01-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Maudhi Tofauti Nzuri

 

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

 

باب أحاديث الدّجال وأشراط الساعة وغيرها

01-Mlango Wa Maudhi Tofauti Nzuri

 

Alhidaaya.com

 

Hadiyth – 1

عن النواس بن سمعان رضي الله عنه قال : ذَكَرَ رَسُولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم الدَّجَّالَ ذَاتَ غَدَاةٍ ، فَخَفَّضَ فِيهِ وَرَفَّعَ حَتَّى ظَنَنَّاهُ في طَائِفَةِ النَّخْلِ . فَلَمَّا رُحْنَا إلَيْهِ ، عَرَفَ ذلِكَ فِينَا ، فَقالَ : (( مَا شَأنُكُمْ ؟ )) قُلْنَا : يا رَسُولَ اللهِ ، ذَكَرْتَ الدَّجَّالَ الغَدَاةَ ، فَخَفَّضْتَ فِيهِ وَرَفَّعْتَ ، حَتَّى ظَنَنَّاهُ فِي طَائِفَةِ النَّخْلِ ، فقالَ : (( غَيْرُ الدَّجَّالِ أَخْوَفنِي عَلَيْكُمْ ، إنْ يَخْرُجْ وَأنَا فِيكُمْ ، فَأنَا حَجِيجُهُ دُونَكُمْ ؛ وَإنْ يَخْرُجْ وَلَسْتُ فِيكُمْ ، فَامْرُؤٌ حَجيجُ نَفْسِهِ ، واللهُ خَلِيفَتي عَلَى كُلِّ مُسْلِمٍ . إنَّهُ شَابٌّ قَطَطٌ عَيْنُهُ طَافِيَةٌ ، كَأنّي أُشَبِّهُهُ بعَبْدِ العُزَّى بنِ قَطَنٍ ، فَمَنْ أدْرَكَهُ مِنْكُمْ ، فَلْيَقْرَأ عَلَيْهِ فَواتِحَ سُورَةِ الكَهْفِ ؛ إنَّهُ خَارِجٌ خَلَّةً بَيْنَ الشَّامِ وَالعِرَاقِ ، فَعَاثَ يَمِيناً وَعَاثَ شِمالاً ، يَا عِبَادَ اللهِ فَاثْبُتُوا )) قُلْنَا : يَا رسُولَ اللهِ ، وَمَا لُبْثُهُ في الأرْضِ ؟ قال : (( أرْبَعُونَ يَوماً : يَوْمٌ كَسَنَةٍ ، وَيَوْمٌ كَشَهْرٍ ، وَيَوْمٌ كَجُمْعَةٍ ، وَسَائِرُ أيَّامِهِ كَأَيَّامِكُمْ )) قُلْنَا : يَا رَسُولَ اللهِ ، فَذلكَ اليَوْمُ الَّذِي كَسَنَةٍ أتَكْفِينَا فِيهِ صَلاَةُ يَوْمٍ ؟ قَال : (( لا ، اقْدُرُوا لَهُ قَدْرَهُ )) .

قُلْنَا : يا رسولَ اللهِ ، وَمَا إسْراعُهُ في الأرْضِ ؟ قال : (( كَالغَيْثِ اسْتَدْبَرَتْهُ الرِّيحُ ، فَيَأتِي عَلَى القَوْمِ ، فَيدْعُوهُم فَيُؤمِنُونَ بِهِ وَيَسْتَجِيبُونَ لَهُ ، فَيَأمُرُ السَّمَاءَ فَتُمْطِرُ ، وَالأرْضَ فَتُنْبِتُ ، فَتَرُوحُ عَلَيْهِمْ سَارِحَتُهُمْ أطْوَلَ مَا كَانَتْ ذُرىً وَأسْبَغَهُ ضُرُوعاً ، وأمَدَّهُ خَوَاصِرَ ، ثُمَّ يَأتِي القَوْمَ فَيَدْعُوهُمْ ، فَيَرُدُّونَ عَلَيْهِ قَولَهُ ، فَيَنْصَرفُ عَنْهُمْ ، فَيُصْبِحُونَ مُمْحِلِينَ لَيْسَ بِأيْدِيهِمْ شَيْءٌ مِنْ أمْوَالِهِمْ ، وَيَمُرُّ بِالخَرِبَةِ فَيَقُولُ لَهَا : أخْرِجِي كُنُوزَكِ ، فَتَتْبَعُهُ كُنُوزُهَا كَيَعَاسِيبِ النَّحْلِ، ثُمَّ يَدْعُو رَجُلاً مُمْتَلِئاً شَبَاباً فَيَضْرِبُهُ بِالسَّيْفِ، فَيَقْطَعُهُ جِزْلَتَيْنِ رَمْيَةَ الغَرَضِ، ثُمَّ يَدْعُوهُ ، فَيُقْبِلُ ، وَيَتَهَلَّلُ وَجْهُهُ يَضْحَكُ ، فَبَيْنَمَا هُوَ كَذلِكَ إذْ بَعَثَ اللهُ تَعَالَى المَسيحَ ابْنَ مَرْيَمَ (عَلَيْهِ السَّلام) ، فَيَنْزِلُ عِنْدَ المَنَارَةِ البَيْضَاءِ شَرْقِيَّ دِمَشقَ بَيْنَ مَهْرُودَتَيْنِ ، وَاضِعاً كَفَّيْهِ عَلَى أَجْنِحَةِ مَلَكَيْنِ ، إذا طَأطَأَ رَأسَهُ قَطَرَ ، وَإِذَا رَفَعَهُ تَحَدَّرَ مِنهُ جُمَانٌ كَاللُّؤْلُؤ ، فَلاَ يَحِلُّ لِكَافِرٍ يَجِدُ رِيحَ نَفَسِهِ إلاَّ مَاتَ ، وَنَفَسُهُ يَنْتَهِي إلى حَيثُ يَنْتَهِي طَرْفُهُ ، فَيَطْلُبُهُ حَتَّى يُدْرِكَهُ بِبَابِ لُدٍّ فَيَقْتُلُهُ ، ثُمَّ يَأتِي عِيسَى (عَلَيْهِ السَّلام) ، قَوماً قَدْ عَصَمَهُمُ اللهُ مِنهُ ، فَيَمْسَحُ عَنْ وُجُوهِهِمْ وَيُحَدِّثُهُمْ بِدَرَجَاتِهِمْ فِي الجَنَّةِ ، فَبَيْنَمَا هُوَ كَذلِكَ إذْ أوْحَى اللهُ تَعَالَى إلى عِيسَى (عَلَيْهِ السَّلام) : أنِّي قَدْ أخْرَجْتُ عِبَاداً لي لا يَدَانِ لأَحَدٍ بِقِتَالِهِمْ ، فَحَرِّزْ عِبَادِي إلى الطُّورِ . وَيَبْعَثُ اللهُ يَأجُوجَ وَمَأجُوجَ وَهُمْ مِنْ كُلِّ حَدَبٍ يَنْسِلُونَ ، فَيَمُرُّ أوائِلُهُمْ عَلَى بُحيرَةِ طَبَريَّةَ فَيَشْرَبُونَ مَا فِيهَا ، وَيَمُرُّ آخِرُهُمْ فَيَقُولُونَ : لَقَدْ كَانَ بهذِهِ مَرَّةً ماءٌ ، وَيُحْصَرُ نَبيُّ اللهِ عِيسَى (عَلَيْهِ السَّلام) وأصْحَابُهُ حَتَّى يَكُونَ رَأْسُ الثَّوْرِ لأَحَدِهِمْ خَيْراً مِنْ مِئَةِ دينَارٍ لأَحَدِكُمُ اليَوْمَ ، فَيَرْغَبُ نَبِيُّ اللهِ عِيسَى (عَلَيْهِ السَّلام) وأصْحَابُهُ رضي الله عنهم إلى اللهِ تَعَالَى ، فَيُرْسِلُ اللهُ تَعَالَى عَلَيْهِمُ النَّغَفَ في رِقَابِهِمْ، فَيُصْبِحُونَ فَرْسَى كَمَوْتِ نَفْسٍ وَاحِدَةٍ ، ثُمَّ يَهْبِطُ نَبِيُّ اللهِ عِيسَى (عَلَيْهِ السَّلام) ، وأصْحَابُهُ رضي الله عنهم إلى الأرْضِ ، فَلاَ يَجِدُونَ في الأرْضِ مَوْضِعَ شِبْرٍ إلاَّ مَلأَهُ زَهَمُهُمْ وَنَتَنُهُمْ ، فَيَرْغَبُ نَبِيُّ اللهِ عِيسَى (عَلَيْهِ السَّلام) وَأصْحَابُهُ رضي الله عنهم إلى اللهِ تَعَالَى ، فَيُرْسِلُ اللهُ تَعَالَى طَيْراً كَأَعْنَاقِ البُخْتِ ، فَتَحْمِلُهُمْ ، فَتَطْرَحُهُمْ حَيثُ شَاءَ اللهُ ، ثُمَّ يُرْسِلُ اللهُ عزوجل مَطَراً لاَ يُكِنُّ مِنهُ بَيْتُ مَدَرٍ وَلاَ وَبَرٍ ، فَيَغْسِلُ الأرْضَ حَتَّى يَتْرُكَهَا كَالزَّلَقَةِ ، ثُمَّ يُقَالُ للأرْضِ : أنْبِتي ثَمَرتكِ ، وَرُدِّي بَرَكَتَكِ ، فَيَوْمَئِذٍ تَأكُلُ العِصَابَةُ مِنَ الرُّمَّانَةِ ، وَيَسْتَظِلُّونَ بِقَحْفِهَا ، وَيُبَارَكُ فِي الرِّسْلِ حَتَّى أنَّ اللّقْحَةَ مِنَ الإِبِلِ لَتَكْفِي الفِئَامَ مِنَ النَّاسِ ؛ وَاللِّقْحَةَ مِنَ البَقَرِ لَتَكْفِي القَبِيلَةَ مِنَ النَّاسِ ، وَاللِّقْحَةَ مِنَ الغَنَمِ لَتَكْفِي الفَخِذَ مِنَ النَّاسِ ؛ فَبَيْنَمَا هُمْ كَذَلِكَ إذْ بَعَثَ اللهُ تَعَالَى ريحاً طَيِّبَةً فَتَأخُذُهُمْ تَحْتَ آبَاطِهِمْ فَتَقْبِضُ رُوحَ كُلِّ مُؤْمِنٍ وَكُلِّ مُسْلِمٍ ؛ وَيَبْقَى شِرَارُ النَّاسِ يَتَهَارَجُونَ فِيها تَهَارُجَ الحُمُرِ ، فَعَلَيْهِمْ تَقُومُ السَّاعَةُ )) . رواه مسلم .

Amesema An-Nawwaas bin Sam'aan: Asubuhi moja Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alitutajia kuhusu Dajjaal, na akamuelezea kama mtu duni na mara nyengine akamnyanyua (akamfanya mkubwa) mpaka tukadhania kuwa yuko katika mabustani ya mitende (iliyo karibu nasi. Tulipoondoka kwake, alitambua hilo kwetu (kuwa tuna wasiwasi mwingi), akasema: "Muna nini nyinyi?" Tukamjibu: "Ee Rasuli wa Allaah! ulitueleza kuhusu Dajjaal asubuhi, ulimdunisha na kumnyanyua mpaka tukadhani kuwa yuko katika bustani za mitende (zilizo karibu nasi)." Akasema: "Siwakhofei nyinyi Dajjaal, kwani akitokea nami niko nayi basi nitawalinda dhidi yake, na akitokezea nami siko pamoja nanyi kila mtu atajitetea na kujilinda mwenyewe. Na Allaah ni khalifa wangu kwa kila Muislamu katika kutokuwepo kwangu. Hakika yeye atakuwa ni kijana (baro baro), nywele zake zitakuwa timtimu na jicho lake moja limechomoza kana kwamba anashabihiana na 'Abdil-'Uzzaa bin Qatwan. Mwnye kukutana naye miongoni mwenu basi amsomee mwanzo wa Suwratil Kahf (Suwrah ya 18). Hakika yeye atajitokeza katika sehemu ya Khallah iliyoko baina ya Shaam na 'Iraaq. Ataleta uharibifu mkubwa sana na mauaji mengi kuliani na kushotoni. Enyi waja wa Allaah! Kuweni imara." Tukamuuliza: "Ee Rasuli wa Allaah! Atakaa kwa muda gani hapa duniani?" Akasema: "Siku arobaini: Siku moja ni sawa na mwaka mmoja, na siku nyengine sawa na wiki moja, na siku zilizobzkia zitakuwa sawa na siku zenu za kawaida." Tukauliza: "Ee Rasuli wa Allaah! Hiyo siku iliyo sawa na mwaka itatutosheleza ndani yake Swalaah ya siku?" Akasema: "Hapana, itabidi mupime kipimo kilicho kadiri ya siku." Tukamuuliza: "Ee Rasuli wa Allaah! Na kasi yake itakuwa vipi katika ardhi?" Akasema: "Itakuwa kama kiwingu kinacho sukumwa na upepo. Atafika kwa kaumu fulani, atawaita (kujiunga naye), nao watamuamini na kuitikia mwiyo wake. Ataziamrisha mbingu, nazo zitanyesha mvua na mimea itachepuza (itamea) katika ardhi. Ng'ombe wao watakaporudi jioni nundu zao zitakuwa zimenona, viwele vyao vimerefuka kwa wingi wa maziwa na wamejenga vizuri pembezoni mwao. Kisha atafika kwa kaumu nyengine, nyae atawaita wajiunge naye lakini watakataa mwito wake. Kwa ajili hiyo ataondoka sehemu hiyo, na hapo hapo watakumbwa na ukame na watakosa mali zao zote. Na atapita katika sehemu iliyohamwa, ataiambia: "Toa hazina yako", hazina hiyo itamfuata kama bomba la nyuki. Kisha atamuita mtu akiwa katika ujana wake wa siha muruwa kabisa, naye atampiga kwa upanga, hivyo kumkata vipande viwili, navyo (hivo vipande) vitawekwa mbali mbali kwa umbali wa kulenga shabaha (kwa mshale). Kisha atamuita, na hivyo vipande vitakuwa vinasogea na kurudi uhai wake huku akiwa anatabasamu. Atakapokuwa anafanya hilo, Allaah Ta'aalaa Atamtuma Masihi mwana wa Maryam ('Alayhis salaam), ambaye atateremka kwenye mnara mweupe, mashariki ya Damascus, akiwa amevaa mapande mawili ya nguo ya manjano na huku mikono yake ameiweka juu ya mbawa za Malaaikah wawili. Pale atakapoinamisha kichwa chake itaonekana kama matone tone ya maji yanadondoka kutoka kichwani mwake na atakapoinua kichwa chake itaonekana kama vile lulu inadondoka kwa sura ya matone. Hakuna kafiri yeyote atakayefikiwa na harufu yake isipokuwa atafariki na harufu yake inakomea masafa ya umbali na upeo wa jicho lake. Baadae mwana wa Maryam atamfuata na kumwinda Dajjaal na kumuwahi katika lango la Ludd (ni mji uliyoko Palestina karibu na maji wa Baytil Maqdis (Jerusalem)  (Lyddah) na kumuua. Kisha 'Iysaa ('Alayhis salaam) atakwenda kwa kaumu walio kingwa na Allaah kutokana na shari za Dajjaal, atawafuta nyuso zao na kuwajulisha daraja zao Peponi. Wakati huo 'Iysaa ('Alayhis salaam) atapata ufunuo kutoka kwa Allaah Ta'aalaa: "Hakika Mimi Nimewatoa waja Wangu ambao hakuna yeyote mwenye nguvu ya kupambana nao katika vita. Hivyo, wachukue waja Wangu kwenye Mlima Tuwr." Allaah Atawatuma Yaajuwj na Maajuwj ambao watashuka kutoka kila upande. Kikosi chao cha kwanza kitapita katika Ziwa la Twabariyah (Bahari ya Galilayo-Galilee) na watakunywa maji yote yaliyomo ndani yake na kikosi cha mwisho kitakapo pita kitasema: "Hakika sehemu hii wakati mmoja ilikuwa na maji." Nabiy wa Allaah, 'Iysaa ("Alayhis salaam) na Swahaaba zake watahusuriwa (hivyo kuwa katika shida) mpaka kiwe kichwa cha fahali wa ng'ombe alichonacho mmoja wao ni bora kuliko Dinari mia moja za mmoja wenu leo. Nabiy wa Allaah, 'Iysaa ('Alayhis salaam) na Swahaaba zake (Radhwiyah Allaahu 'anhum)  hapo watamuelekea Allaah Ta'aalaa na kumuomba, Allaah Ta'aalaa atatuma viini katika shingo zao (Yaajuwj na Maajuwj), hivyo kuwafanya wafe kwa ghafla kufikia asubuhi inayofuata. Hapo, Nabiy wa Allaah, 'Iysaa ('Alayhis salaam) na Swahaaba zake watashuka kwenye mlima huo lakini hawatapata nafasi hata shibiri iliyo tupu bila kuwa na maiti ya Yaajuwj na Maajuwj, na harufu mbaya inayotokana na kuoza kwa miili yao. Nabiy wa Allaah, 'Iysaa ('Alayhis salaam) na Swahaaba zake watamuomba Allaah Ta'aalaa, Ambaye atatuma ndege wakubwa mfano wa nundu ya ngamia ambao wataibeba miili yao ambapo Allaah Atapenda. Baadae Allaah Ta'aalaa Atateremsha mvua ambayo itanyesha kila sehemu yenye makao ya watu sawa makazi hayo yametengenezwa na udongo au manyoa, hivyo ardhi itasafishwa iwe kama kioo. Kisha ardhi itaambiwa: "Chepuza matunda yako na rudisha baraka uliokuwa nayo." Siku hiyo komamanga moja litakuwa na kundi la watu, ambacho (kundi hilo) litaweza kukaa chini ya kivuli cha majani yake. Maziwa yatakuwa mengi kiasi ambacho ngamia mmoja atawatosheleza kundi la watu, na maziwa ya ng'ombe mmoja yatawatosha kabila zima la watu na yale ya mbuzi yatatosha watu walio duni ya kabila. Watakapokuwa katika neema na baraka hiyo, Alaah Ta'aalaa Atatuma upepo mwanana, ambao utawagusa makapwani mwao, hivyo kuchukua roho ya kila Muumini na kila Muislamu. Na hapo watabaki wale waovu miongoni mwa watu ambao watakuwa wanafanya zinaa na wanawake dhahiri shahiri kama punda na bila ya kuona haya yoyote. Na juu ya watu hao ndio Qiyaamah kitasimama." [Muslim].

 

Hadiyth – 2

وعن رِبعِيِّ بنِ حِرَاشٍ ، قال : انطلقت مع أبي مسعود الأنصاري إلى حُذَيفَةَ بن اليمان رضي الله عنهم ، فقال له أبو مسعود : حَدِّثْنِي ما سَمِعْتَ مِنْ رَسُولِ اللهِ صلى الله عليه وسلم ، في الدَّجَّالِ ، قال : (( إنَّ الدَّجَّالَ يَخْرُجُ ، وإنَّ مَعَهُ مَاءً وَنَاراً ، فَأَمَّا الَّذِي يَرَاهُ النَّاسُ مَاءً فَنَارٌ تُحْرِقُ، وأمَّا الَّذِي يَرَاهُ النَّاسُ نَاراً ، فَمَاءٌ بَارِدٌ عَذْبٌ . فَمَنْ أدْرَكَهُ مِنْكُمْ ، فَلْيَقَعْ فِي الَّذي يَراهُ نَاراً، فَإنَّهُ مَاءٌ عَذْبٌ طَيِّبٌ )) فقال أبو مسعود: وَأنَا قَدْ سَمِعْتُهُ . متفق عليه .

Amesema Rib'iyy bin Hiraash: Tuliondoka pamoja na Abi Mas'uwd Al-Answaariy (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuelekea kwa Hudhayfah Al-Yamaaniy (Radhwiya Allaahu 'anhu) akamwambia yeye Abu Mas'uwd (Radhwiya Allaahu 'anhu): "Nihadithie ulichosikia kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kuhusu Dajjaal." Akasema: "Hakika Dajjaal atatoka, na bila shaka akitoka atakuwa na maji na moto (yaani anaamrisha kwa kutumia hivyo vitu). Ama kile watakina watu kuwa ni maji baridi basi huo ni moto unaounguza. Na ama kile watakachokiona watu kuwa ni moto basi hayo ndio maji baridi yaliyo matamu. Atakaye kutana naye miongoni mwenu, basi aangukie katika ambacho watu wanakiona ni moto, basi hayo ni maji matamu yaliyo mazuri." Hapo akasema Abu Mas'uwd (Radhwiya Allaahu 'anhu): "Nami kwa hakika nilisikia (yaani Nabiy Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) hayo." [Al-Bukhaariy na Muslim].

 

Hadiyth – 3

 

 

 

عن عبد الله بن عمرو بن العاص رضي الله عنهما ، قال : قال رسولُ الله صلى الله عليه وسلم : (( يَخْرُجُ الدَّجَّالُ في أُمَّتِي فَيَمْكُثُ أرْبَعِينَ ، لاَ أدْرِي أرْبَعِينَ يَوماً أو أرْبَعِينَ شَهْراً ، أو أرْبَعِينَ عَاماً ، فَيَبْعَثُ اللهُ تَعالَى عِيسَى ابْنَ مَرْيَمَ (عَلَيْهِ السَّلام) ، فَيَطْلُبُهُ فَيُهْلِكُهُ ، ثُمَّ يَمْكُثُ النَّاسُ سَبْعَ سِنِينَ لَيسَ بَينَ اثْنَينِ عَدَاوةٌ ، ثُمَّ يُرْسِلُ اللهُ عزوجل ، ريحاً بَارِدَةً مِنْ قِبَلِ الشَّامِ ، فَلاَ يَبْقَى عَلَى وَجْهِ الأَرْضِ أَحَدٌ فِي قَلْبِهِ مِثْقَالُ ذَرَّةٍ مِنْ خَيرٍ أو إيمَانٍ إلاَّ قَبَضَتْهُ ، حَتَّى لو أنَّ أَحَدَكُمْ دَخَلَ فِي كَبِدِ جَبَلٍ ، لَدَخَلَتْهُ عَلَيهِ حَتَّى تَقْبِضَهُ ، فَيَبْقَى شِرَارُ النَّاسِ في خِفَّةِ الطَّيْرِ ، وأحْلامِ السِّبَاعِ ، لاَ يَعْرِفُونَ مَعْرُوفاً ، ولا يُنْكِرُونَ مُنْكَراً ، فَيَتَمَثَّلُ لَهُمُ الشَّيْطَانُ ، فيَقُولُ : ألاَ تَسْتَجِيبُونَ ؟ فَيَقُولُونَ : فَمَا تأمُرُنَا ؟ فَيَأمُرُهُمْ بِعِبَادَةِ الأوْثَانِ ، وَهُمْ في ذلِكَ دَارٌّ رِزْقُهُمْ ، حَسَنٌ عَيشُهُمْ ، ثُمَّ يُنْفَخُ في الصُّورِ ، فَلاَ يَسْمَعُهُ أحَدٌ إلاَّ أصْغَى لِيتاً وَرَفَعَ لِيتاً ، وَأوَّلُ مَنْ يَسْمَعُهُ رَجُلٌ يَلُوطُ حَوْضَ إبِلِهِ فَيُصْعَقُ ويُصْعَقُ النَّاسُ حولهُ ، ثُمَّ يُرْسِلُ اللهُ -أو قالَ: يُنْزِلُ اللهُ - مَطَراً كَأَنَّهُ الطَّلُّ أو الظِّلُّ ، فَتَنْبُتُ مِنهُ أجْسَادُ النَّاسِ ، ثُمَّ يُنْفَخُ فِيهِ أُخْرَى فَإِذَا هُمْ قِيَامٌ يَنْظُرُونَ ، ثُمَّ يُقالُ : يا أَيُّهَا النَّاسُ هَلُمَّ إلَى رَبِّكُمْ ، وَقِفُوهُمْ إنَّهُمْ مَسْئُولُونَ ، ثُمَّ يُقَالُ : أخْرِجُوا بَعْثَ النَّارِ فَيُقَالُ : مِنْ كَمْ ؟ فَيُقَالُ : مِنْ كُلِّ ألْفٍ تِسْعَمِئَةٍ وَتِسْعَةً وتِسْعِينَ ؛ فَذَلِكَ يَومٌ يَجْعَلُ الوِلْدَانَ شِيباً ، وَذَلِكَ يَومَ يُكْشَفُ عَنْ سَاقٍ )) . رواه مسلم .

Amesimulia 'Abdullaah bin 'Amr bin Al-'Aasw (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Dajjaal atatokea kwa Ummah wangu na ataishi arobaini, (sina hakika ni siku arobaini au miezi arobaini au miaka arobaini). Kisha Allaah (تبارك وتعالى) Atamtuma 'Iysaa mwana wa Maryam, ambaye atamwinda na kumuua. Kisha watu wataishi kwa miaka saba hapana kabisa uadui wala ugomvi baina ya watu wawili. Baadae Allaah (عزّ وجلّ) Atatuma upepo baridi kutoka Shaam, na hatobaki juu ya mgongo wa ardhi yeyote mwenye chembe ndogo kabisa ya kheri au imaan moyoni mwake isipokuwa utachukua roho yake hata lau mmoja wenu ataingia katika pango la jabali, upepo huo utamwingilia humo uchukue roho yake.  Hapo watabaki walio waovu pekee miongoni mwa watu ambao watapaparikia uasherati kama anavyopaparika ndege na watakuwa na tabia za kinyama. Hawatajua mema wala hawatakataza maovu. Shaytwaan atakuja kwao kwa mfano wa mwanaadam na kuwauliza: Je, mutaniitikia wito wangu?  Watasema: Kwani unatuamuru nini? Atawaamuru waabudu masanamu, na wao katika kufanya hivyo watapata riziki zao na maisha yao yatakuwa mazuri. Kisha baragumu litapulizwa, hakuna atakayesikia isipokuwa atageuza shingo upande wake (wa hiyo sauti) na kuinyanyua. Wa kwanza kuisikia atakuwa ni mtu anayeshughulika katika kutengeneza birika ya maji kwa ajili ya ngamia wake. Atakapoisikia sauti hiyo atafazaika (atakufa kwa mshtuko) na watu wengine nao watakufa kwa mshtuko. Kisha Allaah Atatuma au alisema: Allaah Atateremsha - mvua kana kwamba ni matone ya umande au kivuli. Hii itafanya miili ya watu ikue, kisha baragumu litapulizwa mara nyengine na hapo watasimama watu na huku wanaangalia. Kisha kutasemwa: Enyi watu! Njooni mbele ya Rabb wenu na wasimamisheni kwani wao wataulizwa. Kisha itatolewa amri: Watoeni wale ambao ni wa motoni. Kutaulizwa: Wangapi? Wataambiwa: Katika kila elfu watoeni mia tisa na tisini na tisa (999). Hiyo ndiyo siku ambayo itawafanya watoto wadogo waote mvi, na hiyo ni siku ambayo muundi (wa Allaah) utawachwa wazi." [Muslim]

 

Hadiyth – 4

وعن أنس رضي الله عنه قال : قال رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( لَيسَ مِنْ بَلَدٍ إلاَّ سَيَطَؤُهُ الدَّجَّالُ إلاَّ مَكَّةَ وَالمَدِينَةَ ؛ وَلَيْسَ نَقْبٌ مِنْ أنْقَابِهِمَا إلاَّ عَلَيْهِ المَلاَئِكَةُ صَافِّينَ تَحْرُسُهُمَا ، فَيَنْزِلُ بالسَّبَخَةِ ، فَتَرْجُفُ المَدِينَةُ ثَلاَثَ رَجَفَاتٍ ، يُخْرِجُ اللهُ مِنْهَا كُلَّ كافِرٍ وَمُنَافِقٍ ))  . رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwa Anas (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Hakuna mji isipokuwa Dajjaal atauteka ila Makkah na Madiynah. Hakuna katika njia zake isipokuwa kutakuwa na safu za Malaaikah wanaolinda. Dajjaal atateremka Sabakhah, na mji wa Madiynah utakumbwa na mitetemeko mitatu, ambapo kwayo Allaah Atamtoa kila kafiri na mnafiki." [Muslim]

 

Hadiyth – 5

وعن أنس رضي الله عنه : أنَّ رسُولَ الله صلى الله عليه وسلم قال : (( يَتْبَعُ الدَّجَّالَ مِنْ يَهُودِ أَصْبَهَانَ سَبْعُونَ ألْفاً عَلَيْهِم الطَّيَالِسَةُ )) . رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwa Anas (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Dajjaal atafuatwa na Mayahudi wa Asfahaan elfu sabiini waliovaa nguo za kishetani." [Muslim]

 

Hadiyth – 6

وعن أم شريكٍ رضي الله عنها : أنها سَمِعَتِ النَّبيّ صلى الله عليه وسلم ، يقولُ : (( لينْفِرَنَّ النَّاسُ مِنَ الدَّجَّالِ فِي الجِبَالِ )) . رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwake Umm Shariyk (Radhwiya Allaahu 'anhaa) kuwa amemsikia Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: "Watu watakimbilia kwenye majabali ili kujihifadhi na sharti ya Dajjaal." [Muslim]

 

Hadiyth – 7

وعن عمران بن حُصينٍ رضي الله عنهما، قال : سمعتُ رسولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم يقولُ : (( مَا بَيْنَ خَلْقِ آدَمَ إلى قِيَامِ السَّاعَةِ أَمْرٌ أكْبَرُ مِنَ الدَّجَّالِ )) . رواه مسلم .

Amesema 'Imraan bin Huswayn (Radhwiya Allaahu 'anhumaa): Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam akisema: "Baina ya kuumbwa kwa Aadam mpaka kusimama Qiyaamah hakuna janga kubwa zaidi kuliko kuja kwa Dajjaal." [Muslim]

 

Hadiyth – 8

وعن أبي سعيدٍ الخدري رضي الله عنه ، عن النبيّ صلى الله عليه وسلم قال : (( يَخْرُجُ الدَّجَّالُ فَيَتَوجَّهُ قِبَلَهُ رَجُلٌ مِنَ المُؤمِنِينَ فَيَتَلَقَّاهُ المَسَالِحُ : مَسَالِحُ الدَّجَّال . فَيقُولُونَ لَهُ : إلى أيْنَ تَعْمِدُ فَيَقُولُ : أعْمِدُ إلى هذَا الَّذِي خَرَجَ . فَيَقُولُونَ لَهُ : أوَمَا تُؤْمِنُ بِرَبِّنَا ؟ فَيقُولُ : مَا بِرَبِّنَا خَفَاءٌ ! فَيَقُولُونَ : اقْتُلُوهُ . فَيقُولُ بَعْضُهُمْ لِبَعْضٍ : ألَيْسَ قَدْ نَهَاكُمْ رَبُّكُمْ أنْ تَقْتُلُوا أحَداً دُونَهُ ، فَيَنْطَلِقُونَ بِهِ إلى الدَّجَّالِ ، فَإذَا رَآهُ المُؤْمِنُ قالَ : يا أيُّهَا النَّاسُ ، إنَّ هذَا الدَّجَّال الَّذي ذَكَرَ رَسُولُ الله صلى الله عليه وسلم ؛ فَيَأمُرُ الدَّجَّالُ بِهِ فَيُشَبَّحُ ؛ فَيَقُولُ : خُذُوهُ وَشُجُّوهُ . فَيُوسَعُ ظَهْرُهُ وَبَطْنُهُ ضَرْباً ، فَيقُولُ : أَوَمَا تُؤْمِنُ بِي ؟ فَيَقُولُ : أَنْتَ المَسِيحُ الكَذَّابُ ! فَيُؤْمَرُ بِهِ ، فَيُؤْشَرُ بِالمنْشَارِ مِنْ مَفْرِقِهِ حَتَّى يُفَرِّقَ بَيْنَ رِجْلَيْهِ . ثُمَّ يَمْشِي الدَّجَّالُ بَيْنَ القِطْعَتَيْنِ ثُمَّ يَقُولُ لَهُ : قُمْ ، فَيَسْتَوِي قَائِماً . ثُمَّ يَقُولُ لَهُ : أَتُؤْمِنُ بِي ؟ فَيَقُولُ : ما ازْدَدْتُ فِيكَ إلاَّ بَصِيرَةً . ثُمَّ يَقُولُ : يَا أَيُّهَا النَّاسُ إنَّهُ لاَ يَفْعَلُ بَعْدِي بِأَحَدٍ مِنَ النَّاسِ ؛ فَيَأخُذُهُ الدَّجَّالُ لِيَذْبَحَهُ ، فَيَجْعَلُ اللهُ مِا بَيْنَ رَقَبَتِهِ إلَى تَرْقُوَتِهِ نُحَاساً، فَلاَ يَسْتَطِيعُ إلَيهِ سَبيلاً، فَيَأخُذُهُ بِيَدَيْهِ وَرِجْلَيْهِ فَيَقْذِفُ بِهِ ، فَيَحْسَبُ النَّاسُ أَنَّهُ قَذَفَهُ إلَى النَّارِ ، وَإنَّمَا أُلْقِيَ فِي الجَنَّةِ )) . فَقَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم : (( هذا أعْظَمُ النَّاس شَهَادَةً عِندَ رَبِّ العَالَمِينَ )) . رواه مسلم . وروى البخاري بعضه بمعناه .

Imepokewa kutoka kwa Abu Sa'iyd Al-Khudriy (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Atakapokuja Dajjaal, mtu mmoja miongoni mwa Waumini atakwenda kwake na kukutana na walinzi wa Dajjaal ambao watamuuliza: 'Unakwenda wapi?' Atawaambia: "Ninaelekea kwa huyu aliyezuka.' Watamuuliza: 'Kwani wewe humuamini Mola wetu?' Atawaambia: 'Mola wetu (yaani Allaah) hana cha kuficha.' Watasema: 'Muueni.' Lakini baadhi yao watawaambia wengine ya kwamba si Mola wenu amewakataza kumuua yeyote pasi na ruhusa yake? Hivyo watakwenda naye kwa Dajjaal. Yule Muumini atakapomuona atasema: 'Enyi watu! Hakika huyu ni Dajjaal ambaye ametajwa na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam).' Dajjaal atawaamuru watu wake wamshike na wamnyooshe kwa matumbo yake. Atasema: 'Mchukueni na muadhibuni mpaka apate majeraha ya usoni na kichwani mwake.' Atapigwa dhoruba mgongoni na matumboni akiwa mwili mkavu (bila ya nguo). Kisha atamuuliza: 'Je, bado hujaamini?' Atamjibu: 'Wewe ni Masihi muongo.' Ataamrisha akatwe na msumeno kutoka kichwani mpaka kwenye funda la miguu yake. Kisha Dajjaal atatembea baina ya vipande hivyo viwili vya mwili wa huyo Muumini, na hapo atamuamuru: 'Simama', naye atasimama sawa sawa. Kisha atamwambia: 'Je, unaniamini?' Atamjibu: 'Sasa nimekuwa na uoni, yakini na ujuzi zaidi kukuhusu.' Kisha atasema: 'Enyi watu! Hakika huyu hataweza kumdhuru yeyote katika watu baada yangu.' Dajjaal atamshika ili apate kumchinja lakini Allaah Atamfanya kuanzia shingo yake mpaka mtulinga (juu mpaka chini) kuwa shaba, hivyo Dajjaal atashindwa kumuua (au kuwa na hila yoyote juu yake). Atamshika mikono na miguu yake na kumtupa na watu watafikiria kuwa amemtupa motoni lakini hakika ni kuwa atakuwa amemrusha Peponi." Akasema Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Mtu huyu atakuwa na daraja kubwa ya shahada mbele ya Rabb wa walimwengu." [Muslim]

 

Hadiyth – 9

وعن المغيرة بن شعبة رضي الله عنه قال : ما سألَ أَحَدٌ رسولَ الله صلى الله عليه وسلم عَن الدَّجَّالِ أَكْثَرَ مِمَّا سَألْتُهُ ؛ وإنَّهُ قَالَ لِي : (( مَا يَضُرُّكَ )) قُلْتُ : إنَّهُمْ يَقُولُونَ : إنَّ مَعَهُ جَبَلَ خُبْزٍ وَنَهَرَ مَاءٍ . قالَ : (( هُوَ أهْوَنُ عَلَى اللهِ مِنْ ذَلكَ )) . متفق عليه .

Amesema Al-Mughiyrah bin Shu'bah (Radhwiya Allaahu 'anhu): "Hakuna yeyote aliyemuuliza zaidi Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kuhusu Dajjaal, kama nilivyokuwa ninamuuliza mimi. Kwa hakika aliniambia: 'Hataweza kukudhuru.' Nikasema: 'Hakika wao wanasema: 'Hakika yeye atakuwa na mlima wa mkate na mto wa maji.' Akasema: 'Yeye ni duni mno kwa Allaah kuliko hivyo.' [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

Hadiyth – 10

وعن أنس رضي الله عنه قال : قال رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( مَا مِنْ نَبِيٍّ إلاَّ وَقَدْ أَنْذَرَ أُمَّتَهُ الأَعْوَرَ الكَذَّابَ ، ألاَ إنَّهُ أعْوَرُ ، وإنَّ رَبَّكُمْ عزوجل لَيْسَ بِأَعْوَرَ ، مَكْتُوبٌ بَيْنَ عَيْنَيْهِ ك ف ر )) . متفق عليه .

Imepokewa kutoka kwa Anas (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Hakuna Nabiy yeyote isipokuwa amewatahadharisha watu wake na mwenye jicho moja mrongo. Eleweni! Kuwa yeye ana jicho moja na hakika Rabb wenu hana jicho moja. Kati ya macho yake Dajjaal pameandikwa herufi KFR (yaani  kaafir au kafiri)." [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

Hadiyth – 11

وَعَن أبي هريرةَ tرضي الله عنه قال : قالَ رسولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم : (( ألا أُحدِّثُكمْ حديثاً عن الدجالِ ما حدَّثَ بهِ نبيٌّ قَومَهُ ! إنَّهُ أعورُ ، وَإنَّهُ يجيءُ مَعَهُ بِمِثالِ الجنَّةِ والنَّارِ ، فالتي يقولُ إنَّها الجَنَّةُ هي النَّار )) . متفقٌ عليهِ .

Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: " Hamtaki niwaeleze kisa cha Dajjaal, ambacho hakupata Nabiy yeyote kuwaelezea watu wake? Hakika yeye ni mwenye jicho moja, na hakika atakuja na mfano wa pepo moto kile ambacho atasema ndio pepo, basi huo ni moto." [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

Hadiyth – 12

وعن ابن عمر رضي الله عنهما : أنَّ رسولَ الله صلى الله عليه وسلم ذَكَرَ الدَّجَّالَ بَيْنَ ظَهْرَانَي النَّاسِ ، فَقَالَ : (( إنَّ اللهَ لَيْسَ بِأعْوَرَ ، ألاَ إنَّ المَسِيحَ الدَّجَّالَ أَعْوَرُ العَيْنِ اليُمْنَى ، كَأنَّ عَيْنَهُ عِنَبَةٌ طَافِيَةٌ )) . متفق عليه .

Imepokewa kutoka kwa Ibn 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Siku alimueleza mbele ya watu Dajjaal akasema: 'Hakika Allaah si chongo, eleweni kuwa Masihi Dajjaal hana jicho la upande wa kuliani, na basi jicho lake hilo linakuwa kama zabibu iliyoelea." [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

Hadiyth – 13

وعن أبي هريرة رضي الله عنه : أنَّ رسولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم قال : (( لاَ تَقُومُ السَّاعَةُ حَـتَّى يُقَاتِلَ المُسْلِمُونَ اليَهُودَ ، حَتَّى يَخْتَبِئَ اليَهُودِيُّ مِنْ وَرَاء الحَجَرِ وَالشَّجَرِ . فَيَقُولُ الحَجَرُ وَالشَّجَرُ : يَا مُسْلِمُ هذَا يَهُودِيٌّ خَلْفِي تَعَالَ فَاقْتُلْهُ ؛ إلاَّ الغَرْقَدَ فإنَّهُ مِنْ شَجَرِ اليَهُودِ )) . متفق عليه .

Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Qiyaamah hakitafika mpaka Waislamu wapigane na Mayahudi. Mayahudi watakuwa wanauliwa na kujificha nyuma ya miti na mawe. Miti na mawe itasema: 'Ee Muislamu, Ee mja wa Allaah, njoo nyuma yangu yupo Yahudi umuue ila mti wa Gharqad (ni mti wenye miba mikubwa na inapatikana kwa wingi katika ardhi ya Palestina) kwani huo ni mti wa Mayahudi." [Muslim]

 

Hadiyth – 14

وعن أبي هريرة رضي الله عنه قال : قالَ رسولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم : (( والَّذِي نَفْسِي بِيَدِهِ لاَ تَذْهَبُ الدُّنْيَا حَتَّى يَمُرَّ الرجُلُ على القَبْرِ ، فَيَتَمَرَّغَ عَلَيْهِ وَيَقُولُ : يَالَيْتَنِي كُنْتُ مَكَانَ صَاحِبِ هذَا القَبْرِ ، وَلَيْسَ بِهِ الدِّينُ ، ما بِهِ إلاَّ البَلاَءُ )) . متفق عليه .

Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Naapa kwa Yule ambaye nafsi yangu iko mikononi Mwake dunia hii haitaondoka mpaka mtu apite kwenye kaburi, kisha atarudi na aseme: 'Natamani niwe mahala pake.' Hatasema haya kwa ajili ya Dini (na Imani), lakini atasema hayo kwa sababu ya balaa na kukata tama." [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

Hadiyth – 15

وعن أبي هريرة رضي الله عنه قال : قال رسولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم : (( لاَ تَقُومُ السَّاعَةُ حَتَّى يَحْسِرَ الفُرَاتُ عَنْ جَبَلٍ مِنْ ذَهَبٍ يُقْتَتَلُ عَلَيْهِ ، فَيُقْتَلُ مِنْ كُلِّ مِئَةٍ تِسْعَةٌ وَتِسْعُونَ ، فَيَقُولُ كُلُّ رجُلٍ مِنْهُمْ : لَعَلِّي أنْ أكُونَ أنَا أنْجُو )) .

وَفي رواية : (( يُوشِكُ أنْ يَحْسِرَ الفُرَاتُ عَنْ كَنْزٍ مِنْ ذَهَبٍ ، فَمَنْ حَضَرَهُ فَلاَ يَأخُذْ مِنْهُ شَيْئاً )) . متفق عليه .

Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Hakitasimama Qiyaamah mpaka Mto wa Furati utoe jabali la dhahabu, na watu watapigana kwa ajili ya hiyo dhahabu na wengi watauliwa. Katika kila watu watapigana kwa ajili ya hiyo dhahabu na wengi watauliwa. Katika kila watu mia, tisini na tisa watauliwa, hapo atasema kila mtu: 'Huenda nikawa ni mimi ndiye mwenye kuokoka."

Na katika riwaayah nyengine: "Karibu mto wa Furati utafunua hazina ya dhahabu, atakayeifikia (na kuhudhuria wakati huo) asichukue kitu chochote katika dhahabu hiyo." [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

Hadiyth – 16

وعن أبي هريرة رضي الله عنه ، قال : سمعتُ رسولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم يقولُ : (( يَتْرُكُونَ المَدِينَةَ عَلَى خَيْرِ مَا كَانَتْ ، لاَ يَغْشَاهَا إلاَّ العَوَافِي يُريد - عَوَافِي السِّبَاعِ والطَّيرِ - وَآخِرُ مَنْ يُحْشَرُ رَاعِيَانِ مِنْ مُزَيْنَةَ يُرِيدَانِ المَدِينَةَ يَنْعِقَانِ بِغَنَمِهِمَا فَيَجِدَانِهَا وُحُوشاً ، حَتَّى إذَا بَلَغَا ثَنِيَّةَ الودَاعِ خَرَّا عَلَى وُجُوهِهمَا )) . متفق عليه .

Amesema Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu): Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: "Watu wataiacha Madiynah japokuwa iko katika ubora wake ulionao; hawatabaki Madiynah isipokuwa wanaojitafutia riziki zao miongoni mwa wanyama wakali na ndege. Na watu wa mwisho kufa ni wachunga wawili wa mbuzi wa kabila la Muzaynah wakiwa wanakusudia kwenda Madiynah lakini hawamkuti yeyote ila wanyama pori hadi watakapofika katika bonde la Thaniyatul kifudifudi wakiwa wameshakufa." [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

Hadiyth – 17

وعن أبي سعيد الخدري رضي الله عنه : أنَّ النبيَّ صلى الله عليه وسلم قال : (( يكُونُ خَلِيفَةٌ مِنْ خُلَفَائِكُمْ فِي آخِرِ الزَّمَانِ يَحْثُو المَالَ وَلاَ يَعُدُّهُ )) . رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwa Abu Sa'iyd Al-Khudriy (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Karibu na Qiyaamah kutakuwa na mmoja miongoni mwa Makhalifa wenu ambaye atakuwa angawa hela (mali) bila kuhesabu." [Muslim]

 

Hadiyth – 18

وعن أبي موسى الأشعريِّ رضي الله عنه : أنَّ النبيَّ صلى الله عليه وسلم قال : (( لَيَأتِيَنَّ عَلَى النَّاسِ زَمَانٌ يَطُوفُ الرَّجُلُ فِيهِ بالصَّدَقَةِ مِنَ الذَّهَبِ فَلاَ يَجِدُ أَحَداً يَأخُذُهَا مِنهُ ، وَيُرَى الرَّجُلُ الوَاحِدُ يَتْبَعُهُ أرْبَعُونَ امْرَأَةً يَلُذْنَ بِهِ مِنْ قِلَّةِ الرِّجَالِ وَكَثْرَةِ النِّسَاءِ )) . رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwa Abu Muwsaa Al-Ash'ariy (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Utakuja kwa watu wakati ambapo mtu atazunguka na Swadaqah ya dhahabu na asipate mtu wa kuichukua kutoka kwake. Na kutakuwa na uchache wa wanaume na wingi na wanawake mpaka mwanaume mmoja atakuwa anafuatwa wastareheshwe naye." [Muslim]

 

Hadiyth – 19

وعن أبي هريرة رضي الله عنه ، عن النبيِّ صلى الله عليه وسلم ، قال : (( اشْتَرَى رَجُلٌ مِنْ رَجُلٍ عَقَاراً ، فَوَجَدَ الَّذِي اشْتَرَى العَقَارَ فِي عَقَارِهِ جَرَّةً فِيهَا ذَهَبٌ ، فَقَالَ لَهُ الَّذِي اشْتَرَى العَقَارَ : خُذْ ذَهَبَكَ ، إنَّمَا اشْتَرَيْتُ مِنْكَ الأَرْضَ وَلَمْ أشْتَرِ الذَّهَبَ ، وَقَالَ الَّذِي لَهُ الأَرْضُ : إنَّمَا بِعْتُكَ الأَرْضَ وَمَا فِيهَا ، فَتَحَاكَمَا إلَى رَجُلٍ ، فَقَالَ الَّذِي تَحَاكَمَا إلَيْهِ : أَلَكُمَا وَلَدٌ ؟ قالَ أحَدُهُما : لِي غُلاَمٌ ، وقالَ الآخَرُ : لِي جَارِيَةٌ قال : أنْكِحَا الغُلاَمَ الجَارِيَةَ ، وأنْفِقَا عَلَى أنْفُسِهمَا مِنْهُ وَتَصَدَّقَا )) . متفق عليه .

Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mtu mmoja alinunua shamba kutoka kwa mwengine. Yule aliyenunua ardhi hiyo akapata ndani yake chombo kilichojaa dhahabu. Akasema yule mnunuzi wa ardhi (kumuambia mwenziwe - muuzaji): 'Chukua dhahabu yako, kwani mimi nimenunu kwako ardhi na wala sikununua dhahabu.' Na akamjibu yule aliyeuza ardhi: 'Hakika mimi nimekuuzia ardhi na vilivyomo ndani yake.' Wakaipeleka kesi yao kwa mtu mwengine ili wahukumiwe. Yule hakimu akawauliza: 'Je, muna watoto?' Akasema mmoja wao: 'Mimi nina kijana wa kiume.' Na akasema wa pili: 'Mimi nina msichana.' Akasema yule hakimu: 'Muozeni kijana kwa huyo msichana (binti) na muitumie hiyo dhahabu kwao na sehemu yake nyengine itoweni Swadaqah'." [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

Hadiyth – 20

وعن أبي هريرة رضي الله عنه : أنَّه سمعَ رسُول الله صلى الله عليه وسلم يقولُ : (( كانت امْرَأَتَانِ مَعَهُمَا ابْنَاهُمَا ، جَاءَ الذِّئْبُ فَذَهَبَ بابْنِ إحْدَاهُمَا . فَقَالَتْ لِصَاحِبَتِهَا : إنَّمَا ذَهَبَ بِابْنِكِ ، وقالتِ الأخرَى : إنَّمَا ذَهَبَ بِابْنِكِ ، فَتَحَاكَمَا إلى دَاوُدَ صلى الله عليه وسلم فَقَضَى بِهِ لِلْكُبْرَى ، فَخَرَجَتَا عَلَى سُلَيْمَانَ بْنِ دَاوُد صلى الله عليه وسلم فَأَخْبَرَتَاهُ . فَقالَ : ائْتُونِي بِالسِّكِّينِ أشُقُّهُ بَيْنَهُمَا . فَقَالَتِ الصُّغْرَى : لاَ تَفْعَلْ ! رَحِمَكَ اللهُ ، هُوَ ابْنُهَا . فَقَضَى بِهِ للصُّغْرَى )) . متفق عليه .

Imepokewa kutoka kwake Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa amemsikia Rasuli wa Allaahu (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: "Wanawake wawili walikuwa na watoto wao wawili walikuwa na watoto wao wawili, akaja mbwa mwitu akamchukua mtoto wa mmoja wao. Mwezake akasema: 'Kamchukua mtoto wako.' Na yule mwengine naye akasema: 'Hakika amemchukua mtoto wako.' Kesi yao wakaipeleka kwa Daawuwd ('Alayhis salaam), akahukumu mtoto ni wa mkubwa; wote wakatoka kwenda kwa Sulaymaan bin Daawuwd ('Alayhis salaam) wakamuelezea, akawaambia: 'Nileteeni kisu nimpasue niwagawie.' Yule mdogo akasema: 'Usifanye hivyo, Allaah Akahukumu mtoto ni wa yule mdogo." [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

Hadiyth – 21

وعن مِرداس الأسلمي رضي الله عنه قال : قال النبيُّ صلى الله عليه وسلم : (( يَذْهَبُ الصَّالِحُونَ الأَوَّلُ فَالأَوَّلُ ، وَيَبْقَى حُثَالَةٌ كَحُثَالَةِ الشَّعِيرِ أوِ التَّمْرِ لاَ يُبَالِيهُمُ اللهُ بَالَةً )) . رواه البخاري .

Imepokewa kutoka kwa Mirdaas Al-Aslamiy (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Watu wema wataaga dunia mmoja baada ya mwengine na watabaki wale wasiokuwa na maana kama kapi ya shayiri au tende. Allaah Atawapuuza na kutowajali kabisa kipote hicho." [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

Hadiyth – 22

وعن رفاعة بن رافع الزُّرَقِيِّ رضي الله عنه قال : جاء جبريل إلى النبيّ صلى الله عليه وسلم قال : مَا تَعُدُّونَ أهْلَ بَدْرٍ فِيكُمْ ؟ قال : (( مِنْ أفْضَلِ المُسْلِمِينَ )) أوْ كَلِمَةً نَحْوَهَا . قال : وَكَذلِكَ مَنْ شَهِدَ بَدْراً مِنَ المَلائِكَةِ . رواه البخاري .

Amesema Rifaa'ah bin Raafi' Az-Zuraqiyy (Radhwiya Allaahu 'anhu): Alikuja Jibriyl ('Alayhis salaam): kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na kumuuliza: "Je, munawahesabu vipi watu waliopigana katika Vita vya Badr miongoni mwenu?" Akajibu (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Wanachukuliwa kuwa bora miongoni mwa Waislamu" au maneno mfano wa hayo. Akasema Jibriyl ('Alayhis salaam): "Na hivyo ndivyo wanavyochukuliwa wale Malaaikah walio hudhuria vita hivyo." [Al-Bukhaariy]

 

Hadiyth – 23

وعن ابن عمر رضي الله عنهما ، قال : قال رسولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم : (( إذَا أنْزَلَ اللهُ تَعَالَى بِقَومٍ عَذَاباً ، أصَابَ العَذَابُ مَنْ كَانَ فِيهِمْ ، ثُمَّ بُعِثُوا عَلَى أَعْمَالِهِمْ )) . متفق عليه .

Imepokewa kutoka kwa Ibn 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Allaah Ta'aalaa Anapoteremsha adhabu kwa kaumu (watu), adhabu hiyo huwapata wote waliomo ndani, kisha hao watu watafufuliwa Siku ya Qiyaamah kulingana na amali zao." [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

Hadiyth – 24

وعن جابر رضي الله عنه قال : كَانَ جِذْعٌ يَقُومُ إلَيْهِ النَّبيُّ صلى الله عليه وسلم - يَعْنِي فِي الخُطْبَةِ – فَلَمَّا وُضِعَ المِنْبَرُ سَمِعْنَا لِلجِذْعِ مِثْلَ صَوْتِ العِشَارِ ، حَتَّى نَزَلَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم ، فَوضَعَ يَدَهُ عَلَيهِ فَسَكَنَ .

وَفِي روايةٍ : فَلَمَّا كَانَ يَومُ الجُمُعَةِ قَعَدَ النَّبيُّ صلى الله عليه وسلم عَلَى المِنْبَرِ ، فَصَاحَتِ النَّخْلَةُ الَّتِي كَانَ يَخْطُبُ عِنْدَهَا حَتَّى كَادَتْ أنْ تَنْشَقَّ .

وفي رواية : فصَاحَتْ صِيَاحَ الصَّبيِّ، فَنَزَلَ النَّبيُّ صلى الله عليه وسلم ، حَتَّى أَخَذَهَا فَضَمَّهَا إلَيهِ ، فَجَعَلَتْ تَئِنُّ أَنِينَ الصَّبي الَّذِي يُسَكَّتُ حَتَّى اسْتَقَرَّتْ ، قال : (( بَكَتْ عَلَى مَا كَانَتْ تَسْمَعُ مِنَ الذَّكْرِ )) . رواه البخاري .

Amesema Jaabir (Radhwiya Allaahu 'anhu): Kulikuwa na shina la mtende ambalo Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akisimama kwayo yaani anapotoa khutbah, Baada ya kuletwa mimbar kwenye Msikiti wake (Nabiy Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam akawa anaitumia), mara tulisikia siku moja sauti kutoka kwa shina hilo mfano wa sauti ya ngamia mwenye mimba, mpaka Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alipoteremka na kuuweka mkono wake juu yake ndipo kilipotulia." 

Na katika riwaayah nyengine: "Ilikuwa ni siku ya Ijumaa, Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikaa juu ya mimbar, kishina cha mtende ambacho alikuwa akiegemea wakati wa kutoa khutbah kilipiga ukelele mpaka kikawa karibu kupajuka (kupasuka)." 

Na katika riwaayah nyengine: "Kikalia kilio cha mtoto, na hapo Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akashuka na kukikumbatia na hapo kikalia kilio cha mtoto anayeliwazwa mpaka kikatulia. Akasema: 'Kinalia kwa yale kilichokuwa kikisikia katika ukumbusho na khutbah." [Al-Bukhaariy]

 

Hadiyth – 25

وعن أبي ثعلبة الخُشَنِيِّ جُرثومِ بنِ ناشر رضي الله عنه ، عن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال : (( إنَّ اللهَ تَعَالَى فَرَضَ فَرَائِضَ فَلاَ تُضَيِّعُوهَا ، وَحَدَّ حُدُوداً فَلاَ تَعْتَدُوهَا ، وَحَرَّمَ أَشْيَاءَ فَلاَ تَنْتَهِكُوهَا ، وَسَكَتَ عَنْ أشْيَاءَ رَحْمَةً لَكُمْ غَيْرَ نِسْيَانٍ فَلاَ تَبْحَثُوا عَنْهَا )) حديث حسن . رواه الدارقطني وغيره .

Imepokewa kutoka kwa Tha'labah Al-Khushaniy Jurthum bin Naashir (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Hakika Allaah Ta'aalaa Amelalazimisha faradhi musiziwache, na Ameweka mipaka muiivuke na Ameharamisha mambo musiyafanye, na Amenyamaza juu ya mambo mengine ilihali ya kuwa ni rehema kwenu nyinyi bila ya kusahau, basi musiyapekue." [Hadiyth Hasan iliyopokewa na Ad-Daraqutniy na wengineo].

 

Hadiyth – 26

وعن عبد الله بن أبي أَوْفَى رَضِيَ اللهُ عَنهما ، قالَ : غَزَوْنَا مَعَ رَسولِ اللهِ صلى الله عليه وسلم سَبْعَ غَزَوَاتٍ نَأكُلُ الجَرَادَ .

وَفِي رِوَايةٍ : نَأكُلُ مَعَهُ الجَرَادَ . متفق عليه .

Amesema 'Abdillaah bin Abu Awfaa (Radhwiya Allaahu 'anhumaa): "Tulipigana tukiwa pamoja na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), vita saba, tulikuwa tunakula nzige."

Na katika riwaaya nyengine: "Tulikuwa tunakula naye nzige." [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

Hadiyth – 27

وعن أبي هريرة رضي الله عنه : أنَّ النبيَّ صلى الله عليه وسلم قال : (( لاَ يُلْدَغُ المُؤْمِنُ مِنْ جُحْرٍ وَاحِدٍ مَرَّتَيْنِ )) . متفق عليه .

Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Muumini haumwi mara mbili kutoka katika shimo moja." [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

Hadiyth – 28

وعن أبي هريرة رضي الله عنه، قال : قال رسول الله النبيَّ صلى الله عليه وسلم : (( ثَلاَثَةٌ لاَ يُكَلِّمُهُمُ اللهُ يَومَ القِيَامَةِ، وَلاَ يَنْظُرُ إلَيْهِمْ ، وَلاَ يُزَكِّيهِمْ ، وَلَهُمْ عَذَابٌ ألِيمٌ : رَجُلٌ عَلَى فَضْلِ مَاءٍ بِالفَلاَةِ يَمْنَعُهُ مِنِ ابْنِ السَّبِيلِ ، وَرَجُلٌ بَايَعَ رَجُلاً سِلْعَةً بَعْدَ العَصْرِ فَحَلَفَ بِاللهِ لأَخَذَهَا بِكذَا وَكَذَا فَصَدَّقَهُ وَهُوَ عَلَى غَيْرِ ذلِكَ ، وَرَجُلٌ بَايَعَ إمَاماً لاَ يُبَايِعُهُ إلاَّ لِدُنْيَا فَإنْ أَعْطَاهُ مِنْهَا وَفَى وَإنْ لَمْ يُعْطِهِ مِنْهَا لَمْ يَفِ )) . متفق عليه .

Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Aina tatu za watu ambao Allaah Hatozungumza nao Siku ya Qiyaamah wala Hatowaangalia wala Hatowasamehe madhambi yao (Hatowatakasa) na Atawapa adhabu kali sana: (a) Mtu mwnye maji ya ziada jangwani anawanyima wasafiri. (b) Na mtu aliyepanga bidhaa zake kuziuza baada ya Alasiri na akala kiapo cha uwongo kwa jina la Allaah kuwa amelipwa kadhaa na kadhaa kwa bidhaa hizo. Mnunuzi akamwamini na akazinunua bidhaa hizo kwa kiapo hicho hali ya kuwa si sahihi. (c) Na mtu aliyechukua ahadi ya utii kwa kiongozi na akafanya hivyo kwa maslahi ya kidunia. Kiongozi anapompa kitu huridhika na akinyimwa huvunjika moyo (na hawi muaminifu)." [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

Hadiyth – 29

وعن أبي هريرة رضي الله عنه ، عن النبيّ صلى الله عليه وسلم قال : (( بَيْنَ النَّفْخَتَيْنِ أرْبَعُونَ )) قالوا : يَا أبَا هُرَيْرَةَ أرْبَعُونَ يَوْماً ؟ قالَ : أبَيْتُ ، قَالُوا : أرْبَعُونَ سَنَةً ؟ قال : أبَيْتُ . قالُوا : أرْبَعُونَ شَهْراً ؟ قالَ : أبَيْتُ . (( وَيَبْلَى كُلُّ شَيْءٍ مِنَ الإنْسَانٍ إلاَّ عَجْبَ الذَّنَبِ ، فِيهِ يُرَكَّبُ الخَلْقُ ، ثُمَّ يُنَزِّلُ اللهُ مِنَ السَّمَاءِ مَاءً فَيَنْبُتُونَ كَمَا يَنْبُتُ البَقْلُ )) . متفق عليه .

Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Baina ya pulizo (baragumu) mbili ni arobaini." Wakauliza: "Ee Abu Huraiyrah! Je, ni siku arobaini?" Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) akasema: Sikujibu. Wakauliza: "Je, ni miaka arobaini?" Abu Hurayrah akasema: Sikujibu: Wakauliza tena: "Je, ni miezi arobaini?" Abu Huraiyrah akasema: Sikujibu. Kisha akasema: "Na kila kitu cha mwanadamu kitachakaa isipokuwa mfupa mmoja unaoitwa ‘ajbu-dhanab (kifandugu/kitokono), na kwayo ndio mwanadamu ataumbwa upya. Kisha Allaah Atateremsha maji kutoka mbinguni, na watu watamea (wataota) kama zinavyoota mboga." [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

Faida: ‘Ajbu-dhanab (kifandugu/kitokono) ni mfupa ambao upo mwisho wa uti wa mgongo au kifupa cha mkia.

 

Hadiyth – 30

وعن أبي هريرة رضي الله عنه ، قال : بَيْنَمَا النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم في مَجْلِسٍ يُحَدِّثُ القَومَ ، جَاءَ أَعْرَابِيٌّ فَقَالَ : مَتَى السَّاعَةُ ؟ فَمَضَى رسولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم يُحَدِّثُ ، فَقالَ بَعْضُ القَومِ : سَمِعَ مَا قَالَ فَكَرِهَ مَا قَالَ ، وَقَالَ بَعْضُهُمْ : بَلْ لَمْ يَسْمَعْ ، حَتَّى إذَا قَضَى حَدِيثَهُ قالَ : أيْنَ السَّائِلُ عَنِ السَّاعَةِ ؟ )) قال : هَا أنا يَا رسُولَ اللهِ . قال : (( إذَا ضُيِّعَتِ الأَمَانَةُ فَانْتَظِرِ السَّاعَةَ )) قال : كَيفَ إضَاعَتُهَا ؟ قال : (( إذَا وُسِّدَ الأَمْرُ إلى غَيْرِ أَهْلِهِ فَانْتَظِرِ السَّاعَةَ )) . رواه البخاري .

Amesema Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu): Alipokuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) anahotubia kikao cha watu, mara akaja Mbedui na kuuliza: "Qiyaamah kitakuwa lini?" Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akaendelea na mazungumzo yake. Hapo wakasema baadhi ya watu: "Amesikia alichoulizwa, lakini akachukia kukatizwa." Na wengine wakasema: "Bali hajasikia", mpaka alipomaliza mazungumzo yake, akasema: "Yu wapi muulizaji kuhusu Qiyaamah?" Akajibu: "Nipo hapa, ee Rasuli wa Allaah." Akasema: "Inapopotezwa amana (kukawa na hiyana) basi ngojeeni Qiyaamah." Akaulizwa: "Na itapotea vipi?" Akasema: "Pindi uongozi unapopatiwa watu wasio stahiki basi ngojeeni Qiyaamah." [Al-Bukhaariy]

 

 

Hadiyth – 31

وعن أبي هريرة رضي الله عنه : أنَّ رسُولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم قال : (( يُصَلُّونَ لَكُمْ، فَإنْ أصَابُوا فَلَكُمْ ، وإنْ أَخْطَئُوا فَلَكُمْ وَعَلَيْهِمْ )) . رواه البخاري .

Na imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Viongozi wenu watawaongoza nyinyi katika Swalaah, wakiwaongoza sawa hilo litawapatia nyinyi ujira (thawabu) na ikiwa watakosea basi nyinyi bado mtapat ujira na wao watakuwa na makosa (kwa hilo)." [Al-Bukhaariy]

 

Hadiyth – 32

وعن أبي هريرة رضي الله عنه : [ كُنْتُمْ خَيْرَ أمَّةٍ أُخْرِجَتْ لِلنَّاسِ ] [ البقرة : 110 ] قالَ : خَيْرُ النَّاسِ للنَّاسِ يَأتُونَ بِهِمْ في السَّلاسِلِ فِي أعْنَاقِهِمْ حَتَّى يَدْخُلُوا فِي الإسْلاَمِ .

Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba: "Mmekuwa ummah bora kabisa uliotolewa  (mfano) kwa watu" (Aal-'Imraan: 110), akasema: "Wabora wa watu kwa wanadamu ni wale wanaokuja nao wakiwa na silisila (minyororo) shingoni mwao mpaka wanaingia katika Uislamu." [Al-Bukhaariy]

 

Hadiyth – 33

وعن أبي هريرة رضي الله عنه ، عن النبيّ صلى الله عليه وسلم قال : (( عَجِبَ اللهُ عزوجل مِنْ قَومٍ يَدْخُلُونَ الجَنَّةَ فِي السَّلاسِلِ )) رواهما البخاري .

Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Allaah 'Azza wa Jalla Atawaridhia (na kufurahi) kwa kaumu itakayo ingia Peponi wakiwa na silsila (maana yake ni kuwa watafungwa na silsila, kisha watassilimu na kuingia Peponi)." [Al-Bukhaariy]

 

Hadiyth – 34

وعن أبي هريرة رضي الله عنه ، عن النبيّ صلى الله عليه وسلم قال : (( أَحَبُّ البِلادِ إلَى اللهِ مَسَاجِدُهَا ، وَأبْغَضُ البِلاَدِ إلَى اللهِ أسْوَاقُهَا )) . رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Sehemu zinazopendwa zaidi na Allaah ni Misikiti na sehemu zinazo chukiwa sana na Allaah ni masoko yake." [Muslim]

 

Hadiyth – 35

وعن سلمان الفارسي رضي الله عنه من قولهِ قال : لاَ تَكُونَنَّ إن اسْتَطَعْتَ أوَّلَ مَنْ يَدْخُلُ السُّوقَ ، وَلاَ آخِرَ مَنْ يَخْرُجُ مِنْهَا ، فَإنَّهَا مَعْرَكَةُ الشَّيْطَانِ ، وَبِهَا يَنْصبُ رَايَتَهُ . رواه مسلم هكذا .

ورواه البرقاني في صحيحهِ عن سلمان ، قال : قال رسولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم : (( لاَ تَكُنْ أَوَّلَ مَنْ يَدْخُلُ السُّوقَ ، وَلاَ آخِرَ مَنْ يَخْرُجُ مِنْهَا . فِيهَا بَاضَ الشَّيْطَانُ وَفَرَّخَ )) .

Katika kauli ya Salmaan Al-Faarisiy (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: "Ukiweza usiwe ni wa kwanza kuingia sokoni wala wa mwisho kutoka sokoni jitahidi kufanya hivyo kwani hapo ndio uwanja wa vita wa shetani na hapo ndipo anapoweka bendera yake." [Amepokea Muslim hivi]

Na amepokea Al-Barqaaniy katika Swahiyh yake kutoka kwa Salmaan Al-Faarisiy (Radhwiya Allaah 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Usiwe ni wa mwanzo kuingia sokoni wala wa mwisho kutoka katika sehemu hiyo, kwani hapo ndio shetani anataga mayai na ndipo yanapo anguliwa."

 

Hadiyth – 36

وعن عاصمٍ الأحوَلِ ، عن عبدِ اللهِ بن سَرْجِسَ رضي الله عنه قال : قلتُ لِرسولِ اللهِ صلى الله عليه وسلم : يا رسولَ اللهِ ، غَفَرَ اللهُ لَكَ ، قال : (( وَلَكَ )) . قال عاصمٌ : فَقُلْتُ لَهُ : أسْتَغْفرَ لَكَ رسُولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم ؟ قال : نَعَمْ وَلَكَ ، ثُمَّ تَلاَ هذِهِ الآية : [ وَاسْتَغْفِرْ لِذَنْبِكَ وَلِلمُؤْمِنِينَ وَالمُؤْمِنَاتِ ] [ محمد : 19 ] . رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwa 'Aaswim bin Al-Ahwal kutoka kwa 'Abdillaah bin Sarjis (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba nilimwambia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Ee Rasuli wa Allaah! Allaah Amekusamehe madhambi yako yote?" Akasema: "Na zako pia." Akasema 'Aaswim: "Nikamwambia yeye (yaani 'Abdillaah): "Je, Rasuli wa Allaa (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuombea maghfira?" Akasema: "Ndio na hata wewe pia umeombewa", kisha akasoma ayah hii: "Na omba Maghfira kwa dhambi zako na kwa ajili ya Waumini wa kiume na Waumini wa kike." [Muhammad: 19]. [Muslim]

 

Hadiyth – 37

وعن أبي مسعودٍ الأنصاري رضي الله عنه قال : قال النبيّ صلى الله عليه وسلم : (( إنَّ مِمَّا أَدْرَكَ النَّاسُ مِنْ كَلاَمِ النُّبُوَّةِ الأولَى : إذَا لَمْ تَسْتَحِ فَاصْنَعْ مَا شِئْتَ )) . رواه البخاري .

Imepokewa kutoka kwa Abu Mas'uwd Al-Answaariy kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Hakika katika maneno yaliyopatikana na watu kutokana na Manabiy ya kwanza ni: 'Ukitoona haya, basi fanya utakalo.' [Al-Bukhaariy]

 

Hadiyth – 38

وعن ابن مسعودٍ رضي الله عنه قال : قالَ رسُولُ الله صلى الله عليه وسلم : (( أوَّلُ مَا يُقْضَى بَيْنَ النَّاسِ يَوْمَ القِيَامَةِ فِي الدِّمَاء )) . متفق عليه .

Imepokewa kutoka kwa Ibn Mas'uwd (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Kitu cha kwanza kitakacho hukumiwa baina ya watu Siku ya Qiyaamah ni yale yaliyotokea baina yao duniani (madai ya umwagaji damu)." [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

Hadiyth – 39

وعن عائشة رضي الله عنها ، قالت : قال رسولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم : (( خُلِقَتِ المَلاَئِكَةُ مِنْ نُورٍ ، وَخُلِقَ الجَانُّ مِنْ مَارِجٍ من نَارٍ، وَخُلِقَ آدَمُ مِمَّا وُصِفَ لَكُمْ )) . رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwa 'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Malaaikah wameumbwa na nuru na majini wameumbwa kwa ulimi wa moto (kwa mchang'anyiko wa nyekundu na manjano na kijani) na Aadam ('Alayhis salaam) ameumbwa na kitu ambacho tayari mueambiwa." [Muslim]

 

Hadiyth – 40

وعن عائشة رضي الله عنها ، قالت : كان خُلُقُ نَبِيِّ اللهِ صلى الله عليه وسلم القُرْآن . رواهُ مسلم في جملة حديث طويل .

Amesema 'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa): Yalikuwa maadili ya Nabiy wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ni Qur-aan. [Muslim kutoka kwa Hadiyth ndefu]

 

Hadiyth – 41

ووعن عائشة رضي الله عنها ، قالت : قال رسُولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم : (( مَنْ أحَبَّ لِقَاءَ اللهِ أحَبَّ اللهُ لِقَاءهُ ، وَمَنْ كَرِهَ لِقَاءَ اللهِ كَرِهَ اللهُ لِقَاءهُ )) فقلتُ : يا رسولَ اللهِ ، أكَراهِيَةُ المَوتِ ، فَكُلُّنَا نَكْرَهُ المَوتَ ؟ قال : (( لَيْسَ كَذَلِكَ ، ولكِنَّ المُؤْمِنَ إذَا بُشِّرَ بِرَحْمَةِ اللهِ وَرِضْوَانِهِ وَجَنَّتِهِ أحَبَّ لِقَاءَ اللهِ فَأَحَبَّ اللهُ لِقَاءهُ ، وإنَّ الكَافِرَ إذَا بُشِّرَ بِعَذابِ اللهِ وَسَخَطهِ كَرِهَ لِقَاءَ اللهِ وكَرِهَ اللهُ لِقَاءهُ )) . رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwa 'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mwenye kupenda kukutana na Allaah, Allaah Anapenda kukutana naye; na mwenye kuchukia kukutana naye." Nikamuuliza: "Ee Rasuli wa Allaah! Je, hii inamaanisha kuchukia mauti? Hakika sote twachukia mauti." Akasema: "Sivyo hivyo, lakini Muumini pindi anapopatiwa bishara njema ya Rehema ya Allaah na kuridhika kwake na Pepo Yake hupenda kukutana na Allaah, hivyo Allaah Hupenda kukutana naye. Na hakika kafiri anapopatiwa bishara ya adhabu ya Allaah na Hasira Yake, anachukia kukutana na Allaah, hivyo Allaah kuchukia kukutana naye." [Muslim]

 

Hadiyth – 42

وَعَنْ أُمِّ المُؤْمِنِينَ صَفِيَّةَ بنتِ حُيَيٍّ رَضيَ اللهُ عَنها ، قالتْ : كان النبيُّ صلى الله عليه وسلم مُعْتَكِفاً ، فَأَتَيْتُهُ أزُورُهُ لَيْلاً ، فَحَدَّثْتُهُ ثُمَّ قُمْتُ لأَنْقَلِبَ فَقَامَ مَعِي لِيَقْلِبَنِي ، فَمَرَّ رَجُلاَنِ مِنَ الأنْصَارِ رضيَ اللهُ عَنهُما ، فَلَمَّا رَأَيَا النَّبيَّ صلى الله عليه وسلم أسْرَعَا . فقال صلى الله عليه وسلم : (( عَلَى رِسْلِكُمَا ، إنَّهَا صَفِيَّةُ بِنْتُ حُيَيٍّ )) فَقَالاَ : سُبْحانَ اللهِ يَا رسولَ اللهِ ، فقالَ : (( إنَّ الشَّيْطَانَ يَجْرِي مِنَ ابْنِ آدَمَ مَجْرَى الدَّمِ ، وَإنِّي خَشِيْتُ أَنْ يَقْذِفَ فِي قُلُوبِكُمَا شَرّاً - أَوْ قَالَ : شَيْئاً - )) . متفق عليه .

Amesema Mama wa Waumini, Swafiyyah bint Huyayy (Radhwiya Allaahu 'anhaa): Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa katika Itikafu Msikitini, nami nikaenda kumzuru usiku mmoja. Nilizunumza naye kwa muda, kisha nikasimama ili kurudi nyumbani kwangu, na Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasimama ili kunisindikiza. Mara wakapita watu wawili wa Ki-Answari (Radhwiya Allaahu 'anhumaa), na walipomuona Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) walianza kutembea haraka. Akasema Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Simameni (na nendeni taratibu), hakika huyu ni Swafiyyah bint Huyayy." Wakasema: "Ametakasika Allaah (na hana upungufu wa aina yoyote), ee Rasuli wa Allaah (hatuwezi kukufikiria baya)." Akasema: "Hakika shetani anatembea katika mwili wa mwanadamu kama vile mazunguko wa damu, nami nilihofia asitie fikira chafu za shari nyoyoni mwenu - ai alisema: Nimehofia asije akaingia ki tu katika akili zenu." [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

Hadiyth – 43

وعن أبي الفضل العباس بن عبد المطلب رضي الله عنه قال : شَهِدْتُ مَعَ رَسُولِ اللهِ صلى الله عليه وسلم يَومَ حُنَيْن ، فَلَزِمْتُ أنا وأبو سُفْيَانَ بن الحارثِ بن عبد المطلب رَسُول الله صلى الله عليه وسلم ، فَلَمْ نُفَارِقْهُ ، وَرسُولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم ، عَلَى بَغْلَةٍ لَهُ بَيْضَاءَ ، فَلَمَّا التَقَى المُسْلِمُونَ وَالمُشْرِكُونَ ، وَلَّى المُسْلِمُونَ مُدْبِريِنَ ، فَطَفِقَ رَسُولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم ، يَرْكُضُ بَغْلَتَهُ قِبلَ الكُفَّارِ ، وأنا آخِذٌ بِلِجَامِ بَغْلَةِ رَسُولِ اللهِ صلى الله عليه وسلم ، أكُفُّهَا إرَادَةَ أنْ لاَ تُسْرِعَ ، وأبُو سُفْيَانَ آخِذٌ بِرِكَابِ رَسُولِ اللهِ صلى الله عليه وسلم ، فقالَ رَسُولُ الله صلى الله عليه وسلم : (( أيْ عَبَّاسُ ، نَادِ أصْحَابَ السَّمُرَةِ )) . قالَ العَبَّاسُ - وَكَانَ رَجُلاً صَيِّتاً - فَقُلْتُ بِأَعْلَى صَوْتِي : أيْنَ أصْحَابُ السَّمُرَةِ ، فَوَاللهِ لَكَأنَّ عَطْفَتَهُمْ حِينَ سَمِعُوا صَوْتِي عَطْفَةُ البَقَرِ عَلَى أَوْلاَدِهَا ، فقالوا : يَا لَبَّيْكَ يَا لَبَّيْكَ ، فَاقْتَتَلُوا هُمْ وَالكُفَّارُ ، وَالدَّعْوَةُ في الأنْصَارِ يَقُولُونَ : يَا مَعْشَرَ الأَنْصَارِ ، يَا مَعْشَرَ الأنْصَارِ ، ثُمَّ قَصُرَتِ الدَّعْوَةُ عَلَى بَنِي الحَارِثِ بْنِ الخَزْرَجِ ، فَنَظَرَ رَسُولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم ، وَهُوَ عَلَى بَغْلَتِهِ كَالمُتَطَاوِلِ عَلَيْهَا إلَى قِتَالِهِمْ ، فَقَالَ : (( هَذَا حِينَ حَمِيَ الوَطِيسُ )) ، ثُمَّ أَخَذَ رَسُولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم ، حَصَيَاتٍ فَرَمَى بِهِنَّ وُجُوهَ الكُفَّارِ ، ثُمَّ قَالَ : (( انْهَزَمُوا وَرَبِّ مُحَمَّدٍ )) ، فَذَهَبْتُ أنْظُرُ فَإذَا القِتَالُ عَلَى هَيْئَتِهِ فِيما أرَى ، فَواللهِ مَا هُوَ إلاَّ أنْ رَمَاهُمْ بِحَصَيَاتِهِ ، فَمَا زِلْتُ أرَى حَدَّهُمْ كَلِيلاً وَأَمْرَهُمْ مُدْبِراً . رواه مسلم .

Amesema Abul-Fadhwl Al-'Abbaas bin 'Abdil-Muttwallib (Radhwiya Allaahu 'anhu): Nilishuhudia pamoja na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) Vita vya Hunayn. Mimi na Abu Sufyaan bin Al-Haarith bin 'Abdul-Muttwallib tulijilazimisha kuwa karibu na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah 'alayhi wa aalihi wa sallam) wala hatukuachana na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliyekuwa amempanda nyumbu mweupe. Walipokutana Waislamu na mushirikina katika vita hivyo Waislamu waligeuza migongo yao na kuanza kukimbia. Hata hivyo, Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alimtia chonjo nyumbu wake kuwakabili makafiri, nami nilikuwa nimeshika hatamu ya nyumbu wa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ili kumzuia asiende kwa kasi mno. Na Abu Sufyaan alikuwa amezishikilia zikuku (za kupandia) za mnyama huyo wa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam). Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) Akasema: Ee 'Abbaas! Waite Swahaaba wa Samurah (wala waliokuwepo katika Ahadi ya Ridhwaan - Baiah Ridhwaan)." Anasema 'Abbaas (Radhwiya Allaahu 'anhumaa): "Mimi nilikuwa na sauti kubwa. Nikawaita kwa sauti yangu ya juu kabisa: Wako wapi Swahaaba wa Samurah?" Naapa kwa Allaah! Walipoisikia sauti walikimbia haraka haraka kuja kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kama ng'ombe kuwakimbilia ndama wake. wakasema: "Tuko hapa, tuko hapa." Hapo hapo wakaanza kupigana na makafiri. Kwa wakati huo viongozi wa Answari wakaanza kuita: "Enyi kongamano la Answari." Kisha wakaita Bani Al-Haarith ibn Al-Khazraj. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alinyanyua kichwa chake kuangalia vita vinavyoendelea akiwa juu ya nyumbu wake. Akasema: "Hii ni pindi vita vinapo pamba moto na kufikia kilele." Kisha Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alichukua changarawe na kuvirusha kwenye nyuso za makafiri, kisha akasema: "Kwa Rabb wa Muhammad, wameshindwa." Baada ya muda nilikwenda kutizama hali ya vita ambavyo vilikuwa kama awali, lakini naapa kwa Allaah pindi Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliporusha zile changarawe nikaona ile harara na nguvu za makafiri zimepungua, hivyo kuanza kukimbia." [Muslim]

 

 

Hadiyth – 44

وعن أبي هريرة رضي الله عنه قال : قال رسولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم : (( أيُّهَا النَّاسُ ، إنَّ اللهَ طَيِّبٌ لاَ يَقْبَلُ إلاَّ طَيِّباً ، وإنَّ اللهَ أَمَرَ المُؤمِنِينَ بِمَا أَمَرَ بِهِ المُرْسَلِينَ . فقالَ تعالى :[ يَا أَيُّهَا الرُّسُلُ كُلُوا مِنَ الطَّيِّبَاتِ وَاعْمَلُوا صَالِحاً ] [ المؤمنون : 51 ] ، وقال تعالى : [ يَا أيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا كُلُوا مِنْ طَيِّبَاتِ مَا رَزَقْنَاكُمْ ] [ البقرة : 172 ] . ثُمَّ ذَكَرَ الرَّجُلَ يُطِيلُ السَّفَرَ أشْعثَ أغْبَرَ يَمُدُّ يَدَيْهِ إلَى السَّمَاءِ : يَا رَبِّ يَا رَبِّ ، وَمَطْعَمُهُ حَرَامٌ، وَمَشْرَبُهُ حَرَامٌ، ومَلبسُهُ حرامٌ ، وَغُذِّيَ بالْحَرَامِ ، فَأَنَّى يُسْتَجَابُ لِذَلِكَ ؟ رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Enyi watu! Hakika Allaah ni Mzuri Hakubali ila zuri. Na hakika Allaah Amewaamrisha Waumini yale Aliyowaamrisha Rusuli. Akasema Allaah Ta'aalaa: "Enyi Rusuli! Kuleni katika vizuri na tendeni wema." [Al-Muuminuwn: 51]. Na akasema tena Allaah Ta'aalaa: "Enyi walioamini! Kuleni vizuri tulivyo kuruzukunu." [Al-Baqarah: 172]. Kisha akamtaja mtu anayekwenda safari ndefu, nywele zake zimechafuka na kujaa vumbi ainua mikono yake mbinguni (akisema): 'Ee Rabb wangu! Ee Rabb wangu! Na ilhali chakula chake ni cha haramu, kinywaji chake ni cha haramu, kivazi chake ni cha haramu, na amelishwa haramu. Je, atatakabaliwaje kwa hayo anayoomba?' [Muslim]

 

Hadiyth – 45

وعن أبي هريرة رضي الله عنه ، قال : قال رسولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم : (( ثَلاَثَةٌ لاَ يُكَلِّمُهُمُ اللهُ يَوْمَ القِيَامَةِ ، وَلاَ يُزَكِّيهِمْ ، وَلاَ يَنْظُرُ إلَيْهِمْ ، وَلَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ : شَيْخٌ زَانٍ ، وَمَلِكٌ كَذَّابٌ ، وَعَائِلٌ مُسْتَكْبِرٌ )) . رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Watu watatu Allaah Hatozungumza nao Siku ya Qiyaamah wala Hatowatakasa wal Hatowaangalia: Mzee mzinifu, na mfalme mwongo na fakiri mwenye kiburi." [Muslim]

 

Hadiyth – 46

وعن أبي هريرة رضي الله عنه قال : قال رسولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم : (( سَيْحَانُ وَجَيْحَانُ وَالفُرَاتُ وَالنِّيلُ كُلٌّ مِنْ أَنْهَارِ الجَنَّةِ )) . رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Sayhaan (Jexartes), na Jayhaan (Oxus), na Furati (Euphrates) na Nile, ni miongoni mwa mito ya Jannah." [Muslim]

 

Hadiyth – 47

وعن أبي هريرة رضي الله عنه ، قال : أخَذَ رسُولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم بِيَدِي فَقَالَ : (( خَلَقَ اللهُ التُّرْبَةَ يَومَ السَّبْتِ ، وَخَلَقَ فيها الجِبَالَ يَومَ الأحَدِ ، وَخَلَقَ الشَّجَرَ يَومَ الإثْنَينِ ، وَخَلَقَ المَكْرُوهَ يَومَ الثُّلاَثَاءِ ، وَخَلَقَ النُّورَ يَوْمَ الأربِعَاءِ ، وَبَثَّ فِيهَا الدَّوابَّ يَومَ الخَمِيسِ ، وَخَلَقَ آدَمَ صلى الله عليه وسلم ، بَعْدَ العَصْرِ مِنْ يَومِ الجُمُعَةِ في آخِرِ الخَلْقِ فِي آخِرِ سَاعَةٍ مِنَ النَّهَارِ فِيمَا بَيْنَ العَصْرِ إِلَى اللَّيْلِ )) . رواه مسلم .

Amesema Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu): Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alinishika mkono na kuniambia: "Allaah Aliumba ardhi siku ya Jumamosi, na Akaumba ndani yake majabali Jumapili, na Akaumba miti Jumatatu, na Akaumba vitu vinavyo chukiza Jumanne, na Akaumba mwangaza Jumatano, na Akawatawanya wanyama katika ardhi siku ya Alkhamisi, na akamuumba Aadam ('Alayhis salaam) baada ya Alasiri katika siku ya Ijumaa katika viumbe Vyake vya mwisho katika saa ya mwisho ya mchana, baina ya Alasiri na usiku." [Muslim]

 

Hadiyth – 48

وعن أَبي سليمان خالد بن الوليد رضي الله عنه قَالَ : لَقَدِ انْقَطَعتْ في يَدِي يَوْمَ مُؤْتَةَ تِسْعَةُ أسْيَافٍ ، فَمَا بَقِيَ فِي يَدِي إِلاَّ صَفِيحَةٌ يَمَانِيَّةٌ . رواه البخاري .

Amesema Abu Sulaymaan Khaalid bin Al-Waliyd (Radhwiya Allaahu 'anhu): "Hakika katika Vita vya Mu'tah panga zangu tisa zilivunjika mkononi mwangu, na haukubakia mkononi mwangu ila upanga mdogo wa Ki-Yemeni." [Al-Bukhaariy]

 

Hadiyth – 49

وعن عمرو بن العاص رضي الله عنه : أنَّه سَمِعَ رسولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم ، يقولُ : (( إِذَا حَكَمَ الحَاكِمُ فَاجْتَهَدَ ، ثُمَّ أصَابَ ، فَلَهُ أجْرَانِ ، وَإِذَا حَكَمَ وَاجْتَهَدَ ، فَأَخْطَأَ ، فَلَهُ أَجْرٌ )) متفق عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwake 'Amruw bin Al-'Aas (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa alimsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: "Hakimu anapotoa hukumu akajitahidi kisha akaswibu (akapata) basi ana malipo mara mbili. Na anapohukumu akijitahidi kisha akakosea basi ana malipo mara moja." [Al-Bukhaariy na Muslim] 

 

Hadiyth – 50

وعن عائشة رَضِيَ اللهُ عنها : أنَّ النبيَّ صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( الحُمَّى مِنْ فَيْحِ جَهَنَّمَ فَأَبْرِدُوهَا بِالمَاءِ )) متفق عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwa 'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) kuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Homa inatokana na ukali wa mchemko wa Jahanam, kwa hiyo ipozeni kwa maji." [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

Hadiyth – 51

وعن عائشة رَضِيَ اللهُ عنها، عن النبيِّ صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( مَنْ مَاتَ وَعَلَيْهِ صَومٌ، صَامَ عَنْهُ وَلِيُّهُ )) متفق عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwa 'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Atakayefariki na hali imemuwajibikia kulipa baadhi ya funga alizokosa, basi mlezi (au warithi) wake atamlipia (kwa kumfungia siku alizokosa)." [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

Hadiyth – 52

وعن عوف بن مالِك بن الطُّفَيْلِ : أنَّ عائشة رَضِيَ اللهُ عنها ، حُدِّثَتْ أنَّ عبدَ اللهِ بن الزبير رضي الله عنهما ، قَالَ في بَيْعٍ أَوْ عَطَاءٍ أعْطَتْهُ عَائِشَةُ رَضِيَ اللهُ تَعَالَى عنها: واللهِ لَتَنْتَهِيَنَّ عَائِشَةُ أَوْ لأَحْجُرَنَّ عَلَيْهَا، قالَتْ : أَهُوَ قَالَ هَذَا ! قالوا : نَعَمْ . قَالَتْ : هُوَ للهِ عَلَيَّ نَذْرٌ أنْ لا أُكَلِّمَ ابْنَ الزُّبَيْرِ أَبَداً ، فَاسْتَشْفَعَ ابْنُ الزُّبَيْرِ إِلَيْهَا حِيْنَ طَالَتِ الهِجْرَةُ . فَقَالَتْ : لاَ ، واللهِ لاَ أشْفَعُ فِيهِ أبداً ، وَلاَ أَتَحَنَّثُ إِلَى نَذْرِي . فَلَمَّا طَالَ ذَلِكَ عَلَى ابْنِ الزُّبَيرِ كَلَّمَ المِسْوَرَ بْنَ مَخْرَمَةَ ، وَعبدَ الرحْمَانِ ابْنَ الأسْوَدِ بْنِ عَبْدِ يَغُوثَ وقَالَ لَهُمَا : أنْشُدُكُمَا اللهَ لَمَا أدْخَلْتُمَانِي عَلَى عَائِشَةَ رَضِيَ اللهُ عنها ، فَإنَّهَا لاَ يَحِلُّ لَهَا أنْ تَنْذِرَ قَطِيعَتِي ، فَأقْبَلَ بِهِ المِسْوَرُ ، وَعَبدُ الرحْمَانِ حَتَّى اسْتَأذَنَا عَلَى عَائِشَةَ فَقَالاَ : السَّلاَمُ عَلَيْكِ وَرَحْمَةُ اللهِ وَبَرَكَاتُهُ ، أنَدْخُلُ ؟ قالت عَائِشَةُ : ادْخُلُوا . قالوا : كُلُّنَا ؟ قالتْ : نَعَمْ ادْخُلُوا كُلُّكُمْ ، وَلاَ تَعْلَمُ أَنَّ معَهُمَا ابْنَ الزُّبَيرِ ، فَلَمَّا دَخَلُوا دَخَلَ ابْنُ الزُّبَيرِ الحِجَابَ فَاعْتَنَقَ عَائِشَةَ رَضِيَ اللهُ عنها ، وَطَفِقَ يُنَاشِدُهَا وَيَبْكِي ، وَطَفِقَ المِسْوَرُ ، وَعَبدُ الرَّحْمَانِ يُنَاشِدَانِهَا إِلاَّ كَلَّمَتْهُ وَقَبِلَتْ مِنْهُ ، وَيَقُولانِ : إنَّ النَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم نَهَى عَمَّا قَدْ عَلِمْتِ مِنَ الهِجْرَةِ ؛ وَلاَ يَحِلُّ لِمُسْلِمٍ أنْ يَهْجُرَ أَخَاهُ فَوقَ ثَلاَثِ لَيَالٍ ، فَلَمَّا أَكْثَرُوا عَلَى عَائِشَة مِنَ التَّذْكِرَةِ وَالتَّحْرِيجِ ، طَفِقَتْ تُذَكرُهُمَا وَتَبْكِي ، وَتَقُولُ : إنِّي نَذَرْتُ وَالنَّذْرُ شَدِيدٌ ، فَلَمْ يَزَالاَ بِهَا حَتَّى كَلَّمَتِ ابْنَ الزُّبَيرِ ، وأعْتَقَتْ فِي نَذْرِهَا ذَلِكَ أرْبَعِينَ رَقَبَةً ، وَكَانَتْ تَذْكُرُ نَذْرَهَا بَعدَ ذَلِكَ فَتَبكِي حَتَّى تَبِلَّ دُمُوعُهَا خِمَارَهَا . رواه البخاري .

Imepokewa kutoka kwa 'Awf bin Maalik bin Twufayl kuwa 'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhu) alielezewa kuwa 'Abdillaah bin Az-Zubayr (Radhwiya Allaahu 'anhu) alisema kuhusu mauzo au zawadi aliyompatia 'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) ambayo alizigawa kwa masikini, akasema: "Naapa kwa Allaah! Lau kama hatasitisha 'Aaishah kufanya hivyo, basi sitampelekea tena zawadi." Akauliza 'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa): "Je, yeye amesema hivyo?" Wakasema: "Ndio." Akasema: "Ninaapa kwa jina la Allaah kuwa sitazungumza na Ibn Az-Zubayr maisha yangu." Kipindi cha kutozungumza naye kilipokuwa kirefu, Ibn az-Zubayr alimtuma mtu kwenda kumuombea kwa 'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) lakini 'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) alikataa ombi hilo, akasema: "Hapana Wa-Allaahi! Sitakubali ombi lolote kwa niaba yake wala sitavunja nadhiri yangu." Kipindi cha kutozungumza naye kilipozidi zaidi, Ibn az-Zubayr alizungumza na Al-Miswar bin Makhramah na 'Abdir-Rahmaan bin al-Aswad bin 'Abdi Yaghuwth (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwa kuwaambia: "Nawataka nyinyi kwa jina la Allaah munichukue kwa 'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) kwani haifai kwake kuweka nadhiri ya kukata uhusiano nami." Wakamkubalia kwa hilo, Al-Miswar na 'Abdir-Rahmaan, walienda naye huku wamemfinika na mashuka yao mpaka wakafika kwa 'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) na kuomba idhini kwa kusema: "Assalaamu 'Alaiykum wa RahmatuLlaahi wa Barakaatuh, je, tuingie?" Akasema 'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa): "Ingieni." Wakasema: "Sote?" Akasema: "Ndio, ingieni nyote." Na hakujua kuwa Ibn za-Zubayr yuko pamoja nao. Pindi walipoingia, Ibn za- Zubayr aliingia moja kwa moja kwenye sitara ya 'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) na kumkumbatia halati yake, 'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa). Ibn az-Zubayr alianza kulia na kumnasihi amsamehe na Al-Muswar na 'Abdir-Rahmaan nao wakaingilia kati katika kumnasihi azungumze naye na amsamehe. Na wakamwambia: "Unahua ya kuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amekataza mtu kumhama mwenziwe, na haifai kwa Muislamu kumhama nduguye zaidi ya siku tatu." Walipo kithiri kumuomba na kumnasihi 'Aaishah, pia naye aliwakumbusha haki za ujamaa na huku analia na akasema: "Hakika mimi nimeweka nadhiri na kafara ya kuvunja nadhiri na kafara ya kuvunja nadhiri ni nzito na kali." Lakini waliendelea kumnasihi mpaka akazungumza na Ibn Az-Zubayr. Kama kafara ya kuvunja nadhiri, alilazimika kuacha huru watumwa arobaini. Na baada ya hapo kila alipokumbuka nadhiri yake alikuwa akilia mpaka kitambara chake cha kichwa kuloa machozi. [Al-Bukhaariy]

 

Hadiyth – 53

وعن عُقْبَةَ بن عامِرٍ رضي الله عنه : أنَّ رَسُولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم خَرَجَ إِلَى قَتْلَى أُحُدٍ ، فَصَلَّى عَلَيْهِمْ بَعْدَ ثَمَانِ سِنينَ كَالمُوَدِّعِ لِلأَحْيَاءِ وَالأَمْوَاتِ ، ثُمَّ طَلَعَ إِلَى المِنْبَرِ، فَقَالَ : (( إنِّي بَيْنَ أيْدِيكُمْ فَرَطٌ وَأَنَا شَهِيدٌ عَلَيْكُمْ وإنَّ مَوْعِدَكُمُ الحَوْضُ ، وإنِّي لأَنْظُرُ إِلَيْهِ مِنْ مَقَامِي هَذَا ، أَلاَ وإنِّي لَسْتُ أَخْشَى عَلَيْكُمْ أنْ تُشْرِكُوا ، وَلَكِنْ أخْشَى عَلَيْكُمُ الدُّنْيَا أنْ تَنَافَسُوهَا )) قَالَ : فَكَانَتْ آخِرَ نَظْرَةٍ نَظَرْتُهَا إِلَى رَسُولِ اللهِ صلى الله عليه وسلم . متفق عَلَيْهِ .

وفي رواية : (( وَلَكِنِّي أَخْشَى عَلَيْكُمُ الدُّنْيَا أنْ تَنَافَسُوا فِيهَا ، وَتَقْتَتِلُوا فَتَهْلِكُوا كما هَلَكَ مَنْ كَانَ قَبْلَكُمْ )) . قَالَ عُقْبَةُ : فكانَ آخِرَ مَا رَأيْتُ رَسُولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم عَلَى المِنْبَرِ .

وفي روايةٍ قَالَ : (( إنِّي فَرَطٌ لَكُمْ وَأنَا شَهِيدٌ عَلَيْكُمْ وإنِّي واللهِ لأَنْظُرُ إِلَى حَوْضِي الآنَ، وإنِّي أُعْطِيتُ مَفَاتِيحَ خَزَائِنِ الأَرْضِ، أَوْ مَفَاتِيحَ الأرْضِ، وإنِّي واللهِ مَا أخَافُ عَلَيْكُمْ أنْ تُشْرِكُوا بَعْدِي، وَلَكِنْ أَخَافُ عَلَيْكُمْ أَنْ تَنَافَسُوا فِيهَا )) .

وَالمُرَادُ بِالصَّلاَةِ عَلَى قَتْلَى أُحُدٍ : الدُّعَاءُ لَهُمْ ، لاَ الصَّلاَةُ المَعْرُوفَةُ .

Imepokewa kutoka kwa 'Uqbah bin 'Aamir (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliwaswalia waliouwawa Uhud, akawaswalia baada ya kupita miaka minane, kama vile ni mwenye kuaga walio hai na wafu, kisha akapanda juu ya mimbar akasema: "Hakika mimi ni mwenye kukutangulieni mbele yenu, nami ni shahidi kwenu, na ahadi yenu ya kukutana ni kwenye Hawdh (birika), nami ninaiona hapa nilipo; na mimi siwahofii kuwa mtakuwa mushirikina lakini ninawahofia maisha ya dunia yatawaghurisha, na mtaishindania." [Al-Bukhaariy na Muslim]

Na katika riwaayah nyengine: "Lakini ninawahofia maisha ya dunia yatawaghurisha, na mtashindana kwayo na mtaanza kupigana wenyewe kwa wenyewe na hivyo kuangamia kama walivyoangamia waliokuwa kabla yenu." akasema 'Uqbah (Radhwiya Allaahu 'anhu): "Hiyo ndiyo mara yangu ya mwisho kumuona Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) juu ya mimbar." 

