17 Dua'a Za Kufungulia Swala
(27)
اللّهُـمَّ باعِـدْ بَيـني وَبَيْنَ خَطـايايَ كَما باعَدْتَ بَيْنَ المَشْرِقِ وَالمَغْرِبْ ، اللّهُـمَّ نَقِّنـي مِنْ خَطايايَ كَمـا يُـنَقَّى الثَّـوْبُ الأَبْيَضُ مِنَ الدَّنَسْ ، اللّهُـمَّ اغْسِلْنـي مِنْ خَطايـايَ بِالثَّلـجِ وَالمـاءِ وَالْبَرَدْ
“Ewe Mwenyezi Mungu niweke mbali na madhambi yangu kama ulivyoweka mbali baina ya mashariki na magharibi, Ewe Mwenyezi Mungu nitakase na madhambi yangu kama vile inavyoitakaswa nguo nyeupe na uchafu, Ewe Mwenyezi Mungu nisafishe na madhambi yangu kwa theluji na kwa maji na kwa barafu”
(28)
سُبْـحانَكَ اللّهُـمَّ وَبِحَمْـدِكَ وَتَبارَكَ اسْمُـكَ وَتَعـالى جَـدُّكَ وَلا إِلهَ غَيْرُك
“Kutakasika ni Kwako ewe Mwenyezi Mungu , na sifa njema zote ni zako, na limetukuka jina lako, na utukufu niwako, na hapana apasae kuabudiwa kwahaki, asie kuwa Wewe”
(29)
وَجَّهـتُ وَجْهِـيَ لِلَّذي فَطَرَ السَّمـواتِ وَالأَرْضَ حَنـيفَاً وَمـا أَنا مِنَ المشْرِكين ، إِنَّ صَلاتـي ، وَنُسُكي ، وَمَحْـيايَ ، وَمَماتـي للهِ رَبِّ العالَمين ، لا شَريـكَ لَهُ وَبِذلكَ أُمِرْتُ وَأَنا مِنَ المسْلِـمين . اللّهُـمَّ أَنْتَ المَلِكُ لا إِلهَ إِلاّ أَنْت ،أَنْتَ رَبِّـي وَأَنـا عَبْـدُك ، ظَلَمْـتُ نَفْسـي وَاعْـتَرَفْتُ بِذَنْبـي فَاغْفِرْ لي ذُنوبي جَميعاً إِنَّـه لا يَغْـفِرُ الذُّنـوبَ إلاّ أَنْت .وَاهْدِنـي لأَحْسَنِ الأَخْلاقِ لا يَهْـدي لأَحْسَـنِها إِلاّ أَنْـت ، وَاصْـرِف عَـنّْي سَيِّئَهـا ، لا يَصْرِفُ عَـنّْي سَيِّئَهـا إِلاّ أَنْـت ، لَبَّـيْكَ وَسَعْـدَيْك ، وَالخَـيْرُ كُلُّـهُ بِيَـدَيْـك ، وَالشَّرُّ لَيْـسَ إِلَـيْك ، أَنا بِكَ وَإِلَيْـك ، تَبـارَكْتَ وَتَعـالَيتَ أَسْتَغْـفِرُكَ وَأَتوبُ إِلَـيك
“Nimeuelekeza uso wangu kwa yule ambae ameumba mbingu na ardhi hali ya kumtakasia yeye dini yangu, na sikuwa mimi ni katika washirikina, hakika swala yangu na kuchinja kwangu na uhai wangu, na kufa kwangu ni kwa Mwenyezi Mungu Bwana wa viumbe vyote, hana mshirika, na kwa hilo nimeamrishwa, nami ni katika waislamu. Ewe Mwenyezi Mungu , Wewe ndie mfalme, hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki ila Wewe, Wewe ndie Bwana wangu na mimi ni mtumwa (mja) wako. Nimedhulumu nafsi yangu, na nimekiri madhambi yangu kwa hivyo nisamehe madhambi yangu yote, hakika hasamehe madhambi, ila Wewe. Na niongoze kwenye tabia njema (nzuri), kwani haongozi kwenye tabia nzuri ila Wewe. Niepushe na tabia mbaya, kwani hakuna mwenye uwezo wakuniepusha na tabia mbaya ila Wewe. Naitikia mwito Wako, na ninafuraha kukutumikia, na kheri zote ziko mikononi Mwako, na shari haitoki Kwako, mimi nimepatikana kwa ajili Yako, na nitarudi KWako, umetakasika, na umetukuka, nakutaka msamaha na ninarejea Kwako (kwa kutubia )”
(30)
اللّهُـمَّ رَبَّ جِـبْرائيل ، وَميكـائيل ، وَإِسْـرافيل، فاطِـرَ السَّمواتِ وَالأَرْض ، عالـِمَ الغَيْـبِ وَالشَّهـادَةِ أَنْـتَ تَحْـكمُ بَيْـنَ عِبـادِكَ فيـما كانوا فيهِ يَخْتَلِفـون. اهدِنـي لِمـا اخْتُـلِفَ فيـهِ مِنَ الْحَـقِّ بِإِذْنِك ، إِنَّـكَ تَهْـدي مَنْ تَشـاءُ إِلى صِراطٍ مُسْتَقـيم
