, hapana wa wa kumuongoza.  Nakiri kwamba, hapana apasaye kuabudiwa ila Allaah, hali ya kuwa peke Yake, hana mshirika, na ninakiri kwamba Muhammad ni mja Wake na ni Mtume Wake. Allaah Amrehemu na Awarehemu jamaa zake na Maswahaba zake na wanaowafuata hao kwa wema mpaka siku ya malipo na Amsalimishe kwa amani nyingi.

Baada ya yaliyotangulia huu ni ufupi (Mukhtasar) wa kitabu changu  kiitwacho “HISWN AL-MUSLIM MIN ADHKAAR AL-KITAAB WA SUNNAH

Ninamuomba Allaah kwa majina Yake mazuri, na sifa Zake zilizo juu, Ajaaliye kazi hii kuwa, imesafika  lengo lake, kwa kutaka radhi zake Allaah Mtukufu, na Aninufaishe kwa hayo katika uhai wangu huu, na baada ya kufa, na Amnufaishe atakayekisoma, kukichapisha, au aliyekuwa ni sababu ya kukitawanya, hakika  Yeye  Allaah Ndiye  Muweza.

Allaah Amrehemu Mtume wetu Muhammad صلى الله عليه وسلم na Aali zake na Maswahaba wake na wanaowafuata hao, kwa wema mpaka siku ya malipo.

 

************************

 

Share