Na katika riwaayah nyengine amesema: "Hakika mimi nitawatangulieni mbele yenu, nami ni shahidi kwenu, na hakika Wa-Allaahi, naona Hawdh sasa hivi. Na hakika nimepatiwa funguo za hazina ya ardhi au funguo za ardhi. Na hakika Wa-Allaahi siwahofii kuwa mutarudi katika ushirikina baada yangu lakini nawahofia kushindana kwenu ndani yake." Na muradi (maana) ya kuwaswalia waliouwawa Uhud ni kuwaombea dua na wala sio Swalaah inayojulikana.

 

Hadiyth – 54

وعن أَبي زيد عمرِو بن أخْطَبَ الأنصاريِّ رضي الله عنه قَالَ : صلَّى بِنَا رَسُولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم الفَجْرَ ، وَصَعِدَ المِنْبَرَ ، فَخَطَبَنَا حَتَّى حَضَرَتِ الظُّهْرُ ، فَنَزَلَ فَصَلَّى ، ثُمَّ صَعِدَ المِنْبَرَ فَخَطَبَنَا حَتَّى حَضَرَتِ العَصْرُ ، ثُمَّ نَزَلَ فَصَلَّى ، ثُمَّ صَعِدَ المِنْبَرَ فَخَطَبَنَا حَتَّى غَرَبَتِ الشَّمْسُ ، فَأَخْبَرَنَا بِمَا كَانَ وَبِمَا هُوَ كَائِنٌ ، فَأَعْلَمُنَا أَحْفَظُنَا . رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwa Abu Zayd 'Amruw bin Akhtab Al-Answaariyy (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alituswalisha Swalaah ya Alfajiri na baadae akapanda mimbar, akatuhutubia mpaka ikafika Adhuhuri. Hapo aliteremka na kutuswalisha, kisha akapanda tena mimbar na kuendelea na houtba yake mpaka Alasiri, kisha akateremka na kutuswalisha. Baada ya hapo alipanda tena mimbar akatuhutubia mpaka kuzama jua katika hotuba yake hiyo alitufahamisha vitu ambavyo tayari vimepita na pia vile vitakavyokuja (kutokea baadae). Hivyo, wale wajuzi miongoni mwetu ni wale walio hifadhi vitu hivyo." [Muslim]

 

Hadiyth – 55

وعن عائشة رَضِيَ اللهُ عنها ، قالت : قَالَ النَّبيُّ صلى الله عليه وسلم : (( مَنْ نَذَرَ أنْ يُطِيعَ اللهَ فَلْيُطِعْهُ ، وَمَنْ نَذَرَ أَنْ يَعْصِيَ اللهَ فَلاَ يَعْصِهِ )) . رواه البخاري .

Imepokewa kutoka kwa 'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mwenye kuweka nadhiri ya kumtii Allaah, basi amtii. Na mwenye kuweka nadhiri ya kumuasi Allaah, basi asimuasi (asifanye hivo)." [Al-Bukhaariy]

 

Hadiyth – 56

وعن أمِّ شَرِيكٍ رَضِيَ اللهُ عنها : أنَّ رسولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم أمرها بِقَتْلِ الأَوْزَاغِ وقال : (( كَانَ يَنْفُخُ عَلَى إبْرَاهِيمَ )) متفق عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwa Ummu Shariyk (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alimuamuru kuua mijusi, na akasema: "Alikuwa akipuliza (moto uliowashwa ili kumchoma) Ibraahiym ('Alayhis salaam)." [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

Hadiyth – 57

وعن أَبي هريرة رَضِيَ اللهُ عنه قَالَ : قَالَ رسولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم : (( مَنْ قَتَلَ وَزَغَةً فِي أَوَّلِ ضَرْبَةٍ فَلَهُ كَذَا وَكَذَا حَسَنَةً ، وَمَنْ قَتَلَهَا في الضَّرْبَةِ الثَّانِيَةِ فَلَهُ كَذَا وَكَذَا حَسَنَةً دُونَ الأولَى ، وَإنْ قَتَلَهَا فِي الضَّرْبَةِ الثَّالِثَةِ فَلَهُ كَذَا وَكَذَا حَسَنَةً )) .

وفي رواية : (( مَنْ قَتَلَ وَزَغَاً في أَوَّلِ ضَرْبَةٍ كُتِبَ لَهُ مِئَةُ حَسَنَةٍ ، وفي الثَّانِيَةِ دُونَ ذَلِكَ ، وفي الثَّالِثَةِ دُونَ ذَلِكَ )) . رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mwenye kuua mjusi kwa dhoruba (pigo) ya kwanza, atakuwa na hasanati kadhaa na kadhaa na mwenye kumuua kwa pigo la pili, atakuwa na hasanati kadhaa na kadhaa chini ya ile ya kwanza; na atakayemuua kwa dhoruba ya tatu, atakuwa na hasanati kadhaa na kadhaa." 

Na katika riwaayah nyengine: "Mwenye kumuua mjusi kwa dhoruba ya kwanza ataandikiwa hasanati mia, na kwa dhoruba ya pili ataandikiwa chini ya hizo za mwanzo (kidogo kuliko mia) na katika ya tatu chini ya hiyo (ya pili)." [Muslim]. Wamesema watu wa lugha: Al-Wazagh ni mdudu mkubwa mwenye kuudhi.

 

Hadiyth – 58

وعن أَبي هريرة رَضِيَ اللهُ عنه أنَّ رَسُول اللهِ صلى الله عليه وسلم قَالَ : (( قَالَ رَجُلٌ لأَتَصَدَّقَنَّ بِصَدَقَةٍ ، فَخَرَجَ بِصَدَقَتِهِ فَوَضَعَهَا فِي يَدِ سَارِقٍ ، فَأَصْبَحُوا يَتَحَدَّثُونَ : تُصُدِّقَ عَلَى سَارِقٍ ! فَقَالَ : اللَّهُمَّ لَكَ الحَمْدُ لأتَصَدَّقَنَّ بِصَدَقَةٍ ، فَخَرَجَ بِصَدَقَتِهِ فَوَضَعَهَا في يَدِ زَانِيَةٍ ؛ فَأصْبَحُوا يَتَحَدَّثُونَ : تُصُدِّقَ اللَّيْلَةَ عَلَى زَانِيَةٍ ! فَقَالَ : اللَّهُمَّ لَكَ الحَمْدُ عَلَى زَانِيَةٍ ! لأتَصَدَّقَنَّ بِصَدَقَةٍ ، فَخَرَجَ بِصَدَقَتِهِ فوَضَعَهَا في يَدِ غَنِيٍّ ، فَأَصْبَحُوا يَتَحَدَّثُونَ : تُصُدِّقَ عَلَى غَنِيٍّ ؟ فَقَالَ : اللَّهُمَّ لَكَ الحَمْدُ عَلَى سَارِقٍ وَعَلَى زَانِيَةٍ وعلى غَنِيٍّ ! فَأُتِيَ فقيل لَهُ : أمَّا صَدَقَتُكَ عَلَى سارقٍ فَلَعَلَّهُ أنْ يَسْتَعِفَّ عَنْ سَرِقَتِهِ ، وأمَّا الزَّانِيَةُ فَلَعَلَّهَا تَسْتَعِفُّ عَنْ زِنَاهَا ، وأمَّا الغَنِيُّ فَلَعَلَّهُ أَنْ يَعْتَبِرَ فَيُنْفِقَ مِمَّا أَعْطَاهُ اللهُ )) . رواه البخاري بلفظه ومسلم بمعناه .

Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa salla) amesema: "Mtu Fulani alisema Wa-Allaahi nitatoa Swadaqah na akatoka na Swadaqah yake akampa mwizi. Asubuhi yake watu wakawa wanazungumza, 'Mwizi kapewa Swadaqah.' Mtu yule akasema: 'Ee Rabb wangu! Kila sifa njema Wewe Ndiye Unayestahiki, Wa-Allaahi, nitatoa Swadaqah." Basi akatoka na Swadaqah yake , akampa mzinifu (bila kujua). Asubuhi yake watu wakawa wanasema: 'Usiku wa leo mwanamke Malaya amepewa Swadaqah.' Mtu yule akasema: 'Ee Rabb wangu! kila sifa njema Ndiye Wewe Unayestahiki, nimempa Swadaqah mwanamke mzinifu, Wa-Allaahi, nitatoa Swadaqah.' Basi akatoka na Swadaqah yake, akampa tajiri (bila kujua). Asubuhi yake watu wakawa wanasema: 'Tajiri amepewa Swadaqah.' akasema: 'Ee Rabb wangu! Kila sifa njema Wewe Ndiye Unayestahiki, nimetoa Swadaqah kwa mwizi, mzinifu na tajiri.' Akajiwa na mtu (katika usingizi) akaelezwa: 'Ama Swadaqah yako kwa mwizi huenda ikamzuia kuiba, ama mzinifu akaacha uzinifu wake na ama tajiri huenda atapata fundisho akatoa baadhi ya mali yake kwa ajili ya Allaah.' [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

Hadiyth – 59

وعن أَبي هريرة رَضِيَ اللهُ عنه ، قَالَ : كنَّا مَعَ رَسُولِ اللهِ صلى الله عليه وسلم في دَعْوَةٍ ، فَرُفِعَ إِلَيْهِ الذِّرَاعُ ، وَكَانَتْ تُعْجِبُهُ ، فَنَهَسَ مِنْهَا نَهْسَةً وقال : (( أنا سَيِّدُ النَّاسِ يَوْمَ القِيَامَةِ ، هَلْ تَدْرُونَ مِمَّ ذَاكَ ؟ يَجْمَعُ اللهُ الأوَّلِينَ وَالآخِرِينَ في صَعِيدٍ وَاحِدٍ، فَيُبْصِرُهُمُ النَّاظِرُ، وَيُسْمِعُهُمُ الدَّاعِي ، وَتَدْنُو مِنْهُمُ الشَّمْسُ ، فَيَبْلُغُ النَّاس مِنَ الغَمِّ وَالكَرْبِ مَا لاَ يُطِيقُونَ وَلاَ يَحْتَمِلُونَ ، فَيقُولُ النَّاسُ : أَلاَّ تَرَوْنَ مَا أنْتُمْ فِيهِ إِلَى مَا بَلَغَكُمْ ، ألاَ تَنْظُرُونَ مَنْ يَشْفَعُ لَكُمْ إِلَى رَبِّكُمْ ؟ فَيقُولُ بَعْضُ النَّاسِ لِبَعْضٍ : أبُوكُمْ آدَمُ ، فَيَأتُونَهُ فَيقُولُونَ : يَا آدَمُ أنْتَ أَبُو البَشَرِ، خَلَقَكَ اللهُ بِيَدِهِ، وَنَفَخَ فِيكَ مِنْ رُوحِهِ، وأمَرَ المَلاَئِكَةَ فَسَجَدُوا لَكَ ، وأسْكَنَكَ الجَنَّةَ ، ألاَ تَشْفَعُ لَنَا إِلَى رَبِّكَ ؟ ألاَ تَرَى إِلَى مَا نَحْنُ فِيهِ وَمَا بَلَغْنَا ؟ فَقَالَ : إنَّ رَبِّي غَضِبَ اليَوْمَ غَضَباً لَمْ يَغْضَبْ قَبْلَهُ مِثْلَهُ ، وَلا يَغْضَبُ بَعْدَهُ مِثْلَهُ ، وَإنَّهُ نَهَانِي عَنِ الشَّجَرَةِ فَعَصَيْتُ ، نَفْسِي نَفْسِي نَفْسِي ، اذْهَبُوا إِلَى غَيْرِي ، اذْهَبُوا إِلَى نُوحٍ ، فَيَأتُونَ نوحاً فَيَقُولُونَ : يَا نُوحُ ، أنْتَ أوَّلُ الرُّسُلِ إِلَى أهلِ الأرْضِ ، وَقَدْ سَمَّاكَ اللهُ عَبْداً شَكُوراً ، ألاَ تَرَى إِلَى مَا نَحْنُ فِيهِ ، ألاَ تَرَى إِلَى مَا بَلَغْنَا ، ألاَ تَشْفَعُ لَنَا إِلَى رَبِّكَ ؟ فَيقُولُ : إنَّ رَبِّي غَضِبَ اليَوْمَ غَضَباً لَمْ يَغْضَبْ قَبْلَهُ مِثْلَهُ ، وَلَنْ يَغْضَبَ بَعْدَهُ مِثْلَهُ ، وَإنَّهُ قَدْ كَانَتْ لِي دَعْوَةٌ دَعَوْتُ بِهَا عَلَى قَوْمِي، نَفْسِي نَفْسِي نَفْسِي ، اذْهَبُوا إِلَى غَيْرِي ، اذْهَبُوا إِلَى إبْرَاهِيمَ ، فَيَأتُونَ إبْرَاهِيمَ فَيقُولُونَ : يَا إبْرَاهِيمُ ، أنْتَ نَبِيُّ اللهِ وَخَلِيلُهُ مِنْ أهْلِ الأرْضِ ، اشْفَعْ لَنَا إِلَى رَبِّكَ، ألاَ تَرَى إِلَى مَا نَحْنُ فِيهِ ؟ فَيقُولُ لَهُمْ : إنَّ رَبِّي قَدْ غَضِبَ اليَوْمَ غَضَباً لَمْ يَغْضَبْ قَبْلَهُ مِثْلَهُ ، وَلَنْ يَغْضَبَ بَعْدَهُ مِثْلَهُ ، وَإنَّي كُنْتُ كَذَبْتُ ثَلاثَ كَذبَاتٍ ؛ نَفْسِي نَفْسِي نَفْسِي ، اذْهَبُوا إِلَى غَيْرِي ، اذْهَبُوا إِلَى مُوسَى ، فَيَأتُونَ مُوسَى فَيقُولُونَ : يَا مُوسَى أنَتَ رَسُولُ اللهِ ، فَضَّلَكَ اللهُ بِرسَالاَتِهِ وَبِكَلاَمِهِ عَلَى النَّاسِ ، اشْفَعْ لَنَا إِلَى رَبِّكَ ، ألاَ تَرَى إِلَى مَا نَحْنُ فِيهِ ؟ فيقُولُ : إنَّ رَبِّي قَدْ غَضِبَ اليَوْمَ غَضَباً لَمْ يَغْضَبْ قَبْلَهُ مِثْلَهُ ، وَلَنْ يَغْضَبَ بَعْدَهُ مِثْلَهُ ، وَإنَّي قَدْ قَتَلْتُ نَفْساً لَمْ أُومَرْ بِقَتْلِهَا ، نَفْسِي نَفْسِي نَفْسِي ، اذْهَبُوا إِلَى غَيْرِي ؛ اذْهَبُوا إِلَى عِيسَى . فَيَأتُونَ عِيسَى فَيَقُولُونَ : يَا عِيسَى ، أنْتَ رَسُولُ الله وَكَلِمَتُهُ ألْقَاهَا إِلَى مَرْيَمَ وَرُوحٌ مِنْهُ ، وَكَلَّمْتَ النَّاسَ في المَهْدِ ، اشْفَعْ لَنَا إِلَى رَبِّكَ ، ألاَ تَرَى إِلَى مَا نَحْنُ فِيهِ ؟ فيَقُولُ عِيسَى: إنَّ رَبِّي قَدْ غَضِبَ اليَوْمَ غَضَباً لَمْ يَغْضَبْ قَبْلَهُ مِثْلَهُ، وَلَنْ يَغْضَبَ بَعْدَهُ مِثْلَهُ، وَلَمْ يَذْكُرْ ذَنْباً، نَفْسِي نَفْسِي نَفْسِي ، اذْهَبُوا إِلَى غَيْرِي ، اذْهَبُوا إِلَى مُحَمَّدٍ صلى الله عليه وسلم )) .

وفي روايةٍ : (( فَيَأتُونِي فَيَقُولُونَ : يَا مُحَمَّدُ أنتَ رَسُولُ اللهِ وخَاتَمُ الأنْبِياءِ ، وَقَدْ غَفَرَ اللهُ لَكَ مَا تَقَدَّمَ مِنْ ذَنْبِكَ وَمَا تَأَخَّرَ ، اشْفَعْ لَنَا إِلَى رَبِّكَ ، ألاَ تَرَى إِلَى مَا نَحْنُ فِيهِ ؟ فَأنْطَلِقُ فَآتِي تَحْتَ العَرْشِ فَأَقَعُ سَاجِداً لِرَبِّي ، ثُمَّ يَفْتَحُ اللهُ عَلَيَّ مِنْ مَحَامِدِهِ ، وَحُسْنِ الثَّنَاءِ عَلَيْهِ شَيْئاً لَمْ يَفْتَحْهُ عَلَى أحَدٍ قَبْلِي ، ثُمَّ يُقَالُ : يَا مُحَمَّدُ ارْفَعْ رَأسَكَ ، سَلْ تُعْطَهُ ، وَاشْفَعْ تُشَفَّعْ ، فَأرْفَعُ رَأْسِي ، فَأقُولُ : أُمَّتِي يَا رَبِّ ، أُمَّتِي يَا رَبِّ ، أُمَّتِي يَا رَبِّ ، فَيُقَالُ : يَا مُحَمَّدُ أدْخِلْ مِنْ أُمَّتِكَ مَنْ لاَ حِسَابَ عَلَيْهِمْ مِنَ البَابِ الأيْمَنِ مِنْ أَبْوَابِ الجَنَّةِ ، وَهُمْ شُرَكَاءُ النَّاسِ فِيمَا سِوَى ذَلِكَ مِنَ الأبْوَابِ )) . ثُمَّ قَالَ : (( وَالَّذِي نَفْسِي بِيَدِهِ ، إنَّ مَا بَيْنَ المِصْرَاعَيْنِ مِنْ مَصَارِيعِ الجَنَّةِ كَمَا بَيْنَ مَكَّةَ وَهَجَرَ ، أَوْ كَمَا بَيْنَ مَكَّةَ وَبُصْرَى )) . متفق عَلَيْهِ .

