16 Dua'a Za Adhana
Mtu akisikia Muadhini anaadhini anatakiwa asema kama anavyosema Muadhini, ila atakapo sema ;
(22)
حَـيَّ عَلـى الصَّلاة
‘Hayya ala Swalaah‘ “Njooni kwenye swala”
حَـيَّ عَلـى الْفَـلاح
‘Hayya alal falaah’ “Njoni kwenye mafanikio”
Yeye hatomuigiza bali anatakiwa aseme
لا حَـوْلَ وَلا قُـوَّةَ إِلاّ بِِالله
‘Laa Haula walaa quwwata Illaa Billah’
“Hapana uwezo wala nguvu ila za Mwenyezi Mungu “
Muadhini akisema : Ash-hadu anlaa Ilaaha illa Allah, ash-hadu anna Muhammada Rasuulu Allaah.
Anatikiwa mtu aseme ;
(23)
وَأَنا أَشْـهَدُ أَنْ لا إِلـهَ إِلاّ اللهُ وَحْـدَهُ لا شَـريكَ لَـه ، وَأَنَّ محَمّـداً عَبْـدُهُ وَرَسـولُه ، رَضيـتُ بِاللهِ رَبَّاً ، وَبِمُحَمَّـدٍ رَسـولاً وَبِالإِسْلامِ دينَـاً .
“Na mimi pia nakiri kwa moyo na kusema kwa ulimi kwamba hapana Mola apasae kuabudiwa kwa haki, ila Allaah Mmoja Peke Yake, hana mshirika wake na kwamba Muhammad ni mja Wake, na ni Mtume Wake. Nimeridhika kuwa Mwenyezi Mungu ndie Mola wangu, na kuwa Muhammad ni Mtume wangu, na kuwa Uislamu ndio dini yangu”
(24) Kisha baada ya kumjibu Muadhini atamswalia Mtume صلى الله عليه وسلم
Kisha atasema:
اللّهُـمَّ رَبَّ هَذِهِ الدّعْـوَةِ التّـامَّة وَالصّلاةِ القَـائِمَة آتِ محَـمَّداً الوَسيـلةَ وَالْفَضـيلَة وَابْعَـثْه مَقـامـاً مَحْـمُوداً الَّذي وَعَـدْتَه
“Ewe Mwenyezi Mungu , Bwana wa mlingano (mwito) huu uliotimia, na swala ilio simama, mpe Mtume Muhammad صلى الله عليه وسلم) Wasila, na fadhila, na mfikishe daraja yenye kusifiwa, ambayo umemuahidi.
(26) Inafaa mtu kujiombea kati ya Adhana na Iqaama kwani dua kati ya adhana na Iqamah hairudishwi .
- Login or register to post comments
- Email this page