“Ewe Mwenyezi Mungu Mola wa Jibiriil na Mikaail na Israafil, Muumba wa mbingu na ardhi, Mjuzi wa mambo yaliojificha na yaliowazi, Wewe unahukumu baina ya waja Wako katika mambo ambayo walikuwa wakitafautiana, niongoze mimi kwenye haki katika yale waliotafautiana kwa ruhusu Yako. Hakika Wewe unamuongoza umtakae kwenye njia ilionyoka”
(31)
اللهُ أَكْبَـرُ كَبـيرا ، اللهُ أَكْبَـرُ كَبـيرا ، اللهُ أَكْبَـرُ كَبـيرا ، وَالْحَـمْدُ للهِ كَثـيرا ، وَالْحَـمْدُ للهِ كَثـيرا ، وَالْحَـمْدُ للهِ كَثـيرا ، وَسُبْـحانَ اللهِ بكْـرَةً وَأَصيـلا . ( ثَلاثاً )
“Mwenyezi Mungu ni Mkubwa, Mwenyezi Mungu ni Mkubwa, Mwenyezi Mungu ni Mkubwa, sifa njema ni za Mwenyezi Mungu , kwa wingi na sifa njema ni za Mwenyezi Mungu kwa wingi, na sifa njema ni za Mwenyezi Mungu kwa wingi, na ametakasika Mwenyezi Mungu asubuhi na jioni” (Utasema haya mara tatu)
أَعـوذُ بِاللهِ مِنَ الشَّـيْطانِ مِنْ نَفْخِـهِ وَنَفْـثِهِ وَهَمْـزِه
“Najilindia na Mwenyezi Mungu kutokana na shetani, na kupulizia kwake, na kutabana kwake na kutia kwake wasiwasi katika nyoyo za binaadamu”
(32)
Mtume صلى الله عليه وسلم alikuwa akiamka usiku ili kufanya ibada anasema :
اللّهُـمَّ لَكَ الْحَمْدُ أَنْتَ نـورُ السَّمـواتِ وَالأَرْضِ وَمَنْ فيـهِن ، وَلَكَ الْحَمْدُ أَنْتَ قَـيِّمُ السَّـمواتِ وَالأَرْضِ وَمَنْ فيـهِن ، [وَلَكَ الْحَمْدُ أَنْتَ رَبُّ السَّـمواتِ وَالأَرْضِ وَمَنْ فيـهِن] [وَلَكَ الْحَمْدُ لَكَ مُلْـكُ السَّـمواتِ وَالأَرْضِ وَمَنْ فيـهِن] [وَلَكَ الْحَمْدُ أَنْتَ مَلِـكُ السَّـمواتِ وَالأَرْضِ ] [وَلَكَ الْحَمْدُ] [أَنْتَ الْحَـقّ وَوَعْـدُكَ الْحَـق ، وَقَوْلُـكَ الْحَـق ، وَلِقـاؤُكَ الْحَـق، وَالْجَـنَّةُحَـق ، وَالنّـارُ حَـق ، وَالنَّبِـيّونَ حَـق ، وَمـحَمَّدٌ صلى الله عليه وسلم حق, والسَّعََةُحَـق] [اللّهُـمَّ لَكَ أَسْلَمت ، وَعَلَـيْكَ تَوَكَّلْـت ، وَبِكَ آمَنْـت ، وَإِلَـيْكَ أَنَبْـت ، وَبِـكَ خاصَمْت ، وَإِلَـيْكَ حاكَمْـت . فاغْفِـرْ لي مـا قَدَّمْتُ ، وَما أَخَّـرْت ، وَما أَسْـرَرْت ، وَما أَعْلَـنْت ] [أَنْتَ المُقَـدِّمُ وَأَنْتَ المُـؤَخِّر ، لا إِاـهَ إِلاّ أَنْـت] [أَنْـتَ إِلـهي لا إِاـهَ إِلاّ أَنْـت .
“Ewe Mwenyezi Mungu ni Zako sifa njema, Wewe ndie nuru ya mbingu na ardhi na vilivyomo ndani yake, na nizako sifa njema. Wewe ndie sababu ya kusimama kwa mbingu na archi na vilivyomo ndani yake, na nizako sifa njema, Wewe ndie Mola wa mbingu na ardhi na vilivyomo ndani yake; na nizako sifa njema, Wewe ndiye Mfalme wa mbingu na ardhi, na nizako sifa njema, Wewe ni Haki (kweli) na ahadi yako ni yakweli, na neno lako ni lakweli, na kukutana na Wewe ni kweli, na pepo ni kweli, na moto ni kweli, na Mitume ni kweli, na Muhammad صلى الله عليه وسلم ni kweli, na Qiyama ni kweli, Ewe Mwenyezi Mungu , Kwako nimejisalimisha, na kwako nimetegemea, nawewe nimekuamini, na Kwako nimerejea na kwa ajili yako nimeteta, na kwako nimehukumu, kwa hivyo nisamehe niliyoyatanguliza na niliyoyachelewesha, na niliyoyaficha na niliyoyatangaza; Wewe ndiye mwenye kuchelewesha, hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki ila Wewe; Wewe ndie Mola wangu, hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki ila Wewe”
- Login or register to post comments
- Email this page


