25 Dua'a Baada Ya Tashahhud Kabla Ya Salaam
(55)
اللّهُـمَّ إِنِّـي أَعـوذُ بِكَ مِـنْ عَذابِ القَـبْر، وَمِـنْ عَذابِ جَهَـنَّم، وَمِـنْ فِتْـنَةِ المَحْـيا وَالمَمـات، وَمِـنْ شَـرِّ فِتْـنَةِ المَسيحِ الدَّجّال
“Ewe Mwenyezi Mungu mimi nakutaka unihifadhi na adhabu za kaburi, na adhabu ya (moto wa) jahannam, na fitna ya uhai, na ya kufa, na shari ya fitna ya Masihi-dajjaal”
(56)
اللّهُـمَّ إِنِّـي أَعـوذُ بِكَ مِـنْ عَذابِ القَـبْر ، وَأَعـوذُ بِكَ مِـنْ فِتْـنَةِ المَسيحِ الدَّجّـال ، وَأَعـوذُ بِكَ مِـنْ فِتْـنَةِ المَحْـيا وَالمَمـات . اللّهُـمَّ إِنِّـي أَعـوذُ بِكَ مِنَ المَأْثَـمِ وَالمَغْـرَم
“Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi najilinda Kwako kutokana na adhabu ya kaburi, na najilinda Kwako kutokana na fitna ya Masihi-dajjaal, na najilinda Kwako kutokana na fitna ya uhai na ya mauti, Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi najilinda Kwako kutokana na dhambi na deni”
(57)
اللّهُـمَّ إِنِّـي ظَلَـمْتُ نَفْسـي ظُلْمـاً كَثـيراً وَلا يَغْـفِرُ الذُّنـوبَ إِلاّ أَنْت ، فَاغْـفِر لي مَغْـفِرَةً مِنْ عِنْـدِك وَارْحَمْـني، إِنَّكَ أَنْتَ الغَـفورُ الرَّحـيم
“Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi nimejidhulumu nafsi yangu, dhulma kubwa, na hasamehe madhambi ila Wewe, basi nisamehe msamaha kutoka Kwako, na unirehemu, hakika Wewe ni mwingi wa kusamehe, mwingi wa kurehemu”
(58)
اللّهُـمَّ اغْـفِرْ لي ما قَدَّمْـتُ وَما أَخَّرْت ، وَما أَسْـرَرْتُ وَما أَعْلَـنْت ، وَما أَسْـرَفْت ، وَما أَنْتَ أَعْـلَمُ بِهِ مِنِّي . أَنْتَ المُقَـدِّمُ، وَأَنْتَ المُـؤَخِّـرُ لا إِلهَ إِلاّ أَنْـت
“Ewe Mwenyezi Mungu nisamehe niliyoyatanguliza, na niliyoyachelewesha, na niliyoyafanya kisiri, na niliyoyafanya kwa dhahiri na niliyoruka mipaka, na ambayo Wewe unayajua zaidi kuliko mimi, Wewe ndiye mwenye kutanguliza na Wewe ndiye mwenye kuchelewesha, hakuna apasae kuabudiwa kwa haki ila Wewe.
(59)
اللّهُـمَّ أَعِـنِّي عَلـى ذِكْـرِكَ وَشُكْـرِك ، وَحُسْـنِ عِبـادَتِـك
“Ewe Mwenyezi Mungu nisaidie kukukumbuka, na kukushukuru, na uzuri wa kukuabudu”
(60)
اللّهُـمَّ إِنِّـي أَعوذُ بِكَ مِنَ البُخْـل، وَأَعوذُ بِكَ مِنَ الجُـبْن، وَأَعوذُ بِكَ مِنْ أَنْ أُرَدَّ إِلى أَرْذَلِ الـعُمُر، وَأََعوذُ بِكَ مِنْ فِتْنَـةِ الدُّنْـيا وَعَـذابِ القَـبْر .