Amesema Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu): Tulikuwa pamoja na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalhi wa sallam) katika karamu, akaletewa nyama iliyopikwa, akapewa mkono na ilikuwa ni nyama inayompendeza zaidi, akaiuma kwa ncha ya meno mara moja, kisha akasema: "Mimi ndiye Bwana wa watu Siku ya Qiyaamah, je mnaelewa kwa nini hivyo?" Watu wa mwanzo na wa mwisho watakusanywa katika wanja mmoja, anawasikilizisha Mnadi. Jua litawakaribia sana na itawafikia watu watasema: "Hivi hamuoni hali iliyowafikia? Kwa nini hamtafuti, atakaye waombea shafa'a kwa Rabb wenu?" Watu wataelezana wao kwa wao: "Nendeni kwa baba yenu, Aadam ('Alayhis salaam)." Watamwendea Aadam ('Alayhis salaam) na watamwambia: "Wewe ndiwe baba wa wana-Aadam, Allaah Amekuumba kwa Mkono Wake, Akakupulizia roho (ambayo Aliiumba) na Akawaamuru Malaaikah wakakusujudia na Akakueka Peponi tutakie shafa'a kwa Rabb Wako, huoni hali tuliyo nayo? Hupaoni tulipofikia?" Aadam ('Alayhis salaam) atasema: "Hakika Rabb Wangu leo Amekasirika sana, Hakupata kukasirika kabla ya leo kama hivyo na Hatokasirika baada yake kama hivyo, na kwa hakika Alinikataza mti nami nikamuasi, nafsi yangu. Nendeni kwa mwengine, nendeni kwa Nuwh ('Alayhis salaam)." Wataenda kwa Nuwh ('Alayhis salaam) na watamwambia: "Ee Nuwh! Wewe ndiye Rasuli wa kwanza ardhini. Na hakika Allaah Amekuita mja mwingi wa kushukuru, huoni hali tuliyo nayo? Hupaoni tulipofika? Je, hutuombei shafa'a kwa Rabb Wako?" Atasema: "Hakika Rabb Wangu leo Amekasirika sana, Hakupata kukasirika kabla ya leo kama hivyo na Hatokasirika baada yake kama hivyo, na kwa hakika nilikuwa na haki ya kuomba (nilipokuwa duniani) na nikaomba dhidi ya Ummah wangu, nafsi yangu, nafsi yangu, nafsi yangu. Nendeni kwa mwengine, nendeni kwa Ibraahiym ('Alayhis salaam)." Wataenda kwa Ibraahiym ('Alayhis salaam) na watasema: "Ee Ibraahiym! Wewe ni Rasuli wa Allaah na mpezi Wake katika watu wa ardhi, tuombee shafa'a kwa Rabb Wako, kwani huioni hali tuliyo nayo?" Atawaambia: "Hakika Rabb Wangu leo Amekasirika sana, Hakupata kukasirika kabla ya leo kama hivyo na Hatokasirika baada yake kama hivyo, nami nimeongopa mara tatu, nafsi yangu, nafsi yangu, nafsi yangu. Nendeni kwa mwengine, nendeni kwa Muwsaa ('Alayhis salaam)." Watamwendea Muwsaa ('Alayhis salaam) na watamwambia: "Wewe ni Rasuli wa Allaah. Allaah Amekuboresha kwa Urasuli Wake na Maneno Yake juu ya watu, tuombee shafa'a kwa Rabb Wako, kwani hauioni hali tuliyo nayo?" Atasema: "Hakika Rabb Wangu leo Amekasirika sana, Hakupata kukasirika kabla ya leo kama hivyo na Hatokasirika baada yake kama hivyo, nami nimeua nafsi ambayo sikuamrishwa kuiua, nafsi yangu, nafsi yangu, nafsi yangu. Nendeni kwa mwengine, nendeni kwa 'Iysaa." Watamwendea 'Iysaa ('Alayhis salaam) na watamwambia: "Ee 'Iysaa, wewe ni Rasuli wa Allaah na Neno Lake (Kuwa! -na akawa) Alilolitoa kwa Maryam na ni roho Aliyoiumba (Allaah), na umezungumza na watu ukiwa mbelekoni, umdogo, tuombee shafa'a kwani hauoni hali tuliyo nayo?" Na 'Iysaa ('Alayhis salaam) atasema: "Hakika Rabb Wangu leo Amekasirika sana, Hakupata kukasirika kabla ya leo kama hivyo na Hatokasirika baada yake kama hivyo, na hakutaja dhambi, nafsi yangu, nafsi yangu, nafsi yangu. Nendeni kwa mwengine, nendeni kwa Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)." 

Na katika riwaayah nyengine: Watamwendea watamwambia: "Ee Muhammad, wewe ni Rasuli wa Allaah na Mwisho wa Manabiy. Allaah Amekusamehe madhambi yako yaliyopita na yajayo, tuombee shafa'a kwa Rabb Wako, kwani huoni hali tuliyo nayo?" Nitatoka kwenda chini ya Arshi, nitaanguka kwa kusujudu kwa Rabb Wangu. Kisha Allaah Atanifungulia Sifa Zake na Sifa Yake Nzuri kwa kiwango ambacho Hakupata kumfungulia mwengine kabla yangu. Kisha itasemwa: "Ee Muhammad! Inua kichwa chako, omba utapewa." Hapo nitainua kichwa changu na nitasema: "Ee Rabb Wangu, Ummah wangu! Ee Rabb Wangu, Ummah wangu! Itasema: "Ee Muhammad! Waingize katika umati wako wasiohesabiwa mlango wa kuume katika milango ya pepo, nao wanashirikiana na watu katika isiyokuwa hiyo miongoni mwa milango." Kisha atasema: "Naapa kwa Ambaye nafsi yangu iko Mikononi Mwake, hakika umbali kati ya pande mbili za nguzo za lango la Peponi ni kama umbali wa kutokea Makkah na Hajar (ni mji mkubwa ambao uko Bahrayn) au kama umabli wa kutoka Makkah kwenda Buswraa (ni mji unaojulikana ambao ni umbali wa masafa wa siku tatu mpaka Damascus. Unaujulikana kwa jina la Basra uliopo 'Iraaq)." [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

Hadiyth – 60

وعن ابن عباس رضي الله عنهما، قَالَ: جَاءَ إبراهيم صلى الله عليه وسلم بِأُمِّ إسْماعِيلَ وَبِابْنِهَا إسْمَاعِيل وَهِيَ تُرْضِعُهُ ، حَتَّى وَضَعهَا عِنْدَ البَيْتِ ، عِنْدَ دَوْحَةٍ فَوقَ زَمْزَمَ في أعْلَى المَسْجِدِ، وَلَيْسَ بِمَكَّةَ  يَوْمَئِذٍ أَحَدٌ ، وَلَيْسَ بِهَا مَاءٌ ، فَوَضَعَهُمَا هُنَاكَ ، وَوَضَعَ عِنْدَهُمَا جِرَاباً فِيهِ تَمْرٌ ، وَسِقَاءً فِيهِ مَاءٌ ، ثُمَّ قَفَّى إبْرَاهِيمُ مُنْطَلِقاً ، فَتَبِعَتْهُ أمُّ إسْمَاعِيلَ فَقَالَتْ : يَا إبْرَاهِيمُ ، أَيْنَ تَذْهَبُ وَتَتْرُكُنَا بِهذَا الوَادِي الَّذِي لَيْسَ فِيهِ أنِيسٌ وَلاَ شَيْءٌ ؟ فَقَالَتْ لَهُ ذَلِكَ مِرَاراً ، وَجَعَلَ لاَ يَلْتَفِتُ إِلَيْهَا ، قَالَتْ لَهُ : آللهُ أَمَرَكَ بِهَذَا ؟ قَالَ : نَعَمْ ، قَالَتْ : إذاً لاَ يُضَيِّعُنَا ؛ ثُمَّ رَجَعَتْ ، فَانْطَلَقَ إِبْرَاهِيمُ صلى الله عليه وسلم ، حَتَّى إِذَا كَانَ عِنْدَ الثَّنِيَّةِ حَيْثُ لاَ يَرُونَهُ ، اسْتَقْبَلَ بِوَجْهِهِ البَيْتَ ، ثُمَّ دَعَا بِهؤُلاءِ الدَّعَوَاتِ ، فَرَفَعَ يَدَيْهِ فَقَالَ : [ رَبِّ إنِّي أَسْكَنْتُ مِنْ ذُرِّيَّتِي بِوَادٍ غَيْرِ ذِي زَرْعٍ عِندَ بَيْتِكَ الْمُحَرَّمِ رَبَّنَا لِيُقِيمُوا الصَّلَاةَ فَاجْعَلْ أَفْئِدَةً مِّنَ النَّاسِ تَهْوِي إِلَيْهِمْ وَارْزُقْهُم مِّنَ الثَّمَرَاتِ لَعَلَّهُمْ يَشْكُرُونَ ﴿٣٧﴾ ]  [ إبراهيم : 37 ] . وَجَعَلَتْ أُمُّ إسْمَاعِيلَ تُرْضِعُ إسْمَاعِيلَ وَتَشْرَبُ مِنْ ذَلِكَ المَاءِ ، حَتَّى إِذَا نَفِدَ مَا فِي السِّقَاءِ عَطِشَتْ ، وَعَطِشَ ابْنُهَا ، وَجَعَلتْ تَنْظُرُ إِلَيْهِ يَتَلَوَّى - أَوْ قَالَ يَتَلَبَّطُ - فَانْطَلَقَتْ كَرَاهِيَةَ أنْ تَنْظُرَ إِلَيْهِ ، فَوَجَدَتِ الصَّفَا أَقْرَبَ جَبَلٍ في الأرْضِ يَلِيهَا ، فَقَامَتْ عَلَيْهِ ، ثُمَّ اسْتَقْبَلَتِ الوَادِي تَنْظُرُ هَلْ تَرَى أحَداً ؟ فَلَمْ تَرَ أحَداً . فَهَبَطَتْ مِنَ الصَّفَا حَتَّى إِذَا بَلَغَتِ الوَادِي ، رَفَعَت طَرفَ دِرْعِهَا ، ثُمَّ سَعَتْ سَعْيَ الإنْسَانِ المَجْهُودِ حَتَّى جَاوَزَتِ الوَادِي ، ثُمَّ أتَتِ المَرْوَةَ فَقَامَتْ عَلَيْهَا ، فَنَظَرَتْ هَلْ تَرَى أحَداً ؟ فَلَمْ تَرَ أَحَداً ، فَفَعَلَتْ ذَلِكَ سَبْعَ مَرَّاتٍ . قَالَ ابن عباس رضي الله عنهما : قَالَ النبيُّ صلى الله عليه وسلم : (( فَلذَلِكَ سَعْيُ النَّاسِ بَيْنَهُمَا )) ، فَلَمَّا أَشْرَفَتْ عَلَى المَرْوَةِ سَمِعَتْ صَوْتاً ، فَقَالَتْ : صَهْ – تُريدُ نَفْسَهَا – ثُمَّ تَسَمَّعَتْ ، فَسَمِعَتْ أَيضاً ، فَقَالَتْ : قَدْ أسْمَعْتَ إنْ كَانَ عِنْدَكَ غَوَاثٌ ، فَإذَا هِيَ بِالمَلَكِ عِنْدَ مَوْضِعِ زَمْزَمَ ، فَبَحَثَ بِعَقِبِهِ – أَوْ قَالَ بِجَنَاحِهِ – حَتَّى ظَهَرَ المَاءُ ، فَجَعَلَتْ تُحَوِّضُهُ وَتَقُولُ بِيَدِهَا هَكَذَا ، وَجَعَلَتْ تَغْرِفُ مِنَ المَاءِ في سِقَائِهَا وَهُوَ يَفُورُ بَعْدَ مَا تَغْرِفُ . وفي رواية : بِقَدَرِ مَا تَغْرِفُ . قَالَ ابن عباس رضي الله عنهما : قَالَ النبيُّ صلى الله عليه وسلم : (( رَحِمَ اللهُ أُمَّ إسْمَاعِيلَ لَوْ تَرَكَتْ زَمْزَمَ – أَوْ قَالَ لَوْ لَمْ تَغْرِفْ مِنَ المَاءِ - لَكَانَتْ زَمْزَمُ عَيْناً مَعِيناً )) قَالَ : فَشَرِبَتْ وَأرْضَعَتْ وَلَدَهَا ، فَقَالَ لَهَا المَلَكُ : لاَ تَخَافُوا الضَّيْعَةَ فَإنَّ هاهُنَا بَيْتاً للهِ يَبْنِيهِ هَذَا الغُلاَمُ وَأَبُوهُ ، وإنَّ اللهَ لاَ يُضَيِّعُ أهْلَهُ ، وكان البَيْتُ مُرْتَفِعاً مِنَ الأرْضِ كَالرَّابِيَةِ ، تَأتِيهِ السُّيُولُ ، فَتَأخُذُ عَنْ يَمِينِهِ وَعَنْ شِمَالِهِ ، فَكَانَتْ كَذَلِكَ حَتَّى مَرَّتْ بِهِمْ رُفْقَةٌ مِنْ جُرْهُمٍ ، أَوْ أهْلُ بَيْتٍ مِنْ جُرْهُمٍ مُقْبِلينَ مِنْ طَرِيقِ كَدَاءَ ، فَنَزلُوا في أسْفَلِ مَكَّةَ ؛ فَرَأَوْا طَائِراً عائِفاً ، فَقَالُوا : إنَّ هَذَا الطَّائِرَ لَيَدُورُ عَلَى مَاءٍ، لَعَهْدُنَا بهذا الوَادِي وَمَا فِيهِ مَاء. فَأَرْسَلُوا جَرِيّاً أَوْ جَرِيَّيْنِ ، فَإذَا هُمْ بِالمَاءِ . فَرَجَعُوا فَأَخْبَرُوهُمْ ؛ فَأَقْبَلُوا وَأُمُّ إسْمَاعِيلَ عِنْدَ المَاءِ ، فقالوا : أتَأذَنِينَ لَنَا أنْ نَنْزِلَ عِنْدَكِ ؟ قَالَتْ : نَعَمْ، وَلَكِنْ لاَ حَقَّ لَكُمْ في المَاءِ، قَالُوا : نَعَمْ . قَالَ ابن عباس : قَالَ النبيُّ صلى الله عليه وسلم : (( فَألْفَى ذَلِكَ أُمَّ إسْمَاعِيلَ ، وهي تُحِبُّ الأنْسَ )) فَنَزَلُوا ، فَأرْسَلُوا إِلَى أهْلِهِمْ فَنَزَلُوا مَعَهُمْ ، حَتَّى إِذَا كَانُوا بِهَا أهْلَ أبْيَاتٍ وَشَبَّ الغُلاَمُ وَتَعَلَّمَ العَرَبِيَّةَ مِنْهُمْ ، وَأنْفَسَهُمْ وَأَعْجَبَهُمْ حِيْنَ شَبَّ ، فَلَمَّا أدْرَكَ زَوَّجُوهُ امْرَأةً مِنْهُمْ : وَمَاتَتْ أُمُّ إسْمَاعِيلَ ، فَجَاءَ إبْرَاهِيمُ بَعْدَما تَزَوَّجَ إسْمَاعِيلُ يُطَالِعُ تَرِكَتَهُ ، فَلَمْ يَجِدْ إسْمَاعِيلَ ؛ فَسَأَلَ امْرَأتَهُ عَنْهُ فَقَالَتْ : خرَجَ يَبْتَغِي لَنَا - وفي روايةٍ : يَصِيدُ لَنَا - ثُمَّ سَأَلَهَا عَنْ عَيْشِهِمْ وَهَيْئَتِهِمْ ، فَقَالَتْ : نَحْنُ بِشَرٍّ ، نَحْنُ فِي ضِيقٍ وَشِدَّةٍ ؛ وَشَكَتْ إِلَيْهِ ، قَالَ : فَإذَا جَاءَ زَوْجُكِ اقْرَئِي عَلَيْهِ السَّلاَمَ ، وَقُولِي لَهُ يُغَيِّرْ عَتَبَةَ بَابِهِ . فَلَمَّا جَاءَ إسْمَاعِيلُ كَأَنَّهُ آنَسَ شَيْئاً ، فَقَالَ : هَلْ جَاءكُمْ مِنْ أحَدٍ ؟ قَالَتْ : نَعَمْ ، جَاءنا شَيْخٌ كَذَا وَكَذَا ، فَسَأَلَنَا عَنْكَ فَأَخْبَرْتُهُ ، فَسَأَلَنِي : كَيْفَ عَيْشُنَا ، فَأَخْبَرْتُهُ أَنَّا في جَهْدٍ وَشِدَّةٍ . قَالَ : فَهَلْ أَوْصَاكِ بِشَيءٍ ؟ قَالَتْ : نَعَمْ ، أَمَرَنِي أنْ أقْرَأَ عَلَيْكَ السَّلاَمَ ، وَيَقُولُ : غَيِّرْ عَتَبَةَ بَابِكَ ، قَالَ : ذَاكَ أبِي وَقَدْ أَمَرَنِي أنْ أُفَارِقَكِ ! الْحَقِي بِأَهْلِكِ . فَطَلَّقَهَا وَتَزَوَّجَ مِنْهُمْ أُخْرَى ، فَلَبِثَ عَنْهُمْ إِبْرَاهِيمُ مَا شَاءَ اللهُ ، ثُمَّ أَتَاهُمْ بَعْدُ فَلَمْ يَجِدْهُ ، فَدَخَلَ عَلَى امْرَأتِهِ فَسَألَ عَنْهُ . قَالَتْ : خَرَجَ يَبْتَغِي لَنَا قَالَ : كَيفَ أنْتُمْ ؟ وَسَأَلَهَا عَنْ عَيْشِهِمْ وَهَيْئَتِهِمْ ، فَقَالَتْ : نَحْنُ بِخَيرٍ وَسَعَةٍ ، وَأَثْنَتْ عَلَى اللهِ . فَقَالَ : مَا طَعَامُكُمْ ؟ قَالَتْ : اللَّحْمُ ، قَالَ : فمَا شَرَابُكُمْ ؟ قَالَت : الماءُ ، قَالَ : اللَّهُمَّ بَارِكْ لَهُمْ فِي اللَّحْمِ وَالمَاءِ. قَالَ النَّبيُّ صلى الله عليه وسلم : وَلَمْ يَكُنْ لَهُمْ يَوْمَئِذٍ حَبٌّ وَلَوْ كَانَ لَهُمْ دَعَا لَهُمْ فِيهِ، قَالَ : فَهُمَا لاَ يَخْلُو عَلَيْهِمَا أَحَدٌ بِغَيْرِ مَكَّةَ إِلاَّ لَمْ يُوَافِقَاهُ .

وَفِي رواية : فجاء فَقَالَ : أيْنَ إسْمَاعِيلُ ؟ فَقَالَتْ امْرأتُهُ : ذَهَبَ يَصِيدُ ؛ فَقَالَتْ امْرَأتُهُ : ألاَ تَنْزِلُ ، فَتَطْعَمَ وَتَشْرَبَ ؟ قَالَ : وَمَا طَعَامُكُمْ وَمَا شَرَابُكُمْ ؟ قَالَتْ : طَعَامُنَا اللَّحْمُ وَشَرَابُنَا المَاءُ، قَالَ : اللَّهُمَّ بَارِكْ لَهُمْ فِي طَعَامِهِمْ وَشَرابِهِمْ . قَالَ : فَقَالَ أَبُو القاسم صلى الله عليه وسلم : بَرَكَةُ دَعوَةِ إبْرَاهِيمَ . قَالَ : فإذَا جَاءَ زَوْجُكِ فَاقْرَئِي عَلَيْهِ السَّلاَمَ وَمُرِيِهِ يُثَبِّتُ عَتَبَةَ بَابِهِ. فَلَمَّا جَاءَ إسْمَاعِيلُ قَالَ: هَلْ أتاكُمْ مِنْ أحَدٍ ؟ قَالَتْ : نَعَمْ ، أتانَا شَيْخٌ حَسَنُ الهَيْئَةِ ، وَأثْنَتْ عَلَيْهِ ، فَسَألَنِي عَنْكَ فَأَخْبَرتُهُ ، فَسَألَنِي كَيْفَ عَيْشُنَا فَأخْبَرْتُهُ أَنَّا بِخَيْرٍ . قَالَ : فَأوْصَاكِ بِشَيءٍ ؟ قَالَتْ : نَعَمْ ، يَقْرَأُ عَلَيْكَ السَّلاَمَ وَيَأمُرُكَ أَنْ تُثَبِّتَ عَتَبَةَ بَابِكَ . قَالَ : ذَاكَ أبِي ، وأنْتِ العَتَبَةُ ، أمَرَنِي أنْ أُمْسِكَكِ . ثُمَّ لَبِثَ عَنْهُمَ مَا شَاءَ اللهُ ، ثُمَّ جَاءَ بَعدَ ذَلِكَ وإسْمَاعِيلُ يَبْرِي نَبْلاً لَهُ تَحْتَ دَوْحَةٍ قَريباً مِنْ زَمْزَمَ ، فَلَمَّا رَآهُ قَامَ إِلَيْهِ ، فَصَنَعَا كَمَا يَصْنَعُ الوَالِدُ بِالوَلَدِ وَالوَلَدُ بِالوَالدِ . قَالَ : يَا إسْمَاعِيلُ ، إنَّ اللهَ أمَرَنِي بِأمْرٍ ، قَالَ : فَاصْنَعْ مَا أمَرَكَ رَبُّكَ ؟ قالَ : وَتُعِينُنِي ، قَالَ : وَأُعِينُكَ ، قَالَ : فَإنَّ اللهَ أمَرَنِي أَنْ أَبْنِي بَيْتاً هاهُنَا ، وأشَارَ إِلَى أكَمَةٍ مُرْتَفِعَةٍ عَلَى مَا حَوْلَهَا ، فَعِنْدَ ذَلِكَ رَفَعَ القَوَاعِدَ مِنَ البَيْتِ ، فَجَعَلَ إسْمَاعِيلُ يَأتِي بِالحِجَارَةِ وَإبْرَاهِيمُ يَبْنِي حَتَّى إِذَا ارْتَفَعَ البِنَاءُ ، جَاءَ بِهذَا الحَجَرِ فَوَضَعَهُ لَهُ فَقَامَ عَلَيْهِ ، وَهُوَ يَبْنِي وَإسْمَاعِيلُ يُنَاوِلُهُ الحجارة وَهُمَا يَقُولاَنِ : [ رَبَّنَا تَقَبَّلْ مِنَّا إنَّكَ أنْتَ السَّمِيعُ العَلِيمُ ] [ البقرة : 127 ] .

