Skip navigation.
Home kabah

20 Dua'a Za Wakati Wa Kusujudu

(41)

سُبْـحانَ رَبِّـيَ الأَعْلـى  

“Ametakasika Mola wangu aliyejuu" 

(Utasema hivi mara tatu)

(42)

سُبْـحانَكَ اللّهُـمَّ رَبَّـنا وَبِحَـمْدِكَ ، اللّهُـمَّ اغْفِرْ لي

“Kutakasika ni Kwako, Ewe Mwenyezi Mungu , Mola wetu, na sifa njema zote ni Zako, Ewe Mwenyezi Mungu  nisamehe”

(43)

سُبـّوحٌ قُـدّوس، رَبُّ الملائِكَـةِ وَالـرُّوح

“Mwingi wa kutakaswa Mtakatifu, Mola wa malaika na Jibriil”

(44)

اللّهُـمَّ لَكَ سَـجَدْتُ وَبِـكَ آمَنْـت ، وَلَكَ أَسْلَـمْت ، سَجَـدَ وَجْهـي للَّـذي خَلَقَـهُ وَصَـوَّرَهُ وَشَقَّ سَمْـعَـهُ وَبَصَـرَه ، تَبـارَكَ اللهُ أَحْسـنُ الخـالِقيـن

“Ewe Mwenyezi Mungu  Kwako nimesujudu, na Wewe nimekuamini, na Kwako nimesilimu, umesujudu uso wangu kumsujudia  aliyeuumba na akautia sura na akaupasua usikizi wake na uwoni wake, Ametukuka Mwenyezi Mungu  Mbora wa waumbaji”

(45)

سُبْـحانَ ذي الْجَبَـروت ، والمَلَكـوت ، والكِبْـرِياء ، وَالعَظَمَـه

“Ametakasika Mwenye Utawala, na Ufalme, na Ukubwa, na Utukufu”

(46)

اللّهُـمَّ اغْفِـرْ لي ذَنْـبي كُلَّـه ، دِقَّـهُ وَجِلَّـه ، وَأَوَّلَـهُ وَآخِـرَه وَعَلانِيَّتَـهُ وَسِـرَّه

“Ewe Mwenyezi Mungu nisamehe dhambi zangu zote, ndogo na kubwa, za mwanzo na za mwisho, za dhahiri na za siri”

(47)

اللّهُـمَّ إِنِّـي أَعـوذُ بِرِضـاكَ مِنْ  سَخَطِـك ، وَبِمعـافاتِـكَ مِنْ عُقوبَـتِك ، وَأَعـوذُ بِكَ مِنْـك ، لا أُحْصـي ثَنـاءً عَلَـيْك ، أَنْـتَ كَمـا أَثْنَـيْتَ عَلـى نَفْسـِك

“Ewe Mwenyezi Mungu  hakika mimi najilinda kwa radhi Zako kutokana na hasira zako, na kwa msamaha wako kutokana na adhabu yako, na najilinda Kwako unihifadhi na Wewe, mimi siwezi kuzidhibiti sifa Zako, Wewe ni kama ulivyojisifu Mwenyewe”