“Ewe Mwenyezi Mungu najilinda Kwako kutokana na ubakhili, na najilinda kwako kutokana na uwoga, na najilinda kwako kutokana na kurudishwa kwenye umri duni, na najilinda kwako kutokana na fitna ya dunia na adhabu ya kaburi”
(61)
اللّهُـمَّ إِنِّـي أَسْأَلُـكَ الجَـنَّةَ وأََعوذُ بِـكَ مِـنَ الـنّار
“Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi nakuomba pepo na najilinda kwako kutokana na moto”
(62)
اللّهُـمَّ بِعِلْـمِكَ الغَـيْبِ وَقُـدْرَتِـكَ عَلـى الْخَلقِ أَحْـيِني ما عَلِـمْتَ الحـياةَ خَـيْراً لـي، وَتَوَفَّـني إِذا عَلِـمْتَ الوَفـاةَ خَـيْراً لـي، اللّهُـمَّ إِنِّـي أَسْـأَلُـكَ خَشْيَتَـكَ في الغَـيْبِ وَالشَّهـادَةِ، وَأَسْـأَلُـكَ كَلِمَـةَ الحَـقِّ في الرِّضـا وَالغَضَـب، وَأَسْـأَلُـكَ القَصْدَ في الغِنـى وَالفَقْـر، وَأَسْـأَلُـكَ نَعـيماً لا يَنْفَـد، وَأَسْـأَلُـكَ قُـرَّةَ عَيْـنٍ لا تَنْـقَطِعْ وَأَسْـأَلُـكَ الرِّضـا بَعْـدَ القَضـاء، وَأَسْـأَلُـكَ بًـرْدَ الْعَـيْشِ بَعْـدَ الْمَـوْت، وَأَسْـأَلُـكَ لَـذَّةَ النَّظَـرِ إِلـى وَجْـهِكَ وَالشَّـوْقَ إِلـى لِقـائِـك، في غَـيرِ ضَـرّاءَ مُضِـرَّة، وَلا فِتْـنَةٍ مُضـلَّة، اللّهُـمَّ زَيِّـنّا بِزينَـةِ الإيـمان، وَاجْـعَلنا هُـداةً مُهْـتَدين
“Ewe Mwenyezi Mungu , kwa ujuzi Wako wa mambo yaliyo fichikana, na uwezo Wako wa kuumba, niweke hai iwapo uhai ni bora kwangu, na nifishe iwapo kufa ni bora kwangu, Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi nakuomba khofu yako kwa siri na dhahiri na ninakuomba neno la haki wakati nimefurahi na wakati nimekasirika, na ninakuomba matumizi ya wastani wakati wa utajiri na wakati wa umaskini, na ninakuomba neema isiyokwisha na ninakuomba kituliza jicho (moyo) kisicho katika, na ninakuomba kuridhia baada yakuwa umeshanipangia, na ninakuomba maisha ya utulivu baada ya kufa, na ninakuomba ladha ya kukutizama uso Wako, na shauku ya kukutana nawe, pasina madhara yanayodhuru, wala fitna yenye kupoteza. Ewe Mwenyezi Mungu tupambe kwa kipambo cha imani, na tujaalie tuwe waongozi wenye kuongoka”.
(63)
اللّهُـمَّ إِنِّـي أَسْأَلُـكَ يا اللهُ بِأَنَّـكَ الواحِـدُ الأَحَـد ،الصَّـمَدُ الَّـذي لَـمْ يَلِـدْ وَلَمْ يولَدْ، وَلَمْ يَكـنْ لَهُ كُـفُواً أَحَـد ، أَنْ تَغْـفِرْ لي ذُنـوبي إِنَّـكَ أَنْـتَ الغَفـورُ الرَّحِّـيم
“Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi nakuomba, Ewe Mwenyezi Mungu kwa vile Wewe ni Mmoja ulie pekee, Mwenye kutegemewa kwa haja zote, ambae hakuzaa wala hakuzaliwa, na wala hakuna mfano wake na kitu chochote, nakuomba unisamehe makosa yangu hakika Wewe ni Mwingi wa kusamehe,, Mwenye kurehemu”
(64)
اللّهُـمَّ إِنِّـي أَسْأَلُـكَ بِأَنَّ لَكَ الْحَـمْدُ لا إِلـهَ إِلاّ أَنْـتَ وَحْـدَكَ لا شَـريكَ لَـكَ المَنّـانُ يا بَديـعَ السَّمواتِ وَالأَرْضِ يا ذا الجَلالِ وَالإِكْـرام، يا حَـيُّ يا قَـيّومُ إِنِّـي أَسْأَلُـكَ الجَـنَّةَ وَأَعـوذُ بِـكَ مِنَ الـنّار
“Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi nakuomba, kwa vile sifa njema zote ni Zako, hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki ila Wewe, hali yakuwa pekeyako, huna mshirika, mwingi wa kuneemesha. Ewe Mtangulizi (muumbaji) wa mbingu na ardhi (bila kuwa na mfano kabla), Ewe mwenye Utukufu na ukarimu, Ewe Ulie hai mwenye kusimama kwa dhati Yako, hakika mimi nakuomba pepo , na najilinda kwako kutokana na moto”
(65)
اللّهُـمَّ إِنِّـي أَسْأَلُـكَ بِأَنَّـي أَشْـهَدُ أَنَّـكَ أنْـتَ اللهُ لا إِلـهَ إِلاّ أَنْـت ، الأَحَـدُ الصَّـمَدُ الَّـذي لَـمْ يَلِـدْ وَلَمْ يولَـدْ ، وَلَمْ يَكـنْ لَهُ كُـفُواً أَحَـد .
“Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi nakuomba kwa vile ninakiri kwa hakika kwamba Wewe ni Mwenyezi Mungu hapana apasae kuabudiwa kwa haki ila Wewe, hali ya kuwa pekee, mwenye kutegemewa kwa haja zote, ambae hakuzaa wala hakuzaliwa, na wala hakuna mfano wake na kitu chochote”
- Login or register to post comments
- Email this page