وفي روايةٍ : إنَّ إبْرَاهِيمَ خَرَجَ بِإسْمَاعِيلَ وَأُمِّ إسْمَاعِيلَ، مَعَهُمْ شَنَّةٌ فِيهَا مَاءٌ ، فَجَعَلَتْ أُمُّ إسْمَاعِيلَ تَشْرَبُ مِنَ الشَّنَّةِ فَيَدِرُّ لَبَنُهَا عَلَى صَبِيِّهَا ، حَتَّى قَدِمَ مَكَّةَ ، فَوَضَعَهَا تَحْتَ دَوْحَةٍ ، ثُمَّ رَجَعَ إبْرَاهِيمُ إِلَى أهْلِهِ ، فَاتَّبَعَتْهُ أُمُّ إسْماعيلَ حَتَّى لَمَّا بَلَغُوا كَدَاءَ نَادَتْهُ مِنْ وَرَائِهِ : يَا إبْرَاهِيمُ إِلَى مَنْ تَتْرُكُنَا ؟ قَالَ : إِلَى اللهِ ، قَالَتْ : رَضِيْتُ باللهِ ، فَرَجَعَتْ وَجَعَلَتْ تَشْرَبُ مِنَ الشِّنَّةِ وَيَدُرُّ لَبَنُهَا عَلَى صَبِيِّهَا ، حَتَّى لَمَّا فَنِيَ المَاءُ قَالَتْ : لَوْ ذَهَبْتُ فَنَظَرْتُ لَعَلِّي أُحِسُّ أَحَداً . قَالَ : فَذَهَبَتْ فَصَعِدَتِ الصَّفَا ، فَنَظَرَتْ وَنَظَرَتْ هَلْ تُحِسُّ أحداً ، فَلَمْ تُحِسَّ أَحَداً ، فَلَمَّا بَلَغَتِ الوَادِي سَعَتْ ، وأتَتِ المَرْوَةَ ، وَفَعَلَتْ ذَلِكَ أشْوَاطَاً ، ثُمَّ قَالَتْ : لَوْ ذَهَبْتُ فَنَظَرْتُ مَا فَعَلَ الصَّبِيُّ، فَذَهَبَتْ فَنَظَرَتْ فَإذَا هُوَ عَلَى حَالِهِ ، كَأنَّهُ يَنْشَغُ لِلْمَوْتِ ، فَلَمْ تُقِرَّهَا نَفْسُهَا فَقَالَتْ : لَوْ ذَهَبْتُ فَنَظَرْتُ لَعَلِّي أُحِسُّ أحَداً ، فَذَهَبَتْ فَصَعِدَتِ الصَّفَا ، فَنَظَرَتْ ونظَرتْ فَلَمْ تُحِسَّ أَحَداً ، حَتَّى أتَمَّتْ سَبْعاً ، ثُمَّ قَالَتْ : لَوْ ذَهَبْتُ فَنَظَرْتُ مَا فَعَلَ ، فَإذَا هِيَ بِصَوْتٍ ، فَقَالَتْ : أَغِثْ إنْ كَانَ عِنْدَكَ خَيْرٌ ، فَإذَا جِبْرِيلُ فَقَالَ بِعقِبِهِ هَكَذَا ، وَغَمَزَ بِعَقِبِهِ عَلَى الأرْضِ ، فَانْبَثَقَ المَاءُ فَدَهِشَتْ أُمُّ إسْمَاعِيلَ ، فَجَعَلَتْ تَحْفِنُ … وَذَكَرَ الحَديثَ بِطُولِهِ ، رواه البخاري بهذه الروايات كلها .

Amesema Ibn 'Abbaas (Radhwiya Allaahu 'anhumaa): Alikuja Ibraahiym ('Alayhis salaam) na Umm Isma'iyl (ambaye ni Hajar) pamoja na mtoto wake, Isma'iyl ambaye alikuwa ananyonya na kuwaacha chini ya mti mkubwa karibu na Nyumba (yaani Ka'bah), juu kidogo na chemchemi ya Zamzam katika sehemu ya juu ya Msikiti. Na wakati huo kulikuwa hakuna yeyote katika mji wa Makkah wala maji, naye akawaacha huko. Aliwaachia mfuko wa tende na kiriba cha maji. Kisha akaondoka kufuata athari yake (njia yake) kuondoka, Umm Isa'iyl alimfuata na huku anamuuliza: "Ee Ibraahiym! Unakwenda wapi na kutuacha sisi katika bonde hili ambalo halina watu wala kitu chochote?" Alikariri swali hilo mara nyingi, lakini Ibraahiym ('Alayhis salaam) akawa hamtizami. Akamuuliza: "Je, Allaah Ndiye Aliyekuamuru kufanya hivi?" Akajibu: "Ndio." Akasema: "Hivyo, Allaah Hatatuacha kuangamia." Kisha akarudi. Ibraahiym ('Alayhis salaam) akaondoka mpaka akafika sehemu inayoitwa Thaniyyah ambapo walikuwa hawamuoni, na hapo alielekea Ka'bah kisha akaomba kwa dua hizi kwa kunyanyua mikono yake na kusema: "Rabb wetu! Hakika mimi nimewaweka baadhi ya dhuria wangu katika bonde lisilokuwa na mmea wowote, kwenye Nyumba Yako Tukufu (Al-Ka’bah), ee Rabb wetu ili wasimamishe Swalaah. Basi Zijaalie nyoyo za watu zielekee kwao na Uwaruzuku mazao ili wapate kushukuru." [Ibraahiym: 37]Umm Isma'iyl akawa anamnyonyesha Isma'iyl na akawa anakunywa kutoka katika yake maji mpaka yakaisha katika kile kiriba, hapo akaanza kusikia kiu na mtoto wake pia akaanza kusikia kiu na mtoto wake pia akawa anasikia kiu. Alianza kumuangalia mtoto wake ambaye kwa ajili ya kiu alianza kugaagaa - au alisema: Alirusha mateke. Umm Isma'iyl akaondoka hapo kwa kuchukia kumuangalia (mwanae katika hali hiyo) na akaona Swafaa ni jabali lililo karibu naye katika ardhi. Aliukwea, kisha akalielekea bonde na kuanza kutizama kama anamuona mtu yeyote, lakini hakumuona. Akateremka Swafaa mpaka akafika kwenye bonde, alinyanyua ncha ya nguo yake, kisha akaanza kukimbia, mbio za mtu mwenye dhiki mpaka akalivuka bonde na kufika mlima wa Marwah na kuukwea. Alitizama kama atamuona yeyote lakini hakumuona yeyote. akafanya hivyo (kutembea na kukimbia baina ya Swafaa na Marwah) mara saba. Akasema Ibn 'Abbaas  (Radhwiya Allaahu 'anhumaa): Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: "Hiyo ndiyo Sa'yi ya watu baina (hayo majabali mawili)." Mwisho alipofika Marwah (kwa mara ya saba) mara alisikia sauti, akasema: "Sikiliza" - akimaanisha nafsi yake, - kisha akasikiliza kwa makini, akaisikia tena, akasema: "Nimesikia sauti Yako, natamani kuwa utakuwa na usaidizi (kwangu)." Mara akamuona Malaaikah katika sehemu ya Zamzam, ambaye aliigonga ardhi kwa kisigino chake - au alisema: Kwa mbawa zake mpaka yakatoka maji. Hajar akaanza kuyafanyia kibirika kwa mikono yake ili kuyakinga na kujaza kiriba chake kutumia mikono yake nayo yakawa yanatoka kwa nguvu zaidi. 

Na katika riwaayah nyingine: "Kwa kiasi cha alivyokuwa akitia." Akasema Ibn 'Abbaas (Radhwiya Allaahu 'anhumaa): Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: "Allaah Amrehemu Umm Isma'iyl, lau angeiacha Zamzam - au alisema: Lau kama hangekuwa ni mwenye kuteka na kutia kwenye kiriba chake, basi Zamzam ingekuwa ni jicho la maji (chemchemi) kubwa." Akasema: "Akanywa na kumuonyesha mtoto wake." Akamwambia Malaaikah: "Usihofu kuangamia, kwani hapa kutakua na Nyumba ya Allaah (Baytu-Allaah) ambayo itajengwa na huyu mtoto pamoja na babake na hakika Allaah Hatawaacha watu wake (wa sehemu hiyo) kuangamia." Ka'bah wakati huo ilikuwa katika sehemu iliyonyanyuka, kama mfano wa Kuba. Hivyo, maji ya mafuriko yalikuwa yakipita kuliani na kushotoni mwake. Familia hii (ya mama na mtoto wake) walibaki katika hali hii kwa wakati mrefu mpaka msafara wa Jurhum au watu wa nyumba ya Jurhum (familia ya Jurhum) waliotoka katika njia ya Kadaa'a na wakapiga kambi yao katika sehemu ya chini ya Makkah. Wakaona kundi la ndege likiruka na kuzunguka zunguka, wakasema: "Hakika hawa ndege wanazunguka juu ya maji." Sisi tumekuwa tukipita katika bonde hili kwa kipindi kirefu lakini hakukuwa na maji. Wakamtuma mtu wawili ili kuchunguza, nao wakayakuta maji. Walirudi na kuwapasha habari kuhusu hilo. Watu wa msafara walikuja na kumkuta Umm Isma'iyl kwenye maji hayo. Wakamwambia: "Je, utaturuhusu tukae hapa kwako?" Akasema: "Ndio, lakini hamuna haki yoyote na maji." Wakasema: "Tumekubali hilo." Akasema Ibn 'Abbaas (Radhwiya Allaahu 'anhumaa): Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: "Akapata Umm Isma'iyl lile alilokuwa akilitaka, kwani alikuwa anapenda watu (jamii)." Hao wageni wakashukia hapo na wakapeleka ujumbe kwa watu wao ili waje wakae nao, nao wakafanya hivyo na mara makazi hao mapya yakawa na familia kadhaa. Na kijana (Isma'iyl) akakua na kujifunza lugha ya Kiarabu kutoka kwao (wageni). Aliinukia kuwa kijana mwenye umbile na sura nzuri na kupendwa na kila mmoja. Alipofikia makamu ya kuoa walimuozesha binti yao. Katika kipindi hichi Umm Isma'iyl aliaga dunia. Baada ya kuoa, Ibraahiym ('Alayhis salaam) alikuja kutafuta kitu ambacho alikiacha huko, lakini Isma'iyl hakuwepo, hivyo alimuuliza mkewe Isma'iyl (ambaye ni mkwewe) kuhusu mumewe. Mke akasema: "Ametoka kututafutia chakula - na katika riwaayah nyengine: Amekwenda mawindoni." Kisha akamuuliza kuhusu maisha yao na hali zao. Akasema: "Sisi tuko katika dhiki na shida", na akaanza kumlalamikia. Akamwambia: "Akija mumeo, nitolee salamu kwake na mwambie abadilishe kizingiti cha mlango wake." Aliporudi Isma'iyl, ni kana kwamba alimaizi kitu, akauliza: "Je, amekujieni mtu yeyote?" Akasema mkewe: "Ndio, alikuja mzee kadhaa na kadhaa ambaye alituuliza juu yako nami nikamueleza. Aliuliza: Kuhusu maisha yetu, nami nikampasha habari kuwa sisi tunajikokota na tuko katika shida." Akauliza: "Je, alikuusia kitu chochote?" Akasema: "Ndio, ameniamuru nikutolee salamu na anasema: 'Badilisha kizingiti cha mlango wako." Akasema: "Huyo ni baba yangu na ameniamuru nikuache, hivyo rudi kwa wazazi wako." Isma'iyl akamtaliki mkewe huyo na akaowa mwanamke mwengine. Nabiy Ibraahiym ('Alayhis salaam) akakaa bila kuwazuru kwa kitambo kirefu kama alivyopenda Allaa, kisha akawatembelea, lakini pia asimpate mtoto wake, Isma'iyl ('Alayhis salaam). Akaingia kwa mke wa mtoto wake na kumuuliza kuhusu mumewe. Akasema: "Ametoka kututafutia riziki." Akauliza: "Je, nyinyi muko vipi?" Na pia akamuuliza kuhusu maisha yao na hali zao. Akamjibu: "Sisi tuko katika kheri na tuna wasaa (ukunjufu) na akamsifu Allaah Ta'aalaa." Akauliza tena: "Munakula nini?" Akamjibu: "Tunakula nyama." Akauliza: "Kinywaji chenu ni kipi?" Akasema: "Maji." Akasema ('Alayhis salaam): "Ee Rabb wangu! Wabarikie wao katika hiyo nyama na maji." Akasema Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Na hakukuwa na nafaka yoyote wakati huo (katika mji wa Makkah) na lau kungekuwepo basi pia angewaombea (ili vibarikiwe)." Akasema: "Hiyo ndiyo sababu ya kuwa hakuna yeyote isipokuwa watu wa Makkah ndio wanaishi na nyama na maji tu, na hivi haviwafai wengine." 

Na katika riwaayah nyengine: Alikuja Nabiy Ibraahiym ('Alayhis salaam) na kuuliza: "Yu wapi Isma'iyl?" Akamjibu mkewe: "Amekwenda kuwinda." Akasema mkewe: "Hivi basi huteremki, ukala na kunywa?" Akasema: "Na chakula na kinywaji chenu ni nini?" Akamjibu: "Chakula chetu ni nyama na kunywaji chetu ni maji." Akasema: "Ee Rabb wangu! Wabarikie chakula na kinywaji chao." Akasema: Hapo akasema Abul Qaasim (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Baraka kwa dua ya Ibraahiym (ndio Makkah kunapatikana chakula na maji mengi)." Akamwambia: "Akija mumeo, nitolee salamu na mwambie akitilie nguvu kizingiti cha mlango wake." Aliporudi Isma'iyl aliuliza: "Je, amekujieni mtu yeyote?" Akasema mkewe: "Ndio, alikuja mzee mwenye umbile zuri na akamsifu baba mkwe wake. Aliniuliza kukuhusu nami nikampasha habari. Aliniuliza kuhusu maisha yetu na nikamjulisha kuwa tuko katika kheri." Akauliza: Je, amekuusia chochote?" Akasema: "Ndio, anakutolea salamu na anakuamuru ukidhibiti kizingiti cha mlango wako." Akasema: "Huyo ni baba yangu na wewe ndiye kizingiti aliyeniamuru nikukamate (nibakie na wewe)." Kisha Nabiy Ibraahiym ('Alayhis salaam) alikaa kwa kipindi kirefu bila kuwazuru kama alivyopenda Allaah, kisha akaja baada ya muda huo, wakati ambapo Isma'iyl alikuwa amekaa chini ya mti mkubwa uliokuwa karibu na chemchemi ya Zamzam akitengeneza mishale yake. Alipomuona, aliinuka na akafanya kama vile mtoto anavyomfanyia baba yake na baba kwa mwanawe. Akamwambia: "Ee Isma'iyl! Hakika Allaah Ameniamuru kutekeleza jambo Fulani." Akasema: "Hivyo, tekeleza kama alivyokuamuru Rabb Wako." Akasema: Akamwambia: "Nawe utanisaidia?" Akamjibu: "Ndio, nitakusaidia." Akasema: "Hakika Allaah Ameniamuru nijenge Nyumba (yaani Ka'bah) hapa." Na akaashiria kwenye ile sehemu iliyonyanyuka mfano wa kuba na pembezoni mwake. Na katika sehemu hiyo ndiyo walinyanyua nguzo za Nyumba hiyo. Ikawa Isma'iyl anakuja na mawe na Ibraahiym ('Alayhis salaam) anajenga (kwa kuyapanga hayo mawe) na kuta zake ziliponyanyuka, Isma'iyl alileta jiwe na kumuekea Ibraahiym ('Alayhis salaam) ambalo naye alilitumia kusimama juu yake (hiyo ndiyo sehemu inayoitwa Maqaam Ibraahiym). Aliendelea kujenga, huku Isma'iyl anamletea mawe, na huku wanaomba: "Rabb wetu, Tutaqabalie, hakika Wewe Ni Mwenye Kusikia yote, Mjuzi wa yote." [Al-Baqarah: 127]. 

Na katika riwaayah nyengine: "Hakika Ibraahiym ('Alayhis salaam) alitoka wakiwa na kiriba cha maji. Akawa Umm Isma'iyl anakunywa maji kutoka katika kiriba hicho na hivyo kumwezesha kumnyonyesha mtoto wake mpaka wakafika Makkah. Hapo alimuweka mkewe chini ya mti mkubwa, kisha Ibraahiym ('Alayhis salaam) akarudi kwa familia yake. Umm Isma'iyl alimfuata mpaka wakafika Kadaa`a na hapo alimuita kutoka nyuma yake: "Ee Ibraahiym! Unatuachia (chini ya uangalizi wa) nani?" Akasema: "Nawaacha chini ya uangalizi wa Allaah." Akasema: "Timeridhia kuwa chini ya ungalizi wa Allaah." Hapo alirudi na akawa anakunywa maji kutoka kwenye kiriba, na hivyo kumuezesha kutoa maziwa kwa ajili ya kumnyonyesha mtoto wake mpaka yalipomalizika. Akasema (katika nafsi yake): "Lau nitakwenda kuangalia, huenda nikamuona yeyote." Akasema: "akaenda akaukwea mlima wa Swafaa, akatizama na kutizama kama atamuona mtu yeyote, lakini hakumuona yeyote. Alishuka chini na alipofika kwenye bonde alianza kukimbia mpaka akafika Marwah, akapiga mizunguko kadhaa." Kisha akasema: "Lau ningekwenda kuangalia mtoto anafanya nini?" Akaenda kumuangalia, akamkuta katika hali ya kuwa na uchungu wa mauti. Hakuweza kuvumilia mandhari hiyo katika nafsi yake. Akasema (katika nafsi yake): "Lau ningekwenda kutizama tena huenda nikamuona mtu yeyeote." Akaenda na kuukwea mlima Swafaa, akatizama mara kadhaa lakini bila ya mafanikio ya kumuona mtu yeyeote mpaka akafikisha mizunguko saba (ya kukimbia baina ya Swafaa na Marwah). Kisha akasema: "Lau ningekwenda kumtizama mtoto yu hali gani?" Mara akasikia sauti, akasema: "Nipatie msaada ikiwa umekuja na kheri yoyote." Jibriyl ('Alayhis salaam) alifika hapo na kupiga ardhi maji yalianza kutoka, kutoka chini ya ardhi. Umm Isma'iyl alishangazwa sana na hapo hapo akaanza kuyazuia (kwa kuyaekea mipaka ili yahifadhike na yasitoweke)."... Na akaitaja Hadiyth kwa urefu wake. [Al-Bukhaariy kwa riwaayah hizi zote]

 

Hadiyth – 61

وعن سعيد بن زيد رَضِيَ اللهُ عنه قَالَ : سَمِعْتُ رَسُولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم يقولُ : (( الكَمْأَةُ مِنَ المَنِّ ، وَمَاؤُهَا شِفَاءٌ لِلْعَيْنِ )) متفق عَلَيْهِ .

Amesema Sa'iyd bin Zayd (Radhwiya Allaahu 'anhu): Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: "Kam`ah inatokana na Manna, na maji yake ni dawa ya jicho." [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

 

 

 

Share