13 Dua'a Ya Kwenda Msikitini
(19)
اللّهُـمَّ اجْعَـلْ فِي قَلْبـي نُوراً ، وَفي لِسَـانِي نُوراً، وَفِي سَمْعِي نُوراً, وَفِي بَصَرِيِ نُوراً, وَمِنْ فََوْقِي نُوراً , وَ مِنْ تَحْتِي نُوراً, وَ عَنْ يَمِينيِ نُوراَ, وعَنْ شِمَالِي نُوراً, وَمْن أَماَمِي نُوراً, وَمِنْ خَلْفيِ نُوراَ, واجْعَلْ فِي نَفْسِي نُوراً, وأَعْظِمْ لِي نُوراً, وَعظِّمْ لِي نُوراً, وَاجْعَلْ لِي نُوراً, واجْعَلنِي نُوراً, أللَّهُمَّ أَعْطِنِي نُوراً, واجْعَلْ فِي عَصَبِي نُوراً, وَفِي لَحْمِي نُوراً, وَفِي دَمِي نُوراً وَفِي شَعْرِي نُوراً, وفِي بَشَرِي نُوراً (أَللَّهُمَّ اجِعَلْ لِي نُوراً فِي قّبْرِي وَ نُوراَ فِي عِظاَمِي) (وَزِدْنِي نُوراً, وَزِدْنِي نُوراَ , وَزِدْنِي نُوراً) (وَهَبْ لِي نُوراً عَلَى نُوراً )
“Ewe Mwenyezi Mungu , weka katika moyo wangu nuru, na katika ulimi wangu nuru, na katika masikio yangu nuru, na katika macho yangu nuru, na juu yangu nuru, na chini yangu nuru, na kuliani kwangu nuru, na kushotoni kwangu nuru, na mbele yangu nuru, na nyuma yangu nuru, na weka katika nafsi yangu nuru, na nifanyie kubwa nuru, na nifanyie nyingi nuru, na uniwekee mimi nuru, na unifanyie mimi nuru, Ewe Mwenyezi Mungu nipe nuru, na uweke katika mishipa yangu nuru, na katika nyama yangu nuru, na katika damu yangu nuru, na katika nywele zangu nuru, na katika ngozi yangu nuru, (Ewe Mwenyezi Mungu niwekee nuru katika kaburi langu, na nuru katika mifupa yangu) (Na unizidishie nuru, na unizidishie nuru, na unizidishie nuru) (na unipe nuru juu ya nuru ) .
- Login or register to post comments
- Email this